Tuesday, July 27, 2010

Maswali ya wasomaji na majibu


Swali: Mimi sili nyama ya mbuzi wala ya ngo’mbe, nakula nyama ya kuku na samaki tu. Je, kwa kutokula nyama hizo naweza kupata matatizo? Asante na kazi njema. Fredirick – Dar es Salaam.

Jibu: Fredy, asante kwa swali lako. Mtu hawezi kupata matatizo ya kiafya kwa kuacha kula nyama nyekundu (Mbuzi na ng’ombe) bali utapata matatizo ya kiafya kama ukipenda kula nyama hizo kwa wingi. Unachokula ndiyo hasa kinachotakiwa, hata usipokula kwa maisha yako yote huwezi kudhurika na badala yake utakuwa na afya njema. Siku zote inashauriwa tupende kula nyama nyeupe na tuziepuke nyekundu.

Swali: Nawezaje kusafisha utumbo mpana kwa kutumia maji? Pia kwa nini tumbo langu hujaa gesi kila mara? Asante. Msomaji (hakupenda kutaja jina)

JIBU: Njia bora ya kusafisha tumbo kwa njia ya maji ni Enema. Somo hili tumeshaliandika kwa kirefu katika makala zetu zilizopita. Kwa kifupi Enema ni kitendo cha kusafisa utumbo mpana kwa kuweka maji kupitia njia ya haja kubwa na kutoa uchafu wote kwa njia hiyo hiyo. Kuna kifaa maalum (Enema Kit) kinachotumika katika zoezi hili.
Aidha, unaweza pia kusafisha tumbo lako kwa kunywa maji mengi kwa utaratibu maalum (Water Therapy) kama tulivoeleza kwa kirefu katika makala mbili mfululizo katika matoleo yaliyopita.
Kuhusu tumbo lako kujaa gesi, nahisi hali hiyo inachangiwa na tumbo kuwa chafu, hivyo kwa kusafisha tumbo lako bila shaka na tatizo hilo linaweza kutoweka pia, vinginevyo nakushauri nenda hospitali kwa ajili ya kupata vipimo na kujua chanzo cha tatizo na kupewa tiba inayostahili.

Swali: Halo habari? Mimi ni mnene na nina tumbo kubwa, natamani sana nipungue, je nifanyeje? Na mwingine anauliza: Mimi nimetoka kujifungua miezi minne iliyopita nikiwa na kilo 68, lakini hivi sasa nimeongezeka na kuwa na kilo 78 na wala sili sana. je nifanyaje ili nipungue uzito?
Asante Naitwa Sarah

JIBU: Kupunguza mwili hakuna njia ya mkato, ni lazima uzijue na uzingatie kanuni zake. Kanuni ya kupunguza mwili ni kuingiza chakula kidogo na kutoa kingi. Hii ina maana ya kula kiasi na kufanya sana mazoezi ama kazi nyingi, ulaji wako usilingane na shughuli unazozifanya. Huwezi kupunguza uzito kwa kutokula peke yake, bali na kwa kujishughulisha sana au kufanya mazoezi.
Unachotakiwa kufanya kula kidogo au kuacha kula vyakula vizito na badala yake ule vyakula vyepesi kama matunda, mboga za majani, n.k, huku ukifanya sana kazi au mazoezi kwa muda mrefu, kwa kufanya hivyo bila shaka uzito utapungua. Kama hauli sana na mazoezi hufanyi, huwezi kupungua.
Kuhusu kupunguza tumbo, unahitaji kufanya mazoezi maalum ya kuondoa tumbo, nakushauri nenda ‘gym’ utaelekezwa namna ya kufanya mazoezi ya kuondoa tumbo.

Swali: Ninaishi na virusi vya ukimwi na CD4 zangu zimeshuka sana. Nile nini ili CD4 zangu zipande?
Asante, Alex

Jibu: Alex, pole kwa kuumwa, lakini unaweza kuishi kwa muda mrefu kama utazingatia kanuni za ulaji sahihi ambazo tumezieleza sana katika makala yaliyopita. Unachotakiwa kula kwa sasa ni matunda na mboga kwa wingi kila siku. Robo 3 ya mlo wako unaokula kila siku uwe ni wa matunda na mboga mchangayiko. Kula vyakula vya asili vyote unavyoweza kula, kama vile mihogo, viazi, mahindi, karanga, maboga, magimbi, asali, n.k.
Ulaji wa vyakula hivyo kwa wingi kila siku, siyo tu unaweza kupandisha CD4 zako, bali vitakulinda na magonjwa mengine hatari zaidi. Kumbuka kuwa, mtu ambaye hazingatii kanuni za ulaji sahihi, huwa na kinga dhaifu na CD4 chache, hata kama hana virusi vya HIV.

4 comments:

pam said...

Mrisho naomba nimjibu huyo wa cd4 kwa kuwa nina mfano hai wa mtu mwenye virusi nyumbani...zaidi ya yote apendelee sana kula kitunguu kisichosafishwa...yaani kitunguu maji kilichomenywa tu bila kukisuuza ...maana wengi wetu kwenye kachumbari tukiweka kitunguu huwa twakiosha kwa maji au chumvi kwanza sasa kwenye kupandisha cd4 jitahidi unakula kitunguu karibu kila mlo kama huwezi kula hivihivi kata kachumbari ya kitungua fresh kilichomenywa muda huo bila kukisafisha then utaniambia

Mrisho's Photography said...

Pam...asante sana kwa kuongezea...naamini kuna vyakula vingi tena simpo vinavyoweza kumlinda mwenye HIV na akaishi bila kusumbuliwa na maradhi...kitunguu saumu nacho ni sawa na anti biotic..ni kingi ya maradhi mengi.....kama una uwezo wa kumudu vyakula na una hiv huna haja ya kuhofia iwapo tu utazingatia ulaji vyakula vya asili..hapo ni kila kitu...

Disminder orig baby said...

Kitunguu Saumu ni mwisho wa mambo, pendelea kula tende japo kukwa tatu asubuhi mchana na jioni pia. Tende ni kinga kubwa ndani ya mwili.

pam said...

Asante na karibu tena