Saturday, January 2, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!



Yusuf mlela: Avuta zawadi zake Zizzou Fashion
Siku kadhaa baada ya kuibuka mshindi wa Ijumaa Sexiest Bachelor, Yusuf Mlela amekabidhiwa zawadi zake na aliyekuwa mdhamini mkuu wa mpambano huo, Athumani Tippo, kupitia maduka yake ya Zizzou Fashion.

Zizzou alitimiza ahadi hiyo ambayo ni pamba zenye thamani ya shilingi 500,000, Jumanne ya wiki hii kupitia duka lake lililopo pande za Victoria, Dar es Salasam ambamo Mlela aligonga shopping ya nguvu.

Baadhi ya pamba alizochagua Mlela Zizzou Fashion ni pamoja na suruali za jeans na kitambaa, tisheti, viatu, mashati, pafyumu, miwani na nyingine.

Akipiga stori na ShowBiz baada ya shopingi hiyo, staa huyo alisema kwamba amefurahishwa na utaratibu mzima wa kutolewa kwa zawadi hizo ambao haukuwa na dosari hata kidogo. “Nawashukuru sana ninyi waandaaji, heshima niliyoipata ni kubwa, hadi hii leo bado naendelea kupokea pongezi kutoka kwa mashabiki wangu waliopo sehemu mbalimbali. Nimefurahi sana”.
**************************************

Banza Stone
AY
Kanumba
2009..kwa hawa haukua poa sana

Albert Mangwea ‘Ngwair’
Ulikuwa ni mwaka mzuri kwake baada ya kufanya kazi nyingi nzuri zilizomrejesha kwenye chati baada ya kufulia kwa kipindi kirefu tangu alipotoa albamu yake ya kwanza A.K.A MIMI. Mwaka huu alitoa albamu inayoitwa NGE lakini wiki iliyopita alipata pigo baada ya kufiwa na baba yake mzazi.

MB Dog
Jina lake kamili ni Mohamed Mbwana, huyu apata pigo baada ya kufiwa na mwanaye wa kike katikati ya mwaka huu.

Banza Stone
Anaitwa Ramadhani Masanja. Mwaka ulianza vibaya kwa upande wake, aliugua kwa kipindi kirefu kiasi ambacho kuna watu walimzushia kifo. Hivi sasa yupo vizuri na tayari ameonekana jukwaani kwenye maonesho mbalimbali ya muziki wa dansi.

Prof. Jay
Mtu mzima a.k.a Daddy wa Mitulinga ambaye jina lake kamili linatambaa na herufi Joseph Haule, alipata balaa baada ya ndiga yake aina ya Mercedes Benz kupata ajali na kubondeka nyakanyaka. Wakati mzigo unadondoka, ulikuwa unaendeshwa na DJ Choka.

H. Baba
Hamisi Ramadhani Baba naye alipata balaa, mwaka huu alipata ajali na ajali na gari gari lake kuharibika. vibaya. Hata hivyo, mtu mzima huyo anayeiwakilisha Mwanza alisimama vizuri na kulitengeneza mpaka liliporudi barabarani.

Asha Baraka
Unaweza kumwita the Iron Lady kutokana na ungangari wake katika suala la kuhakikisha fedha inaingia. Yeye alipata balaa la kufiwa na baba yake mzazi hivi karibuni wakati tunaelekea kuumaliza mwaka 2009.

DJ Kim
Huyu ni muasisi wa Yo Rap Bonanza, jina lake kamili ni Abdulhakim Magomelo. Alifariki dunia hivi karibuni. Kwa wadau wa Bongo Flava, huyu ni muasisi, kwani ndiye aliyeweza kuibua vipaji vya wakali kama Mr. II a.k.a Sugu na kupaa matawi ya juu.

Ray C
Haukuwa mwaka mzuri kutokana na kukumbwa na misukosuko mingi ya kifedha, kiasi cha kuripotiwa na magazeti mara kwa mara kuwa amefulia.

Zay B
Hivi karibuni aliripotiwa kuwa amenusurika kupigwa risasi baada ya kuvamiwa na majambazi nyumbani kwao, kabla ya hapo aliripotiwa kulazwa hospitali moja iliyopo Tabata, Dar akisumbuliwa vidonda vya tumbo. Hakika haukuwa mwaka mzuri kwake.

Kanumba
Ni msanii wa Tanzania ambaye rekodi zinaonesha kuwa alifanya kazi nyingi ndani na nje ya nchi. Aliteuliwa kama staa wa Afrika kuingia jumba la Big Brother Revolution lakini baadaye badala ya kupongezwa, Watz wakamponda eti hawezi kushusha yai. Hii ilimchafua sana ingawa ilionekana ni zengwe la wenye wivu.

A.Y
Kwa upande wa staa wa commercial, Ambwene Yesaya, yeye alipata zahama kubwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwao, Sinza, Dar na kuibiwa zagazaga kibao, hivyo kumfanya jamaa aanze moja.

Jitaman
Jamaa siku hizi anapenda ajulikane kama Zagamba, yeye alipata ajali mbaya iliyokaribia kuutoa uhai wake. Watu walitangaza kuwa amefariki dunia lakini Mungu ameendelea kumfanya awe mmoja wa wanaovuta hewa hii ya oksijeni, ingawa ukimuona leo, hali ya sura yake yaani reception si kama zamani. Pole sana bro!
**************************************

Jordin-Sparks

Keri

2009 ulikuwa poa kwa hawa, ngoma zao zilibamba
Mwaka wa 2009 ulikuwa ni mzuri na mbaya kwa binadamu wengine, wapo waliopata matatizo ya hapa na pale, wapo waliofanikiwa na kuufurahia zaidi.

Kwa upande wa wasanii wa kiwanja ShowBiz inayo kila sababu ya kuwataja Soulja Boy, Keri Hillson, Jeremih, Jordin Sparks na Drake kuwa ndiyo mastaa waliotoka hivi karibuni na kufanya vyema zaidi 2009 kupitia ngoma zao kadhaa ambazo zilifunga mwaka kwa mafanikio.

Ngoma kama Kiss Me Thru The Phone ya kwake Soulja Boy ilibamba kiasi cha kuwafanya vijana wengi wa Kibongo kuipenda na kuitumia kama ringtone za simu zao. Ilipodondoka kazi yenye jina la Imma Star ya kwake Jeremih ikazidi kuwapagawisha vijana hao wa Kibongo mbali na zile za kina Jordin Sparks, Keri na Drake
*****************************************
Kikosi cha Mizinga, Rado, Wanaume Halisi, kuwania Mil. 2
Kutoka Block 41 pande za Kinondoni, Dar es Salaam tumedondoshewa ishu kwamba Kundi la Kikosi cha Mizinga, linaloongozwa na Kalama Masoud a.k.a Kalapina limeandaa shindano la ‘free style’ kwa baadhi ya wakali wa Hip Hop Bongo, ambalo litachukua nafasi kwenye ufukwe wa Coco leo na mshindi ataondoka na mkwanja taslimu shilingi 2,000,000 kwenye fainali zake zitakazofanyika Febrfuari 2010.

Mratibu wa ishu hiyo Kalapina alisema na ShowBiz kwamba, wakali kama Imam Abbas, Mansulii, LWP, Wanaume Halisi, Rado (Viraka), Serious Man, Dogo Sajo, Lufunyo, wao Kiklosi na wengineo watapanda stejini katika mpambano huo uliopewa jina la Hip Hop Battle King of Stage.

No comments: