Friday, December 4, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

FAINALI HIYOO!!
Mzigo wa Ijumaa Sexiest Bachelor upo mbioni kufikia penyewe, na hivi sasa ni fainali.

Kwa mujibu wa waratibu wa shindano hili, mpango upo kamili na jina la mshindi litatajwa katika hafla kubwa ambayo ndiyo itakuwa fainali.

Waratibu wamenena kuwa maombi ya wapigakura yamezingatiwa kwamba mshindi si vema kupatikana kimya kimya, hivyo wakaomba iwepo fainali ili mshindi atajwe waziwazi mbele ya Watanzania watakaofanikiwa kuhudhuria.

Kutokana na mkakati huo, imeelezwa kuwa siku si nyingi, zijazo, itatangazwa tarehe ya fainali, hivyo msomaji awe tayari kwa tukio kubwa na lenye uzani wa kutosha.

Mzigo bado unawahusu Steven Kanumba, Hemed Suleiman, Yusuf Mlela na Laurence Malima ‘Marlaw’, hivyo kama mmojawapo unaona anakuvutia, basi mpigie kura kwa kuandika SMS, ukiambatanisha namba yake ya ushiriki kisha unaituma kwenda namba 15551.

Kumbuka kwamba kura yako ndiyo kila kitu katika shindano hili ambalo limedhaminiwa na maduka ya Zizzou Fashion yaliyopo Sinza, Afrika sana na Victoria, DSM.

***************************************

Ngwea: Aendelea kupiga bao na N’ge 1982
Kutoka ndani ya Kampuni ya Zizzou Entertainment ambayo imesheheni wakali wa muziki wa Bongo Flava, tumedondoshewa ishu kwamba msanii Albert Magwea a.k.a Ngwea au Cow Bama bado anaendelea kupiga bao kupitia mauzo ya albamu yake ya pili, N’ge 1982 ambayo imeshuka sokoni hivi karibuni ikiwa na ngoma zaidi ya 10.

Kwa mujibu wa uongozi wa kampuni hiyo, albamu ya Ngwea ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya imeonekana kufanya vyema kitaani kutokana na ubora wake, zikiwemo kazi nyingi kali kama Nipe dili, Speed 120, Singida Dodoma, Mida Mibovu, CNN na nyingine.

Akipiga stori na ShowBiz, Ngwea ambaye alikuwa anagonga ‘buku’ pande za Bagamoyo Chuo cha Sanaa alisema kwamba nyimbo 15 kali zilizomo ndani ya albamu hiyo zimeifanya kuwa juu zaidi sokoni na kwamba amewataka mashabiki wake ambao bado hawajaifikia wajaribu kuisikiliza ili waone tofauti iliyopo na nyingine zilizotangulia mtaani. “Kwa wale watakaohitaji kuinunua wacheki na sisi kupitia simu namba 0713 572323, 0754 999950,” alisema.
*****************************************

Andre G: Ahofia kuporwa demu wake!
Dogo’ anayekuja juu kunako game ya muziki wa kizazi kipya, Andre George a.k.a Andre G ndani ya safu hii ameonesha hofu ya kuporwa demu wake na baadhi ya masela wa Bongo wenye tabia ya kutoka na mali za wenzao, Hamida Hassan anadondoka nayo.

Mchizi ambaye hivi sasa anasimamia miguu miwili na ngoma yenye jina la ‘Kichuna wangu’ aliyompa shavu Quick Racka alisema hayo hivi karibuni alipotakiwa na ShowBiz amtaje ampendaye ili jamii ipate kumfahamu.

“Sitoweza kulitaja jina lake kwa usalama wetu kwakuwa nampenda sana, isipokuwa naweza kutaja pande anazoishi ambazo ni Kinondoni ili ajitambue kuwa ni yeye, asifikirie kuwa nina mwingine. Karibu nyimbo zangu zote huwa zinamzungumzia yeye,” alisema Adre G.

Msela alijitambulisha kwenye game kupitia ngoma yake, Jinsi alivyo aliyomshirikisha Mhe. Temba, ikafuatiwa na Marena kisha Kichuna wangu.

*******************************
FID Q Kuongoza msafara
Mchizi kutoka Rock City, Fareed Kubanda a.ka. Fid Q anatarajia kuongoza msafara wa baadhi ya mastaa wa muziki wa kizazi kipya watakaoshuka pande za Iringa na kuangusha burudani ndani ya Uwanja wa Samora Jumapili ya wiki hii.

Ishu inaitwa mtikisiko na mastaa walioungana pamoja kwa ajili ya zoezi hilo ambao wataongozwa na Fid ni pamoja na Chegge, Matonya, Madee, Tundaman, Baby Madaha, Squeezer, Linex, Nay wa Mitego, Dully Sykes, Fell na wengine kibao.
“Mbali na kina Fid Q kufanya bonge la shoo siku hiyo, mabondia Rashid Matumla ‘Snake Boy’ na Chupaki wa Iringa,” watazichapa kuwania ubingwa usiyo rasmi,” alisema mratibu wa ishu hiyo, Eddo.
**********************************

50 cent: Asachiwa na Tyra Banks!
Kutoka pande za Marekani kwa Obama, ShowBiz imeinyaka ishu moja hot inayomuhusu memba na kiongozi wa Kundi la G-Unit, 50 Cent ambaye hivi karibuni alijikuta akisachiwa mfukoni na mrembo Tyra Banks baada ya kumualika kunako kipindi chake, ‘The Tyra Show’.

Mtandao uliyodondosha stori hii unasema kwamba, 50 Cent alipokuwa akihojiwa na Tyra alisema kwamba kamwe hawezi kutembea bila kuwa na dola 25 kwenye mfuko wake wa nyuma ambazo zinakuwa ni za ‘imejensi’ endapo kitatokea kitu chochote kinachohitaji mkwanja zimsaidie.

Kauli hiyo ya 50 ambaye aliibuka katika kipindi hicho kwa ajili ya kunadi Cd yake pamoja na kitabu kinachoizungumzia muvi mpya aliyocheza inayotarajiwa kudondoka kitaani hivi karibuni, ilimfanya Tyra asiamini na kuamua kuzama katika mfuko wa staa huyo wa G-Unit na kuibuka na dola kibao ambazo alizionesha laivu kwa watu waliokuwa wanaangalia kipindi hicho.

COMPILED BY MC GEORGE

No comments: