Miaka 10 ya Jide: Kuwakumbusha mashabiki wake alipotoka
Akiwa amepitia milima, mabonde na vikwazo kibao mpaka kufikia mafanikio aliyonayo leo, mwanadada Judithi Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee yuko tayari kusheherekea miaka kumi tangu aingie kwenye game ya muziki wa kizazi kipya kunako miaka ya 2000.
Mwanadada anayo kila sababu ya kusheherekea kwakuwa tangu ajitupie kwenye fani miaka kumi iliyopita, hajawahi kushuka chini au muziki wake kutosikika kwa muda mrefu kupitia vyombo mbalimbali vya habari tofauti na baadhi ya mastaa alioanza nao safari ambao hivi sasa hawajulikani walipo.
Uvumilivu na mishemishe alizogonga mpaka kufikia hatua ya kumili bendi yenye jina la Machozi vinaifanya a.k.a yake, Komando kuwa ya ukweli zaidi kwani ameonesha ni jinsi gani ni jasiri katika kupambana kwa kuipigania sanaa yake mpaka ikampeleka mbali.
Kupitia blog yake Jide amedondosha maneno yanayosomeka hivi.
“Tarehe 6 August ni Show Kubwa ya Miaka 10 Ya Lady JayDee….chagueni nyimbo mnazopenda kuzisikia, nitajaribu kugusa kuanzia, Machozi, Binti, Moto, Shukrani na Album ya Combination ya Machozi Band”.
Kama bado haujafahamu ishu hiyo ita-take place pande zipi, mpango mzima utachukua nafasi Mzalendo Pub iliyopo ndani ya mjengo wa Millenium Tower, Makumbusho, Dar es salaam. Sisi kama ShowBiz ambao ni wadau wa burudani Bongo tunaungana na mwanadada Jide katika furaha yake ya kutimiza miaka kumi kwa mafaniko japo bado safari yake kimuziki inaendelea.

Mwanadada aliyetengeneza jina kupitia shindano la kufatuta vipaji, Bongo Star Search 2008, Beatrice William, kupitia ShowBiz amedondosha ushauri wake kwa shindano hilo kwamba hivi sasa wanatakiwa kuangalia mshiriki gani ambaye ana uwezo wa kuandika na kuimba nyimbo zake mwenyewe.
Msanii huyo kutoka pande za Mwanza ambaye hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yenye jina la ‘Acha waone’ alifunguka hayo baada ya kuulizwa na safu hii anadhani ni kitu gani kinachowafanya washindi wa BSS washindwe ‘kushaini’ katika game ya muziki.
“Binafsi nadhani umefikia wakati sasa kwa waandaaji na wapiga kura kuangalia nani mwenye uwezo wa kutunga na kuimba, siyo mwenye uwezo wa kuimba nyimbo za watu wengine kama ilivyokuwa kwenye mashindano yaliyopita kitu ambacho kimewafelisha washindi kwakuwa wanashindwa kuandika nyimbo zao,” alisema Beatrice, ambaye kifamilia ni mama wa watoto 3.
************************Chiller ampa shavu Small Jobiso

Mkali wa Bongo Fleva, Aboubakar Shaban Katwila a.k.a Q Chief amempa shavu prodyuza anayekuja juu katika game hiyo, Small Jobiso ambaye kabla ya kuingia huko alikuwa ni dansa maarufu aliyeonesha kipaji chake tangu utotoni.
“Namkubali sana dogo, ye ndiyo kafanya ngoma yangu Saba mara sabini ambayo watu wameipokea vizuri, nalazimika kumpa tano kwasababu ni mkali, naamini siku zijazo atakuwa mkali zaidi,” alisema Chiller.

**********************************
Ray C Amfagilia Mwisho BBA All Stars
Mwanadada Rehema Chalamila a.k.a Ray C leo anatokea tena hapa ShowBiz akiwa na ishu mpya inayomuhusu yeye na ‘X Boyfriend’ wake, Mr. Morogoro a.k.a Mwisho Mwampamba ambaye bado anaendelea kula bata ndani ya mjengo wa Big Brother All Stars huko Sauzi.
Kama bado hujainyaka ishu yenyewe ni kwamba, mwanadada Ray C amefunguka na kumfagilia Mwisho huku akimtakia ushindi mwema katika shindano hilo la BBA kwani bahati kama hiyo huwa haiji mara mbili.
Akipiga stori na Dj Fetty kupitia kipindi cha Bongo Fleva kilichorushwa na kituo cha redio Clouds FM mwishoni mwa wiki iliyopita, Ray C alisema kwamba hakujisikia vibaya Mwisho alipomtaja kama girfriend wake wa zamani kwakuwa anazidi kumtangaza.
“Kwangu iko poa, yeye kunitaja BBA kwakuwa anazidi kunitangaza, ukizingatia kwamba mimi na Mwisho bado tunawasiliana kama marafiki. Kikubwa namtakia ushindi, ajitahidi kwa kuitumia nafasi hiyo aliyoipata mara ya pili vizuri ili arudi Bongo na pesa hizo,” alifunguka Ray C baada ya kuulizwa na Dj Fetty anajisikiaje kutajwa na Mwisho wakati akiingia kwenye mjengo wa BBA?

*************************************
Ni zamu ya Musoma, Mwanza Kujipangusa
Ule mpango wa kujipangusa, yaani ‘Rrraaaaaaaaa’ bado unaendelea na sehemu inayofuata baada ya Tanga na Zanzibar ni Kanda ya Ziwa, Musoma na Mwanza.
Nalizungumzia Tamasha kubwa la Fiesta 2010 ambalo leo liko pande za Musoma huku timu ya wakali wa Bongo Fleva ikichukua nafasi stejini na kujiopangusa pamoja na maelfu ya mashabiki watakaojitokeza usawa huo.
Primetime Promotion ambao ni waandaaji wa mpango huo wa kujipangusa wamesema na ShowBiz kwamba upande huo ishu nzima itachukua nafasi ndani ya Musoma Hotel huku wasanii kama Temba, Chegge, Belle 9, Barnaba, Linah, Beatrice William, Amini, Fid Q na wengine kibao wakisdababisha kuhakikisha burudani yote inakwenda sawia.
“Baada ya Musoma, kesho Jumamosi itakuwa ni zamu ya Mwanza kwa shoo ambayo itaanzia ndani ya Yatch Club na kufuatiwa na Uwanja wa CCM Kirumba Jumapili, huku msanii Fid Q akiwa ndiyo mwenyeji wetu,” walisema waandaaji.

compiled by mc george/ijumaa
No comments:
Post a Comment