Tuesday, July 7, 2009

Unajua umuhimu wa chungwa kwa afya yako?

YOU ARE WHAT YOU EAT
Msimu wa machungwa umewadia na kama mnavyofahamu, unapowadia msimu huu machungwa huzagaa kila mahali na kila kona ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa idadi hiyo ya machungwa na bei huwa nafuu kufikia hadi shilingi 20.

Lakini siyo ajabu pia kuona msimu huu unakwisha bila mtu kula chungwa hata moja. Hii inatokana na kasumba ya binadamu tangu zamani ya kutothamini matunda. Kama wewe ni miongoni mwa watu wenye tabia hiyo, fikiria mara mbili kwa sababu chungwa lina faida nyingi mwilini, zikiwemo zifuatazo:

Chungwa lina kirutubisho kiitwachwo ‘Beta Carotene’ ambacho kina umuhimu mkubwa kiafya kwa sababu hulinda chembechembe hai za mwili dhidi ya maradhi.

Chungwa lina madini aina ya ‘Calcium’, ambayo kila mtu anajua kwamba ni muhimu kwa ustawi wa mifupa na meno, hasa kwa watoto wa shule.

Chungwa lina ‘Folic Acid’ ambayo huhitajika na ubongo ili uweze kufanyakazi yake vizuri ya kufikiri, kutunza kumbukumbu na kuchanganua mambo kwa haraka.

Chungwa husaidia watu wenye matatizo ya shinikizo la damu kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha ‘Magnesium’ ambacho hudhibiti mfumo wa damu.

Chungwa litaulinda mfumo wako wa hewa na kuweka seli za mwili kwenye uwiano unaotakiwa kutokana na kuwa na kiwango kizuri cha madini aina ya ‘Potassium’.

Chungwa huharakisha usagwaji wa chakula na hivyo kupata nguvu mwilini kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘Thiamin’ kinachohitajika kwa kazi hiyo.

Chungwa hutoa nafuu kwa magonjwa ya Pumu, Kikohozi, Kifua Kikuu, Nimonia, baridi yabisi na huzuia ugonjwa wa mawe kwenye figo. Vile vile huondoa hamu ya kunywa pombe kwa wale wanaotaka kuacha unywaji wa pombe na husaidia sana kukata makamasi kwa wale wenye mafua.

Maganda ya chungwa nayo yana kiwango kikubwa cha Vitamin C kama lilivyo chungwa lenyewe. Hivyo ni vizuri kama utaweza kula chungwa na maganda yake au angalau pamoja na nyama zake ili upate virutubisho vyote.

Kama ulikuwa si mlaji wa machungwa mpaka uambiwe na daktari, sasa umefika wakati wa kutambua umuhimu wa chungwa na kuanza kulichangamkia kama vile huna akili nzuri, kwa faida ya afya yako ya sasa na ya baadae.

Ajali michezoni!



Picha zaidi unaweza ukawapa wadau link hii: http://www.nifahamishe.com

Monday, July 6, 2009

UTATA: MICHAEL MUISLAMU, MKRISTO?



Baada ya kifo chake, utata umeibuka kuhusu dini yake, wapo wanaosema Michael alikuwa Muislamu na wapo wanaopinga na kusema alikuwa Mkristo tena wa Madhehebu ya Mashahidi wa Yehova! Wanaosema alikuwa muislamu chanzo chake kilikuwa ni maneno ya kaka mtu Jermaine Jackson aliyoyatoa wakati anatangaza kifo chake na aliporejea kutoka kuhiji Mecca na kukaririwa: “When I came back from Mecca I got him a lot of books and he asked me lots of things about my religion and I told him that it’s peaceful and beautiful.

“He read everything and he was proud of me that I found something that would give me inner strength and peace.

“I think it is most probable that Michael will convert to Islam.

“He could do so much, just like I am trying to do. Michael and I and the word of God, we could do so much,” alisema Jermaine February 24, 2007

Stori nyingine ya hivi karibuni ni ile ya gazeti la udaku la The Sun la Novemba 21,. 2008 ambayo iliandika kuwa Michael alithibitisha kuingia Uislamu kwa kutoa shahada mbele ya sheikh mmoja nchini Uingereza! Stori yenyewe ni hii hapa:

Michael Jackson has become a Muslim — and changed his name to Mikaeel.

The skint superstar, 50, donned Islamic garb to pledge allegiance to the Koran in a ceremony at a pal’s mansion in Los Angeles, The Sun can reveal.

Jacko sat on the floor wearing a tiny hat after an Imam was summoned to officiate — days before the singer is due to appear at London’s High Court where he is being sued by an Arab sheik.

A source told last night how Jacko, brought up as a Jehovah’s Witness, decided to convert as he used a studio at the home of his chum to record a new album.

The star — whose hits include The Way You Make Me Feel — was spotted looking “a bit down” by a producer and a songwriter who had both embraced Islam.

The source said: “They began talking to him about their beliefs, and how they thought they had become better people after they converted. Michael soon began warming to the idea.

“An Imam was summoned from the mosque and Michael went through the shahada, which is the Muslim declaration of belief.” Mikaeel is the name of one of Allah’s angels.

“Jacko rejected an alternative name, Mustafa — meaning “the chosen one”.

Brit singer Yousef Islam, 60 — who was called Cat Stevens until he famously converted — turned up to help Jacko celebrate.- Source: The Sun (UK), Nov. 21, 2008

- LAKINI baada ya taarifa hizo, ukweli ulikuja kudhihirika kuwa yote hayo yalikuwa ni 'rumours' tu, hebu soma hapa:

After such images it did not take very long for western media like the NY Sun and NY Post to declare that Michael Jackson had converted to Islam at a ceremony in L.A. and changed his name to “Mikaeel” (Arabized version of Michael and the name of one of the four major angels of Islam).

The news story was immediately slammed by Jackson’s representatives:

Jackson’s New York lawyer, Londell McMillan, took the opportunity to trash a British press report that Jackson has become a Muslim. “That’s rubbish. It’s completely untrue,” McMillan told reporters.

Na hii nayo ikaendelea kukandamiza msumari wa mwisho kwa kusema:

Still, because the idea of Jackson being a Muslim was just so difficult to give up, many Muslim leaders bought into the account. Just yesterday Imam Zaid Shakir, a traditionalist leader in the United States wrote: “A good friend who is a reliable source of information called and said that Michael had become Muslim. He had been working on an album with the well-known Muslim musician, Dawud Warsby, and another Muslim performer, and the two, sensing Michael’s troubled and depressed state had invited him to Islam. He accepted their invitation. Michael was no stranger to the religion, having been exposed to it by his brother Jermaine, who had converted to the faith in 1989.”

Unfortunately for Zaid Shakir’s “reliable source” the account is not correct. At his blog Dawud Wharnsby reveals that he had never even met Michael Jackson.

Lastly - many have been in touch with me over the past year to inquire about my personal relationship with Michael Jackson. A November 21, 2008 Sun (UK) article spread internationally stating that Michael had adopted the religion of Islam through friendship with both myself and my colleague Idris Phillips during recording sessions in Los Angeles.

For the record: Though our professional circles did cross-over slightly with various common professional acquaintances - I never had the honour or pleasure of meeting Micheal Jackson [sic] personally, nor did we ever correspond on matters of our professions, personal lives or faiths. Now Michael is gone.

Kwa ‘data’ hizo mbili, tukubaliane, tena bila shaka, kuwa Michael Jackson hakuwahi kuwa Muislamu wala hakuwahi kusema hadharani kuwa amesilimu. Na kwa kuwa maandalizi ya mazishi yake yameshajionesha kuwa ataagwa na atazikwa na jeneza mambo ambayo ni kinyume na imani ya Kiislamu, then hawezi kuwa alikuwa MUISLAMU jamani!!!!!



WIKIENDA SHOWBIZ!

TMK WALA SHAVU LIBERIA
Guyz wasiofunikika Bongo Flava, TMK Wanaume Family wanatarajiwa kupiga shoo ya kihistoria kwenye himaya ya mama Ellen Johnson-Sirleaf a.k.a Liberia na kuwa-entertain Waliberia 4 the new style & Slogan Konzi moja manundu 10,000.

Meneja wa TMK, Said Fella a.k.a Mkubwa au Biggie wa Michano alisema nasi kuwa kundi lake limepokea mwaliko rasmi, hivyo Julai 13 that means this month watakwea pipa na kwenda kuwadunda makonzi Waliberia ili waache kufagilia ishuz za kuingia msituni na kupigana vita wenyewe kwa wenyewe.

Fella akiendelea kushusha semi, alitudakisha kuwa shoo hiyo itaitwa “Kujenga ni kupatana kwa wananchi” na kuongeza: “Itakuwa shoo itakayoambatana na ziara ya siku nne cuz tutaondoka Julai 13 na kugeuka Bongo Julai 18, halla mkubwa.”
*****************************************


LUIZA MBUTU na donda mguuni!
‘Hirizi’ ya Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Luiza Nyoni Mbutu seems to priority her job kuliko afya yake.

Last Week kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere katika maonesho ya Sabasaba, Luiza appeared on the Twanga Pepeta stage na kutoa shoo ya nguvu huku mguu wake wa kushoto ukiwa na jeraha kuonesha kuwa aliumia siku si nyingi zilizopita na kabla hajapona sawa sawa, alipanda jukwaani kama kawa.

**********************************************

Ishu ya 'Nose Job' bado ipo kifamily zaidi
Ubadilishaji pua ambao The Jacko aliufanya siyo kitu kigeni ndani ya familia yake, imeelezwa zaidi katika kipindi hiki dunia inaomboleza kifo chake cha ghafla..

Imeelezwa kuwa Wacko alirekebisha pua katika upasuaji ambao huitwa kitaalamu “Rhinoplasty” na kuonekana kioja kwenye jamii lakini kumbe tabia hiyo ni mzuka wa familia yao kwa sababu kuna baadhi ya ndugu zake ambao wamewahi kuingia 'theatre' na kurekebishwa kama yeye.

Janet na La Toya ambao ni dada zake The Jacko ni mfano halisi wa ndugu zake waliofanya Rhinoplasty ambao unaweza pia kuuita kwa lugha nyepesi 'Nose Job' au 'Nose Reshaping'.

Abby Cool & MC George over the weekend imesoma mtandaoni kuwa pia kuna baadhi ya kaka zake The Jacko ambao nao wamefanya 'Nose Job' na walifanya hivyo kwa sababu baba yao, Joseph ‘Joe’ Jackson alipenda kuwakoromea
enzi za utoto wao kwamba pua zao zina shepu mbaya, kauli ambayoilikuwa inawafanya wajione wabaya na hivyo kutumia uwezo walionao wa kifedha kijibadilisha.
*******************************************

****************************************

Ebwana Dah! NICOLE SCHERZINGER
Last week tulikuwa na ishu ya marehemu Michael Jackson kutokana na uzito wake, kwahiyo safu hii ilienda pamoja na mambo mengi kuhusiana na mfalme huyo wa Pop duniani lakini leo, ebwana dah!

Anaitwa Nicole Scherzinger, ni mwanamuziki mwenye sauti inayovuta, sura inayohamasisha na body linalotamanisha, hapa naye anaonesha ufundi wake wa kubadili testi za kimapenzi kwa kutoka na wanaume sita wanaojulikana.

Aidha, staa huyo ambaye alifanya kolabo ya nguvu na Avanty kwenye traki la Love about us, inadaiwa kwamba mwaka 2007 ndiyo alitia fora kwa kubadili wanaume watatu kwa staili ya bandika bandua.

Nicole anatajwa kutoka na Nuno Sousa katika kipindi ambacho hakiwekwi wazi, Nick Hexum kati ya mwaka 2002-05, Talan Torriero 2005-07, Jimmy Iovine 2007, will.i.am 2007, Lewis Hamilton ambaye alianza ‘kuchenguka’ naye mwaka 2008 mpaka sasa.

Kwa kirefu, Nicole anaitwa Nicole Prescovia Elikolani Valiente Scherzinger, majina mengine Nicole Kea, Nikki, Cola, Elikolani. Umri wake ni miaka 31, ana urefu wa futi 5 na inchi 5, rangi ya macho yake ni dark brown, nywele ni black, taifa lake ni Filipino.

Madhehebu yake ni Roman Catholic, alisoma duPont Manual High School na Youth Performing Arts School kabla ya kujiunga Wright State University. Alizaliwa Juni 29, 1978.
*************************************************
Compiled by mc george

Saturday, July 4, 2009

KISA CHA KWELI

Nimehadithiwa kisa kimoja cha kweli na cha kustaajabisha ambacho kimeniacha na maswali mengi na mwisho nikamuuliza aliyenihadithia; “huyo jamaa hakuwa jini kweli? kisa chenyewe nimehadithiwa na dada mmoja aged between 35 – 40 ambaye hapendi nimtaje jina. Alinihadithia kama ifuatavyo:

Mambo? (naishi nae jirani), nina stori nataka nikupe, maana mimi mwenyewe nimeshangaa na mpaka sasa hivi siamini kilichotokea. Wiki iliyopita nilikwenda Morogoro, wakati naondoka hapa nyumbani (anakaa Ilala) kwenda Ubungo nilichukua teksi. Wakati naondoka nilikuwa na jumla ya shilingi 280,0000.

Nilichukua shilingi 30,000 nikaweka kwenye pochi ndogo kisha nikaweka kwenye sidiria, iliyobaki 250,000 nikaweka kwenye bahasha halafu nikaiweka kwenye mkoba wangu ambao nilipokuwa kwenye teksi, niliuweka kwenye kiti cha abiria cha nyuma.

Huyo dereva huwa namuona tu, kwani gari lake huwa analaza jirani yetu, lakini simjui vizuri. Tukiwa tunaelekea ubungo stendi, nilikumbuka simu yangu, nilipojisachi nikaona sina, lakini nilikuwa na uhakika nilipanda nayo, nikamuomba dereva aipige simu yangu ili kama imeangukia ndani ya gari niione.

Nikampa namba yangu akaipiga, kweli ikaita kutoka chini ya kiti nilichokuwa nimekaa. Nikaiokota kisha nikaiweka vizuri tukaendelea na safari yetu hadi Ubungo, tulipofika nikamlipa dereva nauli yake tukaagana. Mimi moja kwa moja kwenye basi hadi Morogoro.

Nilipofika nyumbani Morogoro, nikafungua mkoba wangu ili nitoe ile bahasha yenye 250,000, lakini sikuiona, nikajaribu kupekua vizuri kila mahali lakini wapi, moja kwa moja nikajua ile bahasha yenye pesa nimeibiwa.

Lakini nilipotafakari vizuri, nakaamini sikuibiwa kwenye basi, bila shaka itakuwa nimeidondosha kwenye teksi wakati naiweka vizuri mara baada ya kutoa zile elfu 30, ambazo nilizitoa ili nisipate shida kutoa hela ya nauli ya basi na kutatua shida ndogondogo za njiani.

Kwakweli nilichanganyikiwa, ukizingatia ndiyo pesa niliyokuwa naitegemea katika biashara yangu niliyoendea huko na sikuwa na hela nyingine. Dereva teksi simjui wala namba yake sina, lakini nikakumbuka nilimpa namba yangu ya simu tukiwa tunaelekea Ubungo ili kuipiga wakati natafuta simu yangu. (angalia mambo yanavyoenda hapa).

Nikachukua kisimu changu, nikaangalia missed call za mwisho na kwa kuwa sikuwa nimepigiwa simu na watu wengi, niliiona namba yake mara moja, nikampigia. Huku roho ikinidunda, dereva akapokea simu na baada ya kujitambulisha kwake akanikumbuka na nikamuuliza kama ameokota bahasha kwenye gari yake!

Dereva teksi akasema hajaiona, ila baada ya kunishusha mimi, alipofika kituo cha daladala kilicho jirani na stendi ya Ubungo kuelekea Posta, alipata abiria wengine wanne (si unajua ule mtindo wa abiria wanne kuchanga buku buku) ambao aliwapakia hadi posta.

Wakati wanaelekea posta, abiria mmoja alimuuliza: “dereva, kuna abiria yoyote alipanda huma kabla yetu,?” dereva akamjibu ndiyo. “Basi naomba nikupe namba yangu, akikupigia, mpe namba yangu anaipigie,” alisema yule abiria ambaye ni mwanume wa makamu kiasi. Hata dereva teksi alipotaka kujua kulikoni, hakuambiwa.

Basi, nikamuomba dereva teksi anitumie ile namba na baada ya kunitumia nilimpigia yule kaka. Baada kumpigia simu iliita na kupokelewa. Nikajitambulisha kwake kisha akaniuliza kiasi cha pesa kilichomo na jina langu, maana kwenye ile bahasha niliweka na kitambulisho changu cha kupigia kura.

Baada ya maelezo mafupi, yule kaka akaniambia niondoe wasiwasi hela zangu zote zipo na kunieleza kuwa mara baada ya kupanda kwenye ile teksi, aliiokota bahasha hiyo chini kwenye kiti cha nyuma na hakumwambia abiria mwingine zaidi ya kumuuliza dereva teksi.

Hivyo akaniambia kuwa yeye anafanyakazi Tanesco Ubungo, nikirudi nimtafute anipe pesa zangu. Nikamwambia nimtume ndugu yangu amtafute popote alipo ili ampe hizo pesa ili mimi jikirudi kutoka Morogoro nizikute nyumbani, kaka akakataa, akasisitiza lazima anikabidhi mimi mwenywe!

Nikakubaliana naye, lakini akili ya kwanza kunijia kichwani nikahisi huu utakuwa ndiyo mwanzo wa kutongozwa, lakini yote namwachia Mungu. Hata hamu ya kukaa Morogoro sikuwa nayo, nikalazimika kugeuza siku ya pili yake kurejea Dar.

Nilipofika Dar, nikampigia simu kumtaarifu kuwa nimesharudi, akaniambia niende Ubungo Bus Stand na nikifika pale nimpigie simu atakuja nilipo, kwani ofisi zake zipo jirani hapo Tanesco Ubungo.

Kwa kuwa sikuwa najiamini, nilifuatana na ndugu yangu mmoja hadi Ubungo, nilipofika nilimpigia simu yule kaka, kwanza simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa, nikaanza kuingiwa na wasi wasi huenda nimelshaingizwa mjini. Baadae nilipiga tena na kumpata, akaniambia alikuwa msikitini nimsubiri atakuja baada ya muda. Nilikaa tena kwa muda mrefu na kuendelea kuingiwa na wasiwasi zaidi, kwani alikuwa hatokei.

Wakati naanza kukata tama, mara nakaona simu inaita, kuangalia nakaona ni yule kaka, akaniambia ameshafika na ananitafuta. Nilianza kumuona mimi, nikamuelekeza nilipo akaja.

Wakati anakuja, roho ilikuwa ikinienda mbio, sikuwa na uhakika kama kweli ananiletea pesa zangu au kuna dili anataka kunichezea. Maana kwa mji wa Dar, lolote linaweza kukukuta bila kutarajia.

Alipofika, kwanza alituomba samahani kwa kuchelewa na baada ya kutambulishana pale, akanyoosha mkono wake akaniambia: HESABU PESA ZAKO DADA! Huku moyo ukinienda mbio, nikapokea na kuhesabu pesa zangu huku natetemeka. Nikakuta ZOTE ZIKO SAWA, haikupungua senti tano!!!

Na mimi kuonesha uungwana, nikahesabu shilingi 50,000 nikampa. YULE KAKA AKAZIKATAA KABISA, akasema nimpe hela ya teksi tu shilingi 4,000 aliyokuja nayo pale. Sikuamini masikio yangu. Kweli nikampa kisha tukaaga na akaondoka zake. YULE KAKA SIMJUI, HANIJUI!

Kwa dunia tuliyonayo sasa, nashindwa kuamini kama bado tuna watu waamminifu kama huyu kaka. Hakika mtu kama huyu malipo yake ni makubwa hapa duniani na kesho mbele ya Mungu. Sina cha kukupa wewe kaka, nakuombea kwa Mungu ufanikiwe katika kila jambo unalolifanya!

Hiki ni kisa cha kweli kabisa kama nilivyohadithiwa na yaliyomkuta. Je wewe, mwenzangu, unao uaminifu wa kiasi hicho?

Friday, July 3, 2009

VIJIMAMBO VYA TANGA!

ANKO MO BLOG SPOT inatumaini upo salamaa.. ANKO MO BLOG SPOT inaomba msaada wako kutangaza mtandao wa marafiki wa VIJIMAMBO VYA TANGA

http://www.ankomo.blogspot.com

Mtandao wa VIJIMAMBO VYA YANGA unawezesha watu kutoka sehemu mbalimbali kukutana, kuchat, kushare videos, miziki na mambo mengine mbalimbali
G5 contacts:

Email: ankomo25@yahoo.com or deddyhammy@hotmail.com
Blog: www.ankomo.blogspot.com or VIJIMAMBO VYA TANGA
Phone: +255-719-000-010
Wadau wako kutoka
ANKO MO BLOG SPOT


MTOTO PEKEE ALIYEOKOKA KATIKA AJALI YA NDEGE YA YEMENIA



Mtoto aliyenusurika kimiujiza kwenye ajali ya ndege ya Yemen Airways iliyodondoka kwenye bahari ya Hindi karibu na visiwa vya Komoro na kuua watu 152 ameelezea jinsi alivyonusurika kimiujiza kwenye ajali hiyo. Bahia Bakari mwenye umri wa miaka 14 ndiye abiria pekee aliyenusurika kwenye ajali ya ndege ya Yemenia, Airbus A310 iliyotokea alfajiri ya jumanne wiki hii.

Bahia aling'ang'ania mabaki ya ndege na kuelea juu yake kwa masaa 12 katika hali ya hewa mbaya na bahari ambayo imejaa papa wengi kabla ya waokoaji kufika na kumuopoa.

Mtoto huyo ambaye hali yake inaendelea vizuri baada ya kupewa matibabu nchini Komoro amerudi kwao Ufaransa kuungana na baba yake.

Kassim Bakari, baba wa msichana huyo, akiongea na vyombo vya habari vya Ufaransa alisema kuwa nilipoongea naye kwa simu aliniambia "Tuliona ndege ikiangukia kwenye maji, nilijikuta kwenye maji, niliwasikia watu wakiongea lakini sikuweza kumuona hata mtu mmoja. Nilikuwa kwenye kiza sikuona chochote".

"Baba sikuweza kuogelea vizuri, niling'ang'ania juu ya kitu, sijui ni kitu gani" alisema Bahia akimwambia baba yake.

Bakari ambaye ana watoto wengine watatu alisema kuwa aliposikia habari za ajali ya ndege hiyo, moja kwa moja alifikiria kuwa hatamwona tena mkewe na mtoto wake wa kwanza.

"Ni msichana mwenye aibu sana, sikufikiria kama angenusurika namna hii, Siwezi kusema hii ni miujiza bali ni matakwa ya mwenyezimungu" alisema Bakari.

Bakari alisema kuwa Bahia hadi sasa hajaambiwa kuwa mama yake amefariki.

"Walimwambia kuwa mama yako yupo chumba cha jirani ili kutomshtua lakini ukweli ni kwamba mama yake amefariki na sijui nani ataweza kumwambia" alisema baba wa mtoto huyo.

Waokoaji walimuokoa Bahia kwenye bahari ya Hindi kilomita 16 toka kwenye pwani ya Visiwa vya Komoro.

Waokoaji hao walisema kuwa Bahia alikuwa dhaifu sana wakati anaokolewa, hakuweza hata kulishika boya alilorushiwa na hivyo kumfanya mzamiaji kupiga mbizi na kumpandisha kwenye boti ambako alifunikwa na blanket na kupewa maji ya moto yenye sukari anywe wakati anawahishwa hospitali.

Watu wengi wamestaajabu jinsi mtoto huyo alivyonusurika ajali hiyo na kuelea kwa jumla ya masaa 12 kwenye bahari ambayo imejaa papa wengi tena akiwa hana hata life jacket.

translation: fromcoast.blogspot.com

IJUMAA SHOWBIZ!

K-Sher “Mac Regan siyo mpenzi wangu”
Akiwa bado anawakilisha kunako tamasha kubwa la ZIFF litakalomalizika kesho Visiwani Zanzibar, msanii Khadija Shaban a.k.a K-Sher amesema na ShowBiz kwa njia ya simu kwamba amesikitishwa na uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu kwamba yuko katika uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Orijino Komedi, Alex Chalamila a.k.a Mac Regan.

Akipiga stori na safu hii kwa njia ya simu kutoka pande hizo huku akionesha kuwa na huzuni, K-Sher ambaye ni msanii bora wa kike 2008-2009 alisema kwamba, amesikitishwa na baadhi ya watu wanaoeneza uvumi huo kikiwemo chombo kimoja cha habari (siyo cha Kampuni ya Global Publishers) ambao wamesababisha ahitilafiane na boifrendi wake.

“Mac Regan ni rafiki yangu wa kawaida kama walivyo wasanii wengine wa kiume, sina uhusiano naye wa kimapenzi, nataka watu watambue kwamba mimi nina ‘boifrendi’ wangu huku Zanzibar (hakumtaja jina), taarifa hizo zimemsikitisha hata yeye na watu wengine wanaomzunguka,” alisema msanii huyo ambaye siku chache zijazo anatarajia kuitambulisha albamu yake, yenye jina la ‘K-Sher’ pande za Arusha.
********

Marco chali kusepa MJ Record
Kutoka pande za Masaki Dar es Salaam zilipo Studio za Mj, ShowBiz ilidondoshewa ishu kwamba mtayarishaji muziki maarufu anayepiga mzigo katika mjengo huo, Marco Chali, huenda akala kona baada ya mkataba wake kumalizika juzi Jumatano, Zubagy Akilimia anaanguka na ishu hii.

Baadhi ya wadau wa burudani Bongo waliopo karibu na prodyuza huyo mkali wa Bongo Flava (ambao hawakupenda kutaja majina yao), walisema na safu hii kwamba kwakuwa mchizi hivi sasa jina lake lipo juu kuna uwezekano mkubwa akasepa katika studio hiyo na kwenda kutafuta mkwanja mrefu zaidi baada ya kumaliza mkataba wake na mmiliki wa studio hizo, Joachim Kimaryo a.k.a Master J.

Baada ya kupata data hizo, safu hii ilifunga safari mpaka ndani ya MJ Records na kupiga stori na Marco Chali kuhusiana na ishu hiyo ambapo alisema kwamba. “Ni kweli mkataba wangu ambao nilisaini Julai, 01, 2007 unaisha Julai 01 2009, namshukuru Mungu na napenda kuwaambia bado mi ni tunda la MJ Records, endapo bosi wangu ataridhia nitasaini mkataba mwingine wa miaka miwili, zoezi ambalo linaweza kufanyika mwishoni mwa wiki hii”.
***********

saili kwa wasanii kuendelea mikoani
Baada ya wasanii wengi chipukizi kujitokeza katika usaili wa kutafuta vipaji vitakavyoshiriki kucheza filamu zinazoandaliwa na Kampuni ya Tollywood, Dar es Salaam wiki hii, zoezi linaendelea katika mikoa mingine zilikotolewa fomu za ushiriki.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa filamu wa kampuni hiyo, Hamie Rajab, mkoa utakaofuata ni Morogoro ambapo zoezi la usaili kwa wasanii waliochukua fomu litafanyika Julai 7 na 8 mwaka huu, ikifuatiwa na Tanga ambako usaili utafanyika Julai 10 na 11, kisha Arusha Julai 13 na 14.

“Baada ya Arusha utafuata Mkoa wa Mwanza, usaili utafanyika Julai 17 na 18, tutamalizia na Zanzibar Julai 21 na 22 kisha washindi watakaopatikana watakutana Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa intavyuu ya mwisho kabla ya kuanza zoezi la upigaji picha wa filamu ya ‘Tears On Valentine Day’ Agosti mwaka huu,” alisema Hamie Rajab.
************

Mike T kitambi hichooo!
Miongoni mwa mastaa wa muziki wa kizazi kipya ambao wamenenepeana ghafla ni pamoja na Mike Mwakatundu a.k.a Mike T au Mnyalu, ambaye hivi sasa anaonekana kuwa na kitambi kwa mbali tofauti na ilivyokuwa miaka michache iliyopita, ShowBiz imelicheki hilo, Edna Katabalo anashuka nayo.

Inaonekana mchizi hivi sasa michongo imekaa sawa japokuwa yuko bize na familia yake baada ya kufunga ndoa hivi karibuni na kufanikiwa kupata bebi mmoja. Akiwa ni mwajiriwa wa Kampuni ya simu za mkononi, Zain pande za Morogoro. Mnyalu amesema na safu hii kwamba, kimya chake kunako gemu ya muziki hakijasababishwa na kuishiwa mistari bali ni ajira aliyonayo.

“Ukichanganya ajira na majukumu ya kifamilia niliyonayo nakosa muda mzuri wa kukaa na kuandika mashairi ukizingatia kuwa inanipasa kufanya kazi ambayo itanipatia kipato kizuri kitakachoniwezesha kutunza familia yangu, huu siyo wakati wa kuuza sura,” alisema Mnyalu.
***********


Fid Q “Usinikubali haraka ni ishu ya kweli”
Kama ulikuwa haufahamu , ShowBiz inakuhabarisha kwamba, ngoma mpya ya msanii Fareed Kubanda a.k.a Fid Q (anayeonekana katika picha ya ukweli hapo juu), ‘Usinikubali haraka’ ambayo imemshirikisha Seif Shaban ‘Matonya’ ni ishu ya ukweli ambayo imemtokea na hivi sasa yuko bega kwa bega na mrembo aliyekuwa akimsumbua mpaka kufikia hatua ya kumuandikia mashairi hayo.
********

Mkali wa mwezi monthly best performer
Baada ya kushuhudia ushindi wa msanii Marlaw mwezi uliopita, shindano bado linaendelea kwa kumsaka mshindi wa mwezi huu (Julai).

ShowBiz inakupa nafasi wewe msomaji na mpenzi wa burudani Bongo utuambie unadhani staa gani anastahili kuwa bora kwa mwezi huu?

Andika ujumbe mfupi (SMS) ukilitaja jina la msanii huyo kisha tutumie kupitia simu namba 0787-110 173. E-mail:mcgeorge@gmail.com.
**************


Thursday, July 2, 2009

WANAWAKE WAREFU KULIKO WOTE!!



VP unapokuwa na dem bomba na mrefu kuliko wewe? cheki zingine hapa:
NIFAHAMISHE.COM

Wednesday, July 1, 2009

BARBEQUE IN MILTON KEYNES


SUMMER FAMILY FUN DAY & BARBEQUE IN MILTON KEYNES, ON SATURDAY 11th July from 3:30pm to 11pm at CONNIBURROW PAVILLION,MILTON KEYNES,MK14 7AJ..Triple J'S Bring to you the best music varieties,family games,Along with BBQ (Nyama Choma) & Other foods. Entries £5 adults, Children Free. Food prices will start from £1, For more information please contact 07717624731 or 07946510798..


Thanks In Advance

Mdau MK