Friday, December 19, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Hadija Sure
Neema ChandeJokate Mwegelo
Wema Sepetu


IJUMAA SEXIEST GIRL: NELLY OUT!

Tukiwa tunaelekea kuwapata warembo watano bora watakaoingia ‘Top 5’ kunako shindano hili, Ijumaa Sexiest Girl, kisha kuwatafuta watatu watakaongia kwenye fainali kubwa, tunayo kila sababu ya kuwafahamisha kwamba, Nelly Kamwelu ndiye mshiriki aliyeliaga shindano hili leo na kuifanya safari yake iishie hapa.

Binti huyo anakuwa mshiriki wa tano kutoka na kulifanya shindano libaki na wasichana wanaodhaniwa wana mvuto saba, kama wanavyoonekana pichani na majina yao chini.

Mratibu wa shindano hili, Oscar Ndauka, amesema kwamba, anampongeza Nelly kwa kufikia hatua hiyo na kwamba urembo na mvuto wake vingeweza kumfikisha mbali zaidi lakini wanaheshimu kura za wasomaji ambao ndiyo Majaji wa mpambano huu. “Siyo kwamba washiriki wanaotolewa awakustahili kushinda, isipokuwa wasomaji ndiyo wanaoamua.

“Shindano linaendelea mpaka atakapopatikana mshindi (Ijumaa Sexiest Girl), tunawaomba wasomaji na wapenzi wa mpambano huu waendelee kuwa na sisi hadi tutakapofika mwisho wa safari hii ndefu. Wanachotakiwa ufanya ni kutuandikia ujumbe mfupi (SMS) wakimtaja mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuwa mshindi, kisha watume kwenda simu namba 0784-275 714,” alisema Ndauka.

2 comments:

Anonymous said...

Duh!Kumbe mratibu wa shindano hilo,Oscar Ndauka,ni demu na ni mmoja wa washiriki (at least according to picha ya kwanza hapo juu).Najua umekosea na ulikuwa unamaanisha huyo demu anyeitwa Somebody Ndauka.By the way,je huyo binti hana undugu na Oscar?If so,hiyo haiwezi kuathiri shindano zima kwa vile mwandaaji ana maslahi binafsi katika mmoja wa washiriki?Mark my word,huyu binti alikuwa aage mashindano zamani sana lakini ANA NAFASI YAKE ALOKWISHAANDALIWA,nayo ni USHINDI.

Anonymous said...

kumbe kuna mtu amekurekebisha kwenye picha ya kwanza.kwa mara ya kwanza ndio nimefungua blog yako abdala mrisho nimependa hili shindano ila kwa makosa uliyoyafanya hapo juu kwa kukosea hilo jina hata kama ndauka girl atashinda itaonekana mlimuandaa kushinda. na sijui kwa nini mpaka leo hujaedit hilo jina au huwa hurudii kusoma kazi unazofanya mwenyewe