Friday, January 8, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

AY
Joti
Tundaman

Mastaa waliokumbwa na kashkash za majambazi
Kupitia hapa, leo tumeona ni vema tuwacheki mastaa ambao kwa nyakati tofauti walijikuta katikati ya kashkash na majambazi, hivyo kuumia au kupata hasara.
Wakati tunagusa hili, ni vema ukawa na kumbukumbu kuwa hivi sasa Tundaman hajapona majeraha, baada ya kuvamiwa na majambazi ambao walimuibia na kumuumiza vibaya.

Tunda alikuwa safarini Afrika Kusini pamoja na Madee, aliporudi tu, usiku jamaa wakamvamia na kumpora zagazaga kibao, huku wakimuachia maumivu makali. Jamaa aliumaliza mwaka vibaya.

Mwanadada Gaidi, Zainab Lipangile ‘Zay B’ yeye mwaka jana aliumaliza kwa mtindo wa aina yake, baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na kuporwa vitu fulani fulani. Mbali na uporaji, jamaa walimlenga risasi lakini ikamkosa mwanamuziki huyo na kuingia kwenye mguu wa mdogo wake.

Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, yeye alivamiwa nyumbani kwake Mbezi miaka michache iliyopita, aliporwa zagazaga kibao, hivyo kuingia hasara kubwa.
Kati ya wasanii waliokumbwa na masahibu mwishoni mwaka jana, ni Ambwene Yesaya ‘AY’, yeye alivamiwa nyumbani kwake Sinza na kuporwa vitu kibao, na baada ya hapo jamaa akaamua kudumisha ulinzi kwa kuajiri Mmasai.

Mkali Dulayo yeye alivamiwa barabarani na kuporwa na vibaka wanaotumia silaha hatari, wakati Dully Sykes na Mr. Blu wao ilikuwa mitaa ya Tabata ambapo walitekwa na wahuni kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa. Hii iliripotiwa gazetini.

Kundi zima la Orijino Komedi liliingia kwenye kashkash ya majambazi mwaka jana, wakati memba wote walipokuwa wanaishi pamoja kwenye nyumba moja iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.

Baada ya kuvamiwa, wasanii wa kundi hilo, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Emanuel Mgaya ‘Masanja’, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Joseph Shamba ‘Vengu’, waliporwa fedha na vitu vingine vya thamani.
**************************************
**************************************

Veto ya Sugu yakubalika kitaani
Albamu mpya ya mwana Hip Hop ‘bei mbaya’ Bongo, Joseph Mbilinyi ‘Mr. II’ inayokwenda kwa jina la Veto, tayari imeanza kukubalika, kutokana na idadi kubwa ya Wamachinga kutoa ripoti chanya kuhusu mauzo.

Wamachinga walioripoti kwa mtu mzima Sugu a.k.a Mr. II katikati ya wiki hii, walisema kuwa jinsi wanavyosumbuliwa mtaani na wadau wanaoiulizia Veto, ni wazi kwamba inakubalika, hivyo wengi wanapenda kuipata.

Akiongea nasi juzi, Sugu alisema kuwa ameona Wadosi ambao walikuwa wanauza zamani ni wazinguaji, hivyo ameamua kubadilisha upepo kwa kuuza mwenyewe, akiwatumia Wamachinga nchi nzima ili kupata fedha yenye maelezo halisi.

“Watu wananipigia simu, wananiuliza Veto vipi? Wadosi wanatuumiza, kwahiyo tunasambaza na Wamachinga, kwahiyo popote pale mdau akimuona Mmachinga amwite amuulize Veto, atapata albamu bora ya Hip Hop,” alisema Sugu.
compiled by mc george

No comments: