
Hisia hizo zimeibuka baada ya msanii huyo kuonekana akitangaza Kipindi cha Afro Beat hivi karibuni na kurudiwa mara kadhaa na kituo hicho, huku akimwagiwa sifa kuwa alikamua vizuri sana.
Baada ya Mai wa Jesse kuhamia TBC 1 kipindi hicho kimekuwa hakina mtangazaji maalum, lakini nyepesi nyepesi kutoka kwa chanzo kimoja kilichopo Channel 5 zinasema kwamba muongozaji wa kipindi hicho, Josiah Murungu akishirikiana na Musa wamekuwa wakiendesha zoezi la kumsaka mrithi wa Mai kimya kimya.
Koleta alipopigiwa simu ili aeleze kama amepata ajira katika kituo hicho, alisema hana taarifa zozote, lakini ni kweli alitangaza kipindi hicho kwa siku moja.
“Sijui chochote kaka yangu, niliombwa na akina Josh nitangaze, nikawaambia wanipe muda nijiandae wakasema watanipa maelekezo mafupi kabla ya kurekodi, nilipowakubalia, wakanielekeza kisha nikarekodi,” alisema Koleta.
Alipoulizwa kama alikuwa na taarifa za shindano la kumsaka mrithi wa Mai, alisema: “Sijaambiwa kama nashindana, kwa ujumla sijui chochote.”
1 comment:
Mh1 huyu niliyemuona jana Gymkhana kaongozana na watoto si rizki???
Post a Comment