Friday, October 10, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Ray C akiwa na Ice Cub alipokuwa Marekani mwaka jana

Fiesta 2008: Arusha mko tayari kujiramba?

Ile burudani yenye jina la Fiesta ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni ‘Jilambe’, baada ya kutoka Tanga wiki hii inadondoka A-Town kwa shoo ambayo itapigwa ndani ya Ukumbi wa Matongee Carnival Park, Oktoba 14, siku ya Jumanne ambayo pia itakuwa ni kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. JK Nyerere.

Utaratibu wa Fiesta miaka yote huwa ni burudani kwa kwenda mbele, ndiyo sababu kubwa iliyomfanya mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Godfrey Kusaga aiambie safu hii kwamba, wasanii kama Ray C, Chid Benz, Marlaw, Mwasiti, Dully Sykes, Prof Jay, A.Y, Q Jay, Nyota Ndogo kutoka Kenya na wengine kibao watakwenda ‘laivu’ stejini.

“Wapenda burudani wa Arusha watapata fursa ya kujilamba kwa kiingilio cha shilingi elfu tano tu. Baada ya kutoka huko tutakwenda kujilamba na mashabiki wa Mbeya, Dandu Hall ndiyo eneo la tukio, utakuwa ni moto ule ule ambao ulianzia Tanga, yaani wasanii wakali na shoo kali,” alisema God.


Jay (kushoto) akiwa na mmoja wa watayarishaji video kutoka Marekani

Jay: Amaliza kazi ya MTV Ghana

Kutoka ‘makao makuu’ ya familia ya Chokambaya, mitaa ya Kijitonyama, kiongozi wa umoja huo, Joseph Haule a.k.a Prof. Jizze amesema na ShowBiz kwamba, kazi iliyompeleka mjini Acra, Ghana imekamilika na tayari ameshadondoka Bongo.

Siku chache baada ya kudondoka ‘dizim’ mchizi alitamka kwamba, ofa aliyopewa na Kituo cha Televisheni cha MTV, kufanya wimbo na msela wa Ghana, Kwawe Kese kisha video iliyotayarishwa na mkali kutoka Marekani, Litle X imeshakamilika na kwamba anachosubiri ni kwenda kimataifa zaidi.

‘Baada ya kukamilisha zoezi la kupiga picha za video hiyo, ambalo lilichukua takribani siku sita, nilirudi Bongo, wiki iliyopita nilikwenda tena Ghana kwa ajili ya uzinduzi wa video hiyo, nashukuru Mungu kila kitu kimekwenda safi, inawezekana siku chache zijazo nitakuwa wa kimataifa zaidi,” alisema Jay.


Roy aacha simanzi kwa wasanii

Sisi waandaaji wa ShowBiz tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wasanii wote wa Bongo Flava, hasa waliyowahi kufanya kazi na mtayarishaji muziki, Roy Bukuku kupitia Studio za G2 ambaye alifariki dunia mapema wiki hii mkoani Mbeya.


MISS TZ ‘08 Full :Majukumu

Miss Vodacom Tanzania 2008, Nasreem Mohamed akitoa msaada kwa watoto yatima wanaoishi katika Kituo cha Nira Children and Youth Orphans Foundation (NICHIYOFO) kilichopo Mbagala wilayani Temeke jijini Dar es Salaam juzi.

Picha: Christopher Lissa)

(COMPILED BY mc George.)

No comments: