Monday, November 30, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!


Madee: Tunaishukuru Global inatuthamini wasanii, safu ya Mpaka Home ni babu kubwa ila tunaomba iboreshe vitendea kazi ili picha zinazotoka kwenye gazeti ziwe kama ulaya.


Kanumba: Mpaka home ipo juu, mimi ni mmoja wa mastaa wa mwanzo kutembelewa, muhimu tuendelee kushirikiana kwasababu Global ni daraja la mastaa kufanikiwa.

Frola Mvungi: Mpaka Home inabidi iwe inaangalia, kuna wengine maisha yao ni uongo, wanajifanya wanaishi sehemu nzuri kumbe ni Bongo Dar es Salaam.

Ray: Wasanii wa Bongo wananyanyasika sana, hali ni mbaya inabidi waandishi waendelee kuwaandika ili jamii iwahurumie inunue kazi zao.

Fella: Mpaka Home inatusaidia sana sisi wasanii, angalau siku hizi tukipata pesa tunanunua hata makochi au godoro ili tukitembelewa tuonekane smati.

Tunda: Nafurahi kualikwa kwenye sherehe ya miaka minne ya Mpaka Home, naikubali, nipo pamoja na Global.

Safu ya gazeti la Risasi yenye heshima kubwa nchini, Mpaka Home imezaliwa upya. Happy Birthday Mpaka Home! Leo hii ni mwaka wa nne au kwa lugha ya wenyewe, unaweza kuita 4th Anniversary. Novemba 23, 2005 ndiyo ilianza kuruka ‘on air’, na staa wa kwanza kudondokewa alikuwa ni mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Benny Kinyaiya. Staa wa pili kufanyiwa programu ya Mpaka Home inayopatikana ndani ya Gazeti la Risasi litokalo kila siku ya Jumatano alikuwa ni mwana-Hip Hop mwenye vocal za kigumu, Fareed Kubanda ‘Fid Q’.

Mafanikio kwa jumla, mpango mzima wa Mpaka Home hutekelezwa na msanifu kurasa wa magazeti mbalimbali ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, George Alphonce ‘MC’ na mwandishi wa habari, Imelda Mtema. Ukweli ni kuwa MC na Imelda wamefanyakazi kubwa ambayo imeweza kuwavutia wengi, kiasi ambacho baadhi ya magazeti ya vyombo vingine vya habari, yamekuwa yakivutiwa na kuiga kile ambacho kinafanywa na Mpaka Home. Miaka minne ya Mpaka Home haijaenda bure, katika kipindi chote hicho, imeweza kufanyakazi na mastaa 1092, idadi ambayo ni kubwa katika jamii yetu.

Mpaka Home haijafanyakazi Dar peke yake, imekuwa ikisafiri sehemu mbalimbali nchini, ilikwenda Morogoro mara tatu ambako ilifanya programu na wasanii, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, Koba Anatori a.k.a MC Koba (Mtu Pori) na bondia, Francis Cheka. Koba na Sele waligongwa na MC wakati Cheka, yeye ishu yake ilitekelezwa na Imelda ambaye pia alisafiri hadi Zanzibar mara tatu na kuwaweka hadharani, Bi. Kidude, Berry Black, Berry White na Baby J.

Katika kipindi chote hicho, imekuwa ikipokea maoni mengi, huku safu ambayo ilimhusu mwana Bongo Flava, Abbas Hamis Kinzasa ‘20%’ ikiwa bado inashika namba moja, kutokana na jinsi maisha yake yalivyowagusa wengi. 20%, kazi yake ilifanyika nyumbani kwao Kimanzichana, kitu kikubwa ambacho kiliwavutia wengi ni mjengo wao ambao ni ghorofa la udongo. Ni matumaini yetu kuwa Mpaka Home itaendelea kuwa juu, ikiwagusa watu wengi. MC na Imelda wapo sawa kwa ajili kulisongesha.

Sherehe fupi ya 4th Anniversary ya Mpaka Home imefanyika ndani ya mjengo wa Magazeti Pendwa, Global ambapo mastaa waliohudhuria ni Meneja wa TMK Family, Said Fella, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Kanumba. Mstaa wengine wakubwa waliohudhuria ni Madee, Tundaman, Yusuf Mlela na Flora Mvungi.
************
compiled by mc george

No comments: