Monday, January 25, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Meseji ya leo: Watoto wa kishua wameiua Bongo Fleva
Hii ni meseji nyingine kuhusu kifo cha Bongo Fleva, mambo mengi yanazungumzwa kama vile wasanii kutokuwa na malengo, ubunifu lakini kuna pointi ya msingi ambayo inasahaulika.

Ni lazima ujue Bongo Fleva ilianza vipi, hapo ndipo utaweza kutambua ni kwanini inakufa. Utapata jibu kwa kuangalia hali halisi ya game la kipindi hiki.

Ukweli ni huu; Bongo Fleva asili yake ni muziki wa uswahilini. Kule kwenye maneno ya shombo. Watu wake wao hawataki tambo za utajiri, wanahitaji kufarijiwa kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili.

Hata kama ukiwaimbia mapenzi, basi yawe ni yale yanayowahusu. Si mashairi ya ufukweni, ndani ya jumba la kifahari, tiles kila kona. Mazingira hayo huona hayawahusu na mara moja watakataa traki yako.

Can u imagine when Bongo Fleva was on air? Nyimbo zilizotamba ni zile zenye ujumbe, wakali waliofunika wote walitoka uswahilini a.k.a uswazi. Walipoanza kuibuka watoto wa kishua na muziki ukaondokewa ladha yake, leo tunauona unakufa.

Angalia nini alichokuwa anaimba Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Mikononi mwa Polisi, Hali Halisi, Busara na nyingine, zilikuwa zinaamsha hisia za watu wenye maisha duni ambao walikuwa wakikumbana na shuruba za kila siku, ikiwemo kukamatwa na kusingiziwa kesi na polisi.

Angalia Chemsha Bongo ya Hard Blasters Crew (HBC) na albamu nzima Funga Kazi 2000. Mawe yaliyokuwemo yalikuwa na ujumbe ambao watu wanaojua nini maana ya shida waliupokea kama faraja kwao, kwa kuona kwamba angalau wasanii wanakumbuka shida zao.

Hujiulizi kwanini Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, Haroun Kahena ‘Inspector’, Kalama Bakari ‘Luteni’ wa Gangwe Mob walikuwa mastaa wakubwa waliotawala soko la muziki. Mabaga Fresh walivyoonesha nini maana ya watu dhiki na life ya kisamjo!

Nature na Ugali aliijaza Diamond Jubilee mpaka pomoni, pia Gangwe walitia nyomi kwenye ukumbi huo kwenye uzinduzi wa Simulizi za Ufasaha, wakajaza PTA a.k.a Sabasaba au siku hizi Mwalimu Nyerere Square katika utambulisho wa albamu ya Nje Ndani.

Inspector akajaza nyomi PTA tena alipozindua albamu ya Pamba Nyepesi. Maonesho yote ya Bongo Fleva yaliyokusanya idadi kubwa ya mashabiki, asilimia kubwa ya watu walitoka uswazi, huko ndiko kwenye mizuka.

Watoto wengi wa Kishua maonesho yao hayajazi, wale wenye muziki wao ndiyo siku hizi mara wanabaniwa, ooh ubunifu hamna, pesa ya kuingia studio inasumbua.

Watu wanataka mistari, “Jumba la udongo choo cha makuti passport size” ninyi mnawaletea “naendesha gari kama la Obama, demu wangu anafanya shopping Brooklyn” ndiyo maana Bongo Fleva inakufa.

Watoto wa kishua hawajui shida ndiyo maana tungo zao ni kusifia matumizi ya hela, wanawake, magari. Ujanja kidogo na kukubali kujikosoa, Bongo Fleva itarudi kwenye chati.
*******************************************

Jokate: King & Queen yamuweka levo nyingine
Miss Tanzania namba 2, 2006-07, Jokate Mwegelo yupo levo nyingine, hii ni kwa mujibu wa traki babkubwa ‘Kings & Queens’ ya mkali Ambwene Yesaya ‘A.Y’.

Ndani ya ngoma hiyo, A.Y kawashirikisha Jokate na Cecilia Wairimu ‘Amani’ lakini stori ni jinsi Miss Tanzania huyo alivyoweza kufanya performance ya kiwango cha juu katika audio na video ya wimbo huo.

Ndani ya traki hiyo, Jokate anaitikia vizuri katika chorus ambayo amefanya na A.Y, upande wa kideoni, Miss Tanzania huyo yupo sawa, kacheza vizuri na kamera, pia mdomo hauachi sauti. Anastahili pongezi.

Yote kwa yote ni kwamba Kings & Queens imetulia, A.Y kasimama vema kama kawaida, Amani amezidi kuing’arisha traki. Big Up!


cheki video ya wimbo huo

*************************


H. Baba: Nimetupiwa uchawi na fulani
Mtaalam wa muziki wa TAKEU, Hamis Ramadhan Baba ‘H’, amesema kuwa ametupiwa uchawi na mwanamuziki mwenzake ambaye tunambakiza anonymous mpaka hapo baadaye.

H. Baba, alifanya straight talk to Abby Cool & MC George over the weekend na kusema kuwa kutokana na kutupiwa uchawi na fulani, mambo yake mengi yaliharibika kiasi cha kuachana na aliyekuwa mchumba wake, Irene Uwoya ‘Kataut’.

“Sasa hivi nina nafuu baada ya kupata tiba, huko nyuma nilikuwa sijielewi kabisa, nikafuatilia nikagundua kwamba kumbe nimerogwa. Mambo yangu mengi yaliharibika, niligombana na watu wengi na nikawa sijielewi.

“Ni kweli kabisa kikulacho kipo nguoni mwako, mchawi wangu ni rafiki yangu, tulikuwa tunashauriana mambo ya muziki lakini kumbe ananiroga, mwanga mkubwa! Nimemjua na sasa hivi nimepona.

“Matatizo mengi yalitokana na Irene, unajua watu wengi hawakupenda niwe na Irene, kwahiyo ili kunikomoa ikabidi waniroge, mimi na Irene tukawa hatuelewani, tunagombana mpaka tukaachana,” alisema H.

Hata hivyo, H. Baba alisema kuwa hivi sasa yote amesahau na anajipanga vema kwa ajili ya albamu yake mpya, inayokuja kwa jina la Goma la Uswazi ambayo itaundwa na mawe manane yenye akili.

Irene kwa sasa ni mke wa mwanasoka wa kimataifa wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alifunga ndoa Julai mwaka jana.
*******************


Solange Knowles: Only guys wawili waliomcheki kitandani
Ni habari ile ile ya kuangalia ni staa gani kachetuka na nani, ni full kumulikana, Ebwana Dah! This week, Solange Knowles yupo chamber na hapa inawekwa hadharani orodha ya wanaume ambao kwa nyakati tofauti wamemcheki on bed.

Solange, mdogo wa mwanamuziki superstar, Beyonce Gissele Knowles, anatajwa kujikunja na wanaume wawili tu katika vipindi tofauti.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja wenye ofisi zake kwenye himaya ya Obama a.k.a Marekani, Julez Santana ndiye kidume anayetajwa wa kwanza kuchangamsha damu na Solange, ingawa haitajwi ni lini ‘walifanzana’ kweli na kuachana huku wakiwa wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.

Daniel Smith yupo nambari ‘bee’, yeye anatajwa kuanza kupumzika na mrembo huyo mwaka 2004 kabla ya kuamua kumchukua jumla kwa ndoa takatifu. Ndiyo maana yake!

Jina lake kamili ni Solange Piaget Knowles, ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo. Urefu wake ni futi 5 na inchi 8. Alizaliwa Juni 24, 1986, Houston, Texas, Marekani, ni muumini wa madhehebu ya Methodist.

Amewahi kufanya kazi na rapa dogolee, Lil Romeo, pia ni mwandishi wa nyimbo za mastaa mbalimbali akiwemo Kelly Rowland.
*******************


Fresh Jumbe: Wakongo wanatawala soko la dansi Bongo
Galacha wa muziki wa dansi Bongo, Fresh Jumbe Mkuu yupo nchini huku leo ikiwa ndiyo kwanza anafunga wiki tangu alipowasili kwenye ardhi ya JK.

Yupo hapa kwa ajili ya kutoa shoo kali za muziki wake, Ijumaa ya wiki hii yupo kwenye Ukumbi wa Landmark Hotel, Ubungo, Dar es Salaam hapo atashirikiana vema na Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.

Fresh pia anajiandaa kwa ajili ya Tamasha la Sauti za Busara ambalo amealikwa, litakalofanyika pande za visiwa vya marashi ya karafuu, Zanzibar kama kawa.

Katika ‘intavyuu’ na mwandishi wetu, Hemed Kisanda, Fresh anasema kuwa muziki wa dansi wenye asili ya Kitanzania umefunikwa kwa kiwango kikubwa na ule wenye ladha ya Kongo.

Kutokana na hilo, Fresh akasema kuwa havutiwi na hali iliyopo kwamba soko la muziki wa dansi linakuwa mikononi mwa Wakongo, wakati ‘enzi za mwalimu’, Wabongo walijidai sokoni na kwenye maonesho yao kumbi zilijaa.

“Enzi hizo tulifanikisha muziki wetu kuwa juu tofauti na ilivyo sasa,” anasema Fresh ambaye anafanya maisha yake ya muziki nchini Japan.

Fresh ambaye amewahi kuzitumikia bendi mbalimbali nchini wakati huo kama DDC Mlimani Park, Juwata Jazz, Bicco Stars, Safari Sound na Dar International, anasema kuwa dhamira yake ni kufika mbali kisanii.

Anawataja mastaa wa Afrika ambao wanampa ‘mzuka’ wa kuumiza kichwa ili afikie rekodi zao kuwa ni Angelique Kidjo, Yosou Ndour, Yvonne Chakachaka na Hughes Masekela.

compiled by mc george

No comments: