Mwimbaji na Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, akiserebuka na dada yake, Khadija Yusuf, wakati wa uzinduzi wa albamu ya My Valentine ya kikundi hicho, uzinduzi ambao ulijaza mashabiki kibao katika ukumbi wa PTA ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere mwishoni mwa wiki iliyopita. Mzee na Dadake waliimba wimbo wao wa Udugu Hazina Yetu lakini wakashindwa kuumaliza baada ya kuangua kilio jukwaani..!! Khadija amerejea kundini hivi karibuni baada ya kuhama kundi hilo.
“Sugu Nenda Bungeni Mbilinyi Okoa Mbeya”Mastaa wa Hip Hop wamuimbia Sugu
Wanaharakati wanaomsha hisia za mapinduzi kwenye soko la Bongo Fleva, wameamua kuacha shughuli zao na kuanza kumpigia debe Legend wa Bong Hip Hop, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Muasisi wa mradi wa Anti Virus, Fred Maliki ‘Kinega Mkoloni’ katika straight talk to Abby Cool & MC George over the weekend juzi (Jumamosi), alisema kuwa kila kitu kinakwenda vizuri na fujo zitaongezeka baada ya Sugu kushinda kura za maoni.
“Leo (juzi) ndiyo kura za maoni CHADEMA zinapigwa Mbeya Mjini. Hatuna shaka kwamba mheshimiwa Sugu atashinda na kukiwakilisha chama chetu kugombea jimbo hilo. Baada ya ushindi huo fujo zitaanza rasmi,” alisema Mkiloni.
Alisema kuwa yeye, Danny Msimamo na mastaa wengine wataingia studio rasmi baada ya matokeo ya kura za maoni ili kumfanya Sugu ajisikie yupo kwenye mapambano, huku nyuma yake wapo wana harakati wengi. “Tutatoka na wimbo unaitwa Sugu Nenda Bungeni. Mbali na sisi, pia nawasimamia wasanii wa Isanga Family ambao wao tayari wana wimbo wao, Mbilinyi Okoa Mbeya,” alisema Mkoloni. ****************************
Trina:Aidondokea dhambi ya ngono kwa fujo, usagaji kwa sana!
Maombi ya wasomaji wengi wa safu hii yanatufanya tumuweke mdada hardcore pande za Obama. Ni Trina na anafunuliwa kuhusu mambo yake ya kimapenzi.
Ebwana Dah! Kwa mujibu wa site ya kiwanja ambayo imejipa jukumu la kufunua uhusiano wa kimapenzi wa mastaa mbalimbali, Trina siyo tu kwamba ameweka rekodi ya kufanya mapenzi na wanaume kadhaa, bali pia ametengeneza namba ya wanawake aliotenda nao usagaji.
C-Murder ndiye mwanaume anayetajwa wa kwanza kudondoka in bed na mgumu Trina kabla ya Jamie Foxx kuunga. Hata hivyo, kwa wote hao wawili, haitajwi ni lini alishirikiana nao kuibanjua amri ya sita. Bilionea Sean Cutter ‘ Jay-Z’ au ukipenda muite Baba Beyonce, naye yumo kwenye orodha ya Trina ambapo mwanadada huyo alipopeana naye ‘shiti’, hakuona hatari kusagana na staa wa R&B, Kelly Rowland ambaye ni memba wa kundi marehemu la Destiny’s Child.
Baada ya Kelly, Trina alinogewa na mchezo wa usagaji, kwahiyo alipoondoka hapo, akaanza kupeana penzi la kisela na mwana Hip Hop wa kike mwenye sifa za kibabe, Missy Elliot. Mark Wahlberg alimtumia Trina mwaka 2000 na Cash Money Brother, Lil Wayne alipumzika kwa mdada huyo kuanzia mwaka 2005 lakini ilipofika mwaka 2006, kila mtu alianza kivyake.
Rasi Baker aligusa mwaka 2007 na mwaka huo huo, Kenyon Martin alichangamsha naye damu. Jina lake kamili ni Katrina Le`verne Taylor, umri wake ni miaka 31. Alizaliwa Desemba 3, 1978, Miami, Florida, Marekani. Dini yake ni Mkristo. ****************************
Maimartha, Papic wa Yanga ngoma drooSuper Character wa Mai & Ben Show ya TBC1, Mimartha Moshi Jesse ‘Oprah wa Bongo’ amesema kuwa watu wanachonga sana anapoonekana kwenye shughuli tofauti akiwa ametinga kiwalo cha aina moja, na kufafanua kwamba wanaopakaza hawajui kama hiyo ni Papic style.
Mai alisema kuwa yeye anazo nguo nne ambazo zinafanana ambazo huzitumia kama sare ya ‘u-MC’ kwenye shughuli mbalimbali, kama ilivyo kwa Kocha wa Yanga, Kostadim Papic ‘Clinton’ ambaye naye ana kawaida ya kuvaa nguo za aina moja anapokuwa kazini.
“Mimi siwezi kuwa kauka nikuvae hata siku moja. Nina viwalo vingi. Watu wakiona nimevaa mfululizo, wajue zipo za kumwaga, kila siku nabadili ila hawajui kwa sababu wanaona kitu kinafanana kuanzia rangi mpaka mshono na mvaaji ni yule yule,” alisema Mai ambaye hujulikana pia kama namba 1,2 na 3. Imeandikwa na Shakoor Jongo
**********************
Kutoka BBA:Munya ampeleka puta Paloma, Mwisho ni full mapozi
Washiriki wa shindano la Big Brother Afrika All Stars, Paloma na Munya, Ijumaa iliyopita waliamua kuingia kwenye mpambano usio rasmi wa kupima ubavu na mshindi kumtupia mwenzake kwenye bwawa la kuogelea.
Katika tukio hilo ambalo Abby Cool & MC Georger over the weekend ililirekodi kwa macho yake kideoni, Munya alithibitisha kuwa mwanaume atabaki kuheshimiwa kwa kipimo chake kwa sababu kila mara Parloma licha ya kutumia nguvu nyingi, alijikuta akitupiwa bwawani.
Paloma, alionekana amekusudia kumtoa nishai Munya kwa kupambana naye akitumia nguvu, lakini kila mara, alijikuta akishindwa kufurukuta mbele ya mikono ya mtoto wa kiume, hivyo mpaka mwisho akawa amelowa chapachapa. Wakati pambano hilo likiendelea, Tatiana Durao wa Angola, yeye alikuwa akishangilia na kumhimiza Paloma ili aweze kumshinda Munya, ingawa haikuwezekana.
Baadaye, Tatiana naye alitakiwa kwenda kukabiliana na Munya ili Paloma apumzike lakini aligoma katakata, hivyo kukimbilia ndani. Wakati yote yakiendelea, mshiriki wa Tanzania, Mwisho Mwampamba ‘Mr. Morogoro’ alikuwa mpole, akiongea kwa mapozi kwenye jakuzi.
Kwa upande mwingine, Meryl wa Namibia, aliendelea kuwapa mateso ya mitima midume iliyomo mjengoni, kutokana na hulka yake ya kuzurura bila nguo. Hata hivyo, ni wazi kuwa kwa Meryl, mshipa wa noma haupo, kwani amewahi kuonywa kuhusu hilo lakini amebaki na tabia yake.
*********************
Lady jaydee: Mimi Teja, nimekufa kwa GardnerQueen of Afropop ukanda wa Afrika Mashariki, Judith Mbibo Wambura Habash ‘Lady Jaydee’ anatoa picha kwamba watu wamuache anapoimba yeye ni Teja kwa sababu penzi lake kwa mume wake, Gardner G Habash halipimiki.
Akihojiwa kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kwenye Televisheni ya TBC1, Jaydee ambaye ana majina lukuki kama Jide, Mama Somefood, Komando, Binti Machozi, Binti Kujishtukia na mengineyo, alisema kuwa yeye kwa Gardner ni Teja.
Kauli hiyo ya Komando Jide, imetosha kutoa tafsiri kuwa Gardner ndiye chanzo cha kuandika wimbo huo ambao unachukua umaarufu kwa sasa. Mtangazaji Enock Bwigane katika kukoleza mahojiano hayo, alisema kuwa yeye ni teja kwa mke wake na Jide akajibu: “Na mimi na teja kwa Gardner.”
compiled by mc george/ijumaa
1 comment:
JAMANI SIO PALOMA NA MUNYA NDIO WALISUKUMANA BALI WALIKUWA PALOMA NA HINNINGTON YULE MSHIRIKI WA UGANDA, LOH EBU TUWEKEE HABARI ZA UHAKIKA SIO UNAKURUPUKA TU
Post a Comment