Tuesday, January 19, 2010

UKWELI KUHUSU UNYWAJI KAHAWA


YOU ARE WHAT YOU EAT
Kahawa ni miongoni mwa vinywaji maarufu sana duniani. Mamilioni ya watu hunywa kahawa kila siku, ama wakiwa nyumbani, ofisini au matambezini. Ladha nzuri na uchangamfu anaoupata mtu baada ya kupata kikombe kimoja au viwili, ndiyo sifa pekee na kubwa iliyonayo kahawa.

Kutokana na umaarufu na matumizi yake kuwa makubwa kiasi hicho, tafiti kadhaa za kisayansi zimefanyika na zinaendelea kufanyika ili kujua faida na hasara za kinywaji hiki katika afya ya binadamu.

Baada ya tafiti nyingi kufanyika, ukweki umedhihirika kuwa kahawa inapotumika kwa wastani, haina madhara kiafya bali ina faida. Wastani unaozungumziwa hapa, ni ule wa kunywa vikombe vya ukubwa wa watsani visivyozidi vinne mpaka vitano kwa siku.

Aidha, mwongozo uliotolewa hivi karibuni na Wakala wa Viwango vya Vyakula wa nchini Uingereza, umependekeza kuwa wanawake waja wazito wasinywe kahawa zaidi ya vikombe viwili kwa siku, sawa na miligramu 200.

Katika muongozo huo, imetahadharishwa kutokuzidisha kiwango cha ‘caffein’e mwilini kwa kunywa vinywaji vingine pia ambavyo vina kiasi kikubwa cha ‘caffeine’ ikiwa ni pamoja na vinywaji baridi kama Coca-Cola, Chai, Chokoleti na vinywaji vingine vya kuongeza nguvu.

UHUSIANO WA SARATANI NA KAHAWA
Utafiti na makala nyingi zilizoandikwa kuhusu ugonjwa wa saratani, zinaonesha kuwa binadamu tunaweza kujiepusha kwa asilimia 35 na magonjwa mbalimbali ya satarani, kwa kuzingatia lishe bora na kubadili mtindo usiofaa wa maisha.

Kila mwaka, zaidi ya watu milioni 10 duniani hupatwa na saratani na zaidi ya watu milioni 6 hufariki dunia kutokana na magonjwa mbalimbali ya saratani. Tafiti mbalimbali zimefanyika kuhusu unywaji wa kahawa na uwezo wa kahawa kuzui au kusababisha saratani.

Matokeo ya utafaiti huo, umeonesha kuwa unywaji wa kahawa hauna athari mbaya zinazohusiana na ugonjwa wa saratani na badala yake kuna uwezekano mkubwa wa kahawa kutoa kinga kwa aina kadhaa za saratani.

Aina za saratani zilizofanyiwa utafiti kwa kuoanisha na matumizi ya kahawa ni pamoja na Saratani ya Kizazi (Ovarian Cancer), Saratani ya Kibofu cha Mkojo (Bladder Cancer), Sratani ya Tumbo (Bowel Cancer), Saratani ya Ini (Liver Cancer) na Saratani ya Kongosho (Pancreatic Cancer).

Katika hitimisho lao, jopo la wataalamu kutoka Mfuko wa Dunia wa Utafiti kuhusu Saratani, wapatao 21 ambao wanahehsimika duniani, baada ya kupitia na kutathmini tafiti 7000 kuhusu matumizi ya vinywaji pamoja na kahawa, walihitimisha kwa kusema kuwa ni dhahiri kahawa haihatarishi mtu kupatwa na saratani ya kongosho wala figo.

Zaidi ya hayo, taarifa zilizopo za kisayansi zinaonesha kuwa unywaji wa kahawa siyo sababu ya mtu kupatwa na saratani ya aina yoyote katika mwili, bali kahawa imeonesha kuwa kinga ya baadhi ya saratani, hususani Saratani ya Ini, Saratani ya Utumbo mdogo na Saratani ya Kizazi. Muhimu mtu azingatie kiwango.

3 comments:

Unknown said...

BRO, THANK U VERY MUCH FOR TAKING CARE OF OUR HEALTH.

GOD BLESS U

SCHOLA

Anonymous said...

Thnx 4 dat bro for letting us know.......

Moses Kivunge said...

Kuna mtu alisema never ask google quations about health na sasa nimeamini nimetoka kusoma mda si mrefu kuwa kahawa inaweza sababisha saratani huku naambiwa inauwezo wa kuikinga saratani sasa which is which ukizingatia sioni reference zozote.....bongo bwana nadhani inabidi utupatie reference juu ya information zako kutoka watu mbalimbali walio fanya research juu ya kahawa. Maana unaweza shukuru upo salama katika kutumia kahawa kumbe hakuna usalama.