Zay B: huu ndiyo mjengo wangu na ndinga yangu, nani anasema nimefulia?
Kutoka Bongo mwana Hip Hop wa kike aliyeleta mapinduzi katika game ya muziki wa kizazi kipya kwa upande wa wasichana, Zainabu Lipangile a.k.a Zay B (PICHANI JUU) mwishoni mwa wiki iliyopita alidondoka ndani ya safu hii na kupiga stori mbili tatu ikiwemo kutangaza baadhi ya aseti anazomiliki hivi sasa kama alivyofanya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.
Ndani ya safu hii Zay B alisema kwamba wapo baadhi ya watu, wakiwemo wasanii wenzie wamekuwa wakivumisha maneno mitaani kwamba hivi sasa amefulia baada ya kupotea kwenye game kwa muda mrefu kitu ambacho amekikanusha, ndiyo sababu iliyomfanya atangaze mali zake.
“Unajua watu wengine huwa wanakosa ishu za kuongea, mimi kutosikika siyo kwamba nimefulia, kuna ishu kibao nafanya zinazoniingizia kipato, kwanza muziki wa Bongo haulipi na umejaa majungu. Ningekuwa nimefulia ningeweza kujenga nyumba au kununua gari?” Alihoji Zay B huku akionesha picha za nyumba yake zilizokuwa kwenye simu.
Mwanadada huyo alisema kwamba mjengo huo ameushusha pande za Buyuni, Pugu nje kidogo ya Dar es Salaam huku akimiliki gari aina ya Toyota Premio. “Mbali na hayo pia nimesaini mkataba wa kufanya kazi ya muziki na Kampuni ya Butile Africa Group ya Afrika Kusini, watu wasifikiri nipo nipo tu, sijafulia kihiivyo,”.
*******************
Bob Haisa ajitokeza!
Siku kadhaa baada ya safu hii kugonga ishu iliyomhusu staa wa muziki wa mduara kutoka pande za Mwanza, Haisa Mbuya a.k.a Bob Haisa iliyobeba kichwa cha habari “Bob Haisa yupo kama hayupo” mchizi ameibuka na kuweka kila kitu fresh.
Akipiga stori na safu hii mwishoni mwa wiki iliyopita huku pembeni akiwa na waifu wake, Sweet K, Haisa’ alisema, siyo kwamba hayupo isipokuwa kitu kinachomfanya asisikike kwa sana hivi saa ni kutokuwa na meneja wa kudili na muziki wake.
“Mimi nipo na albamu yangu, Safari ya Mwanza bado ipo mtaani inafanya poa, isipokuwa hivi sasa sina meneja, niliamua kujitegemea mwenyewe baada ya kugundua kampuni nyingi zinazowasimamia wasanii zinaweka maslahi yao mbele zaidi kuliko sisi,” alisema.
***********************
Fresh Jumbe adondoka Bongo kwa kazi moja!
Mkongwe wa muziki wa dansi nchini ambaye maskani yake ni kule pande za Japan, Fresh Jumbe amedondoka Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya kugonga kazi moja ya ukweli kunako Tamasha la Sauti za Busara litakalofanyika mapema mwezi ujao Visiwani Zanzibar.
Akipiga stori na Abby Cool & MC George over the Weekend muda mfupi baada ya kukanyaga ndani ya Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, Jumbe alisema kwamba ishu iliyomfanya aje Bongo mapema wakati shoo bado ni maumivu aliyonayo moyoni kwa wasanii wenzie wa nyumbani ambao kazi zao zinashindwa kupenya kwenye sikio la Kimataifa.
“Nataka kushirikiana na wasanii wenzangu wa hapa nyumbani kuhakikisha muziki wetu unauzika hadi nje ya bara la Afrika. Kabla sijaenda Zanzibar nitafanya shoo na Twanga Pepeta na kukaa na wanamuziki wengine wa dansi ili kujadili ni jinsi gani tunaweza kuuvusha muziki wetu mbali zaidi,” alisema Jumbe.
*****************************
Ray C akubali kutoka na Prodyuza
Prodyuza ‘yanki’ anayepiga dili kupitia game ya muziki wa kizazi kipya, Victor Faiz Bahaj ameamua kuingiza voko mwenyewe huku akimpa shavu staa wa sanaa hiyo, Rehema Chalamila a.ka. Ray C’.
“Ngoma itakwenda kwa jina la Mahabuba na tayari Ray C amekubali kutoa sapoti ya kutosha kwangu. Nataka kuja kivingine katika muziki, naamini hii ngoma itakayofanyika One Record itafanya maajabu,” alisema Victor.
compiled by mc george
No comments:
Post a Comment