Beatrice Moses: Watoto watatu hawanizuii kufanya muziki
Inawezekana ishu hii ikawa kama ‘sapraiz’ kwa wasomaji wengi wa ShowBiz au mashabiki wa msanii Betrice Moses ambaye ni zao la BSS 2009 aliyesimama katika game ya muziki wa kizazi kipya hivi sasa akiwa na ngoma yenye jina la ‘Acha waseme’ ikiwa pamoja na video yake.
Kama haujafahamu bado, mbali na kushiriki vyema kunako shindano la BSS na kuonesha uwezo mkubwa katika shoo zake, msanii huyo (picha kubwa katika pozi) ni mama wa watoto wa watatu ambao ni Milee, Abel na mdogo wao Vaines na kwamba yuko taiti na game ili kuhakikisha madogo hao wanapata mahitaji yote ikiwemo elimu.
Akipiga stori na ShowBiz msanii huyo alitamka kwamba, haoni sababu ya kuficha kuwa ana familia kama ilivyo kwa mabinti wengine kwakuwa kwake anajivunia watoto na hata anapoonekana kuwa ‘tait’ na game ya muziki mashabiki wake watambue kwamba majukumu ndiyo yanampa mzuka zaidi wa kazi.
“Huwezi amini, nilijifungua mwanangu wa kwanza nikiwa na umri wa miaka 18, mpaka sasa nina miaka 25, kipindi chote hicho nilikuwa tayari kwenye game ya muziki, japo sikuwahi kutoka kama ilivyo sasa. Wanangu wapo kwa bibi yao (mama yake mzazi) Mwanza pande za Igogo wanaendelea na shule huku mimi na baba yao tukiendelea kuwasapoti kwa kila kitu,” alisema Beatrice.
Kuhusu game msanii huyo ambaye atakuwa mwenyeji wa tamasha la Fiesta 2010 pande za kwao, Kanda ya Ziwa alisema kwamba, baada ya kufanya vizuri na ngoma hiyo, Acha waseme siku kadhaa zijazo atasimamisha jiwe lingine kati ya mawili aliyokwisharekodi. “Zipo ngoma mbili, Dance floo na Ndiyo sababu ambazo nitazikabidhi kwa wadau ili wachague moja ambayo itakwenda hewani, naomba mashabiki wangu waendelee kunipa sapoti ili niongeze mzuka zaidi,”.
Dodoma
rrraaaa!! rrraaaaa!!
Dodoma mko tayari kujipangusaaa!! Nalizungumzia Tamasha la Fiesta 2010 ambalo lilianza kupagawisha katikati ya wiki iliyopita pande za Morogoro, ikifuatiwa na Arusha na Moshi na sasa ni zamu ya watu wa Dodoma kuondoa matatizo yao kupitia shangwe hizo ambazo zitapigwa kesho ndani ya Uwanja wa Jamhuri.
Primetime Promotion ndiyo waandaaji, ndani ya safu hii wamesema kwamba kama ilivyokuwa sehemu nyingine zilizotangulia ndivyo itakavyokuwa Dodoma kwasababu huwa hawabahatishi na kwamba idadi ya wasanii watakaodondoka pande hizo itakuwa ya kutosha.
Baadhi ya wasanii waliotajwa kushuka Dom ni pamoja na Juma Nature, Fid Q, Keisha, Madee, Kassim, Tundaman, Johmakini, Bele 9, Barnaba, Mwasiti, Linah, Amini, Diamond, Godzilla, Roma, Niki wa Pili, Young Dee, Mataluma na wengine kibao.
Baada ya pande hizo msafara utaelekea Tanga kwa shughuli
kama hiyo huku timu ya wasanii ikizidi kuongezeka.
Waandaaji hao walisema kwamba, baada ya Tanga, mzigo utatua Zanzibar, kisha Kanda ya Ziwa kabla ya kurudi Dar na kuangusha burudani ya ukweli kwa shoo itakayopigwa kunako sehemu itakayotajwa hivi karibuni.
Fella Ageukia kaswida
Wengi wanaweza wakashangaa na kujiuliza inakuwaje? Lakini kwake iko poa tu kwakuwa ni muumini mzuri wa Dini ya Kiislam ndiyo sababu iliyomsukuma kugeukia pande hizo na kufanya kazi ya Mungu mpaka kukamilisha albamu yenye nyimbo nne za Kaswida ikiwa na jina la Mazingira.
Namzungumzia Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Hassan Fella ambaye amesema na ShowBiz kwamba, kila kitu anachofanya na kufanikiwa ni mapenzi ya Mungu ndiyo sababu kubwa iliyomfanya ageukia upande huo kwa kuwasaidia vijana wa Chuo cha Kiislamu chenye jina la Al-Madrasaty Salama kilichopo Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam.
“Mkubwa tumetoa albamu au Nashdi, inaitwa Mazingira ikiwa na Kaswida 4 ambazo ni Ndoa, Ukimwi, Rushwa na Mazingira yenyewe. Pia tumetoa na video yake ikiwa kwenye DVD na VCD kazi zote tunasambaza wenyewe, kwa mara ya kwanza tutazitambulisha Agosti mosi mwaka huu,” alisema Fella.
Mume wa Christina Millian abambwa na kimwana beach
Kwa wale wapenzi wa mastaa wa kiwanja, akiwemo mrembo Christina Millian na mumewe Dream, hii ishu inaweza ikawa inawahusu na kutamani kuijua. Kwa mujibu wa mtandao wikiendi iliyopita mume huyo wa Millian alibambwa na kimwana mwingine wakijiachia ufukweni.
Mtandao mmoja unaodili na michongo ya mastaa wa mbele ulisema kwamba, wikiendi hii kulikuwa na mshangao wa ajabu juu ya picha za mume wa Christina Millian, Dream yule aliyeandika, Single ladies (Put your ring on) ya Beyonce baada ya paparazi kupata picha zake akiwa na kimwana mweupe badala ya mkewe Christina, watu wengi walishtuka na hakuna aliyeamini.
Muda mfupi baadaye Christina aliamua kutupia maneno kwenye ukurasa wake wa twitter akisema kwamba. “Hivyo ndivyo ilivyo, amini mnachokiona machoni mwenu”. Dream alipohojiwa na jarida la Us alisema kwamba, yeye na mwanamuziki Christina Millian waliachana tangu mwaka jana, waliamua tu kuweka habari “private” kwa kumlinda mtoto wao Violet mwenye miezi sasa. Inasemekana mpaka sasa Christina bado yuko na pete ya ndoa mkononi.
compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments:
Post a Comment