Tuesday, December 8, 2009

Ukweli kuhusu Saratani na lishe


Baada ya utafiti wa muda mrefu, mtafiti maarufu wa ugonjwa wa Saratani (Cancer), Johns Hopkins, amegundua kuwa kuna njia mbadala ya kudhibiti seli (cells) zinazosababisha kansa mwilini, mbali ya ile njia inayojulikana kitabibu ya tibakemikali (chemotherapy) na mionzi (Radiation).

Katika ulimwengu wa lishe, kansa inaelezwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa virubisho muhimu mwilini, ingawa kwa baadhi ya watu hutokana na sababu za kinasaba na kimazingira wanayoishi.

Tunaelezwa kuwa, kwa kawaida, kila mtu ana seli za kansa mwilini. Seli hizo huwa hazionekani kwa vipimo mpaka pale zinapoongezeka hadi kufikia kiasi cha bilioni moja. Mgonjwa wa saratani anapoambiwa na daktari kuwa hana tena seli za saratani baada ya matibabu, huwa ina maana kwamba seli zake zimefikia kiwango cha chini ambacho hakiwezi kuonekana kwa vipimo tena wala kuleta madhara makubwa.

Aidha, inaelezwa zaidi kuwa kila mtu katika maisha yake, hutokewa na seli za saratani kati ya mara 6 hadi zaidi ya mara 10, wakati seli hizo zinapotokea hutegemea kinga ya mwili aliyonayo mtu, kama kinga iko chini huweza kujizalisha na kuwa uvimbe, lakini kinga ya mwili inapokuwa imara, seli hizo hudhibitiwa vilivyo.

Hivyo, ili kujiepusha na uwezekano wa kupatwa na saratani ya aina yoyote, ni vyema kuimarisha kinga yako ya mwili. Njia pekee ya kuimarisha kinga ya mwili ni kuzingatia lishe sahihi na kubadilisha staili ya maisha kwa ujumla. Kwa sababu upungufu mkubwa wa virutubisho mwilini, ndiyo kichocheo kikubwa cha kuibuka seli za saratani.

Tiba ya kemotherapi na mionzi siyo kimbilio zuri sana katika kukabiliana na seli za saratani, kwani wakati wa kuteketeza seli za saratani, mionzi huunguza pia seli nzuri za kwenye mifupa, tumbo, ini, figo na mapafu na kuacha makovu kadhaa kwenye tishu za mwili.

Tiba ya mwanzo ya kemotherapi na mionzi husaidia kupunguza ukuaji wa uvimbe, lakini unapofanyika kwa muda mrefu huleta madhara katika sehemu nyingine za mwili.

Mwili unapokuwa na sumu nyingi mwilini zitokanazo na tiba ya muda mrefu ya kemotherapi na mionzi, kinga ya mwili huishiwa nguvu au huteketezwa kabisa, hivyo mtu kuishiwa na kinga mwilini hivyo kukabiliwa na magonjwa na maambukizi lukuki.

Johns Hopkins akiezea zaidi madhara ya tiba hizo za mionzi anasema kuwa, tiba ya kemotherapi na mionzi inapofanyika kwa muda mrefu hufanya chembe za saratani kuwa sugu na ngumu kuziondoa. Upasuaji nao huweza kusababisha kusambaa kwa saratani sehemu zingine za mwili.

IPI NJIA BORA YA KUDHIBITI KANSA KWA LISHE?
Njia bora na ya uhakikika zaidi katika kupambana na seli za saratani ni kuzishindisha na njaa kwa kuacha kula vyakula ambavyo huzifanya seli hizo ziishi na kustawi.

CHAKULA CHA SELI ZA SARATANI NI NINI?
Sukari ni miongoni mwa vyakula vya seli za saratani. Kwa kuacha kula sukari, utakuwa umekata mgao muhimu sana wa chakula cha saratani. Badala ya sukari, tumia asali halisi na achana kabisa na ulaji wa sukari au vyakula vyenye sukari.

Maziwa nayo si mazuri kwa mgonjwa wa saratani kwa sababu huzalisha kitu kiitwacho ‘mucus’, hasa kwenye utumbo, ambacho ni chakula cha seli za saratani mwilini. Hivyo kwa kuacha kunywa maziwa utakuwa umesitisha uzalishaji wa ‘mucus’ na hivyo seli kukosa chakula chake na kufa.

Seli za saratani hupenda kuishi kwenye mazingira yenye asidi, hivyo usipende kula vyakula vinavyozalisha asidi kwa wingi.

Itaendelea wiki ijayo.

No comments: