Friday, January 22, 2010

IJUMAA WIKIENDA




Kifo cha Bongo Flava: Malengo ni tatizo kubwa
Yap, tunaongelea kifo cha Bongo Fleva, wadau wanasema muziki unaelekea kaburini. Mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin Maalim Gurumo aliwahi kusema Bongo Flava ni kama ‘beg gee’ kwamba una utamu wa muda mfupi na unachosha mapema.

Leo ni miaka michache tangu mkongwe huyo alipotoa kauli hiyo na kweli Bongo Fleva inaelekea kaburini. Inakufa tunaiona! Matatizo ni mengi yanayosababisha muziki huo uchinjiwe baharini, leo tunaangalia kipengele kimoja. Malengo!

Last week kupitia hapa, tulieleza kuwa uwezo mdogo wa kutoa shoo jukwaani ni tatizo nambari wani lakini leo tunaongelea malengo kama sehemu nyingine ya matatizo, yanayochangia kifo cha Bongo Fleva.

Malengo! Exactly. Wasanii hawapo serious kuchangamsha ubongo wao kujua nini kilichopo kesho na wafanye lipi kuhakikisha ikifika keshokutwa wanaendelea kuwa juu kwenye soko la muziki.

Wanamuziki wengi hawajui kujipanga, wakipata vijisenti leo, wanashindwa kuwa wabunifu. Mtu anapokosa ubunifu maana yake hana malengo ya kufika mbali. Tusibishane!

Angalia mastaa waliojikusanyia pesa nyingi kwenye muziki wao, tena kwa fujo, leo hii wapo choka mbaya, hawakubaliki tena! Zaidi ya miongo miwili yupo kwenye game, Busta Rhymes bado yupo sawa na anakubalika kibiashara, lakini leo waliovuma mwanzoni mwa miaka ya 2000 Bongo, wapo mahututi.

Yupo wapi Nature a.k.a Mfalme wa Kighetto ghetto, au Inspector Haroun a.k.a Mfalme wa Rap Katuni? Hao ni mifano tu, waliliteka soko la Bongo Fleva lakini leo yanayowahusu ni ya kusikitisha.

Hii ni mbaya sana, inabidi wasanii wetu kuwa na malengo ya kuwepo kwenye game muda mrefu kwa sababu inapotokea kuporomoka ghafla tena baada ya kuvuma kwa muda mfupi, it does not make sense!
**************************************

Johmakini ni funiko la chuma East Africa
Kutoka hapa, wiki iliyopita tuliwaletea shindano baabkubwa, tukiwataka wasomaji waweze kutuma maoni yao wakimtaja msanii ambaye anafunika jukwaani.

Matokeo ni kwamba mwana-Hip Hop, John Simon a.k.a Johmakini ni nambari wani, hii ni kutokana na wingi wa kura ambazo tulizipokea kutoka kwa wasomaji.

Johmakini a.k.a the Man of Hip Hop Swagger amekusanya kura nyingi huku mwana Nako 2 Nako Soldiers, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ akikamata nafasi ya pili.

Mchizi kutoka Kenya, Juacali a.k.a Genge Master anashika nafasi ya tatu, huku mchizi wa Uganda, Joseph Mayenja ‘Chameleon’ akitajwa namba nne.

Mr. Salary, Nameless yupo namba tano, Redson ametajwa wa sita, kichaa wa Genge, Nonino amebakizwa nafasi ya saba na Bebecool na Boby Wine wamefungana katika 8 track.

Nice Lucas Nkenda ‘Mr. Nice’ yupo nafasi ya tisa, Khaleed Mohamed ‘TID’ namba 10, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ anasimama 11, huku Abdul Sykes ‘Dully’ ni wa 12.
Wasanii wengine waliopewa alama za juu kwa kazi nzuri jukwaani ni Hamis Ramadhani Baba ‘H. Baba’, Blu3, Wahu na Juliana Kanyomozi wa Uganda.
*********************************



Twanga: Kuutambikia 2010 leo, Fresh Jumbe wiki ijayo
Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, imeazimia kufanya mambo makubwa mwaka 2010 na leo itafanya tambiko zito kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Landmark, Ubungo, Dar es Salaam.

Twanga a.k.a Kisima cha Burudani, kitafanya tambiko hilo kwa kutoa burudani kali kwa mashabiki wake, lengo likiwa kuukaribisha vema mwaka 2010 na kutambulisha kazi mpya kwa mashabiki wake.

Mkurugenzi wa African Stars Entertainment Tanzania (ASET), Asha Baraka aliliambia gazeti hili mapema wiki hii, jijini Dar es Salaam kuwa timu nzima ya Twanga imejipanga kwa ajili ya kuukaribisha mwaka leo.

“Hii ni shoo maalum ya bendi yetu kwa ajili ya mashabiki wetu, tutatoa burudani ya kiwango cha juu ili kuwadhihirisha mashabiki wetu kwamba 2010 bado tupo fiti na tutaendelea kufunika,” alisema Asha.

Wakati huo huo, Ijumaa inayokuja a.k.a next Friday itakuwa patashika nguo kuacha mwili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Landmark, Ubungo, Dar wakati mwanamuziki wa kimataifa Bongo, Fresh Jumbe na timu kamili ya Twanga Pepeta watakapokuwa kazini.

Fresh ambaye anafanya maisha yake ya muziki nchini Japan, yupo Bongo kwa ajili ya shoo mbalimbali na nambari wani ni ile ya Ijumaa ijayo ndani ya Landmark Hotel, Ubungo.
COMPILED BY MC GEORGE

No comments: