Friday, January 18, 2008

NANI ALISEMA NI TUZO YA OSCAR?




Baadhi ya Wasomaji wamezua mjadala usiokuwepo kuhusu tuzo ya Kanumba, hebu tuisome habari hii iliyoandikwa kuelezea tuzo hiyo, sioni mahali palipoandikwa kuwa KANUMBA AMEPEWA TUZO YA OSCAR...labda ni macho yangu..!

Msanii wa filamu nchini, Steven Kanumba mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akimwaga chozi la furaha nchini Marekani baada ya kupewa tuzo ya Best Tanzania Hollywood Achievement, kutoka Kampuni ya Universal Hollywood ya nchini humo.

Kanumba ambayealiwasiliana na mwandishi wetu kwa njia ya barua pepe alisema kuwa, amefurahi sana na hakuamini macho yake alipotembea juu ya red carpet (kapeti jekundu) kupokea tuzo hiyo.

“Kaka nina furaha sana usiku huu wa leo, nimepewa tuzo nyingine kama Best Tanzania Achievement Actor yaani muigizaji mwenye mafanikio kutoka Tanzania iliyotolewa na Kampuni ya Universal Hollywood, nimetembea juu ya kapeti jekundu huku machozi yakinitoka, kusema kweli siamini kilichotokea,” alisema Kanumba.

Alisema mara baada ya kumaliza zoezi la kupokea tuzo, waliandaliwa sherehe ya nguvu kwenye Ukumbi wa Aqua Lounge, Los Angeles ambapo ilihudhuriwa na mastaa kibao wa Hollywood.

Msanii huyo alisema kuwa, kwa muda mfupi aliokaa huko amejifunza mengi na ameweza kujichanganya na baadhi ya mastaa wanaoigiza sinema za kutisha duniani kama anavyoonekani akiwa amepozi nao kwenye picha ya ukurasa wa mbele.

Hii ni tuzo ya pili kwa msanii huyo kutunikiwa kutoka Marekani ambapo ya kwanza ni ya Johnwyne International Award.

Kanumba yuko nchini Marekani kwa takriban miezi mitatu sasa kwa mwaliko wa Kampuni ya Johnwyne ya Hollywood. (Source: www.globalpublisherstz.com)

7 comments:

Anonymous said...

yeye akitaka kutoa wasiwasi mbona katuma picha nyingi lakini hiyo ya akikanyaga red carpet hakuna au wakati anakabidhiwa mbona hakuna picha na ni tukio muhimu kupiga picha tunashangaa tunaona tu kasimama na kina pimbi wa USA eti amepewa award????? na pia ni lazima zishindane na cinema nyingine za tanzania aache ushamba hii ni dunia nyingine ya utandawazi yaani globalization, uwezi kuibuka na story tu ukaanza kusema ohh! hapana watu wanataka ukweli, na kama ungepiga picha na denzel mwenyewe si tungekoma sisi ushamba wewe umeenda kutembea kama wanavyokwenda wengine

Anonymous said...

E bwana, I wont mind usipotoa hii comment. WEwe ni mwandishi cheap. Mwenzio Michuzi kashtukia dili ndo maana hajabandika hiyo habari. Mrisho tuko Marekani so tunajua mambo yanavyoenda huku. Habari uliandika inaonyesha upeo wako mdogo wa uandishi. Unaonekana hujasafiri wewe, bado limbukeni. Huyo Kanumba anapenda sifa za bure, atkuharibia jina. Nenda blog ya Chemi Che Mponda uone alivyoi-present habari hiyo; anaonyesha kuelewa.

Anonymous said...

KUANZIA LEO, GLOBAL PUBLISHERS NA BLOG HII YA KWAKO NAONDOA KWENYE MY FAVORITE LIST YA BLOG NAZOZIPIGIA DEBE NA KUZITEMBELEA DAILY. IQ YAKO NDOGO

MDAU
SEATTLE, USA

Anonymous said...

Nyinyi waandishi wa udaku msifanye kila mtu hana upeo. Sijui labda kwakuwa wasomaji wenu wengi mnalenga tabaka fulani lakini haina maana muwe mnadanganya watu kama watoto.
Wewe mtu kapewa tuzo hana hata picha za siku ya tukio? ila ana picha akiwa amesimama na tuzo barabarani. au ndo alikabidhiwa hapo na huyo jamaa? Kupewa tuzo huwa linakuwa tukio maalum na lazima angepigwa picha, tena nyingi tuu.
Kwanini mnadanganyika kirahisi? najua mmesoma na mna uwezo wa kuchambua cha kuandika. Mnatufanya tuhoji kuhusu uwezo wenu. Searh on google. there is no such a thing.

Anonymous said...

na wewe acha ujinga,huo uandishi wako ni wa nini?ulisomea wapi?
ukweli ni hivi,hicho kidud alichoshika kanumba anachosema ni award aliyopewa inafanana na tuzo ya oscar,na hakuna mtu yeyote duniani mwenye kibali cha kutengeneza oscar inayofanana na ya oscar.hilo watu ndio wanalobisha,angeshika kidude chengine na kudanganya watanzania hapo kweli,lakini sio hiyo.
watanzania wanawaamini lakini mbona mnazidi kuwadanganya?
acheni kudanganywa kijinga,sasahivi watanzania wapo kila pande za dunia,wanajua kinachoendelea duniani,lazima kanumba aombe msamaha kwa uongo wake.

Anonymous said...

Kanumba kachemka... Hii si dunia ya kudanganya watu... Mrisho angalia ripoti za uongo zinaweza kukuharibia credibility yako. Mwambbie Kanumba aweke picha ya kutunukiwa hiyo zawadi... ya Best Tanzania Hollywood Achievement, kutoka Kampuni ya Universal Hollywood ya nchini humo.
Google Best Tanzania Hollywood Achievement utaona kama kuna kitu cha namna hiyo.

KANUMBA ACHA FIX kadanganye washamba wenzako!

MDAU Minneapolis, USA

Anonymous said...

Mimi nauliza swali tu, waswahili tunasema kuuliza si ujinga. Hivi kitu kama hakipatikani kwenye "google" ndio kusema hakipo? Na je yote yanayopatikana kwenye "google" ni ya kweli? Nauliza tu, samahani.