Monday, August 23, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Zuhura Kumnasa ukaloge kwanza!
Sistaduu anayefanya vyema kwenye game ya muziki wa Kizazi Kipya, Zuhura Mrisho anadaiwa kuwa mgumu kinoma kung’oleka kimapenzi na maneno ya kitaa yanasema kwamba, ili umpate basi lazima upitie kwa sangoma kuweka mambo sawa kwanza.

Akipiga stori na safu hii, Zuhura ambaye pia aliwahi kuiwakilisha Bongo kupitia Shindano la kumtafuta Kisura wa Afrika, Nokia Face Of Afrika 2006, alisema:

“Najaribu kuyaweka maisha yangu mbele kwanza, mambo mengine baadaye, sipendi mambo ya mapenzi, kwa sababu najua hayana future, napambana na life kwanza.”

Hata alipobanwa aeleze kwasasa yupo katika uhusiano na nani alitilia ngumu, akieleza kwamba hayo ni maisha yake binafsi na hapendi kuingiliwa ingawa msimamo wake ulibaki kuwa hana time kabisa na wanaume.

Pamoja na stori hiyo, hivi sasa Zuhura anasikika na mzigo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Napagawa’ songi ambalo ndani yake lina mashairi ya kimapenzi, akiwa amepiga kolabo na Kindago wa TMK Majita.
**********
H. baba: Muvi ya Promota itaniweka pazuri
Mkali wa miondoko ya TAKEU nchini, Hamisi Ramadhani a.k.a H Baba amesema filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Promota itamuweka pazuri, maana mambo aliyoyafanya ndani yake yanatisha.

H Baba aliiambia safu hii juzi jijini Dar es Salaam kuwa, uwezo aliouonesha akishirikiana na wakali wengine kama Yusuf Mlela kwenye sinema hiyo ndiyo unaompa ‘kiburi’ kwamba lazima afunike.

“Sitaki kuongea sana, watu wavute subira kidogo watakutana nayo kitaani. Ni mzigo wa ukweli utakaozidi kuniweka kileleni. Siyo filamu ya kukosa,” alitamba H Baba ambaye kibao chake cha Mpenzi Bubu kilifanya maajabu kwenye anga la muziki.
**********
Diamond Apata ajali, avamiwa na vibaka!
Bwa’mdogo anayesumbua ndani ya game ya muziki wa Bongo Fleva, Abdul Nasib ‘Diamond’ wiki iliyopita haikuwa nzuri kwake baada ya kupata ajali ya gari na kuvamiwa na vibaka ambao walipora baadhi ya vitu vyake vya thamani, Shakoor Jongo anashuka katika para zinazofuata.

Ishu ilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, mishale ya saa saba za usiku, pande za Kigogo, Dar ambapo Diamond alikuwa akitokea Magomeni akielekea Ilala, lakini alipofika eneo hilo, gari lake likagongwa na gari lingine. Diamond alipopatikana kwa njia ya simu, alisema:

“Ni kweli gari langu liligongwa na kugeuka lilipotokea, lakini dereva wa gari lililonigonga, alikimbia. Cha kushangaza vibaka wakanivamia na kuanza kunipora baadhi ya vitu vyangu. “Purukushani ilikuwa kubwa, lakini bahati nzuri muda mfupi baadaye alitokea baunsa John Cena akanisaidia”.

*****************
Jesica, demu wa Kala
Kala Arudi Bongo bila demu wa Kiganda
Mkali wa Hip Hop Bongo, Kala Jeremiah, ambaye ali-spend miezi kadhaa jijini Kampala Uganda akiwa na mchuchu aitwaye Jesica, amerejea nchini kimya kimya akiwa mikono mitupu, tofauti na matarajio ya wengi kuwa angekuja na mamsapu wake huyo.

Akiteta na Abby Cool & MC George Over the Week-end juzi, sosi wetu alisema: “Jamaa karejea, lakini yupo peke yake, wengi tuliamini angekuja na demu wake, lakini ndiyo hivyo, msela kashuka mwenyewe.” Kala alipopigiwa simu ili kufafanua, alikuwa na haya ya kusema:

“Yeah! Ni kweli sijaja na Jesca, lakini hiyo haimanaanishi kwamba tumeachana. She is still my love, nimeshindwa kuja naye kwa sababu uhusiano wetu haujawa plain kwa wazee wake, na mimi kama muungwana, sikuona busara kutoroka naye, ila kwa taarifa yako, ndoto yetu ni ndoa.”
*********************************

Justin Bieber Kana miaka 16, kameshajiachia na mademu wawili!
E bwana dah! Kama kawa ipo kitaani na leo imenasa orodha ya mademu waliowahi kulala kitanda kimoja na dogo anayetesa katika muziki wa R&B pande za Marekani,Justin Bieber.

Kinda huyo raia wa Canada, akiwa ndiyo kwanza anagonga miaka 16 ya kuishi dunia tangu alipozaliwa mwaka 1994, tayari ameshakula bata na Caitlin Beadles kuanzia mwaka 2007-2008 kabla ya kufunga pazia na Kristen Rodeheaver mwaka 2009 huku maelezo yakisema kwamba, bado wapo pamoja.

Wengi wa mashabiki wake waliotoa comments zao, walisema kwamba, dogo ni cheche sana na kama kwa umri huo tayari ameshamiliki vimwana wawili, basi akifikisha miaka ishirini huenda idadi ikawa kubwa zaidi.
*********************

compiled by mc george/wikienda

No comments: