Saturday, November 13, 2010

MBIO ZA VODACOM MWANZA CYCLE CHALLENGE ZAFIKIA TAMATI‏

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro, akiinua bendera kama ishara ya uzinduzi rasmi kwa mbio za Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa wanaume na wanawake.


Pichani juu ni washiriki wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge Kilometa 196 kwa wanaume wakichuana vikali katika mbio hizo zilizofanyika jijini Mwanza.
Mshindi wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa upande wa wanaume Hamiss Clement(shinyanga) akimalizia mbio hizo na kuibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia Masaa 5:19:43,kwa kilometa 196.
Mshindi wa mashindano ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge kwa upande wa wanawake Sophia Hadson(Arusha)akimalizia mbio hizo na kuibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia Saa 2:32:14 kwa kilometa 80.

Mwandishi Wetu, Mwanza
HAMISI Clement wa Shinyanga leo ( jana) alinyakua taji la’ Vodacom Mwanza Cycle Challenge’ lililokuwa likishikiliwa na Mussa Milao wa Arusha na kuzawadiwa sh mil 1.5 na waandaaji wa mashindano hayo baada ya kutumia saa 5:19.43.
Clement katika mashindano hayo alishiriki mbio za umbali wa Kilomita 196, abazo zilianzia Nata hadi Nyashimo ambako alitumia baiskeli ambayo si ya mashindano ambako liwaacha mbali wenzake wengi waliokuwa na baiskeli za mashindano.

Mshindi wa pili wa mashindano hayo kwa wanaume ni Richard Laizer aliyetumia saa 5:20.12 ambaye alizwadiwa sh mil 1 huku wa tatu Said Konda wa Shinyanga abaye alitumia saa 5:20.30 ambaye alizawadiwa sh 700,000.

Kwa upande wa Wanawake Sophia Adison wa Arusha naye alinyakua taji la mashindano hayo baada ya kushika nafasi ya kwanza ya mashindano hayo baada yakutumia saa 2:32.14 na kuzwadiwa sh mil 1.1, taji ambao lililuwa likishikiliwa na Beatrice Kennedy wa Dodoma ambaye mwaka huu amenyakua nafasi ya tano ya mashindano hayo.

Mshindi wa pili kwa wanawake ni Martha Anthony wa Mwanza ambaye alitumia saa 2:34.27 ambaye alizawadiwa sh 800,000 huku wa tatu alikuwa ni Ndyashimbi Kurya wa Mwanza alinyakua nafasi ya tatu baada ya kutumia saa 2:36.34.

Adison katika mashindano hayo alishiriki mbio za umbali wa Kilomita 80, kutokea Nata hadi Nyanguge ambako uzoefu ulimsaidia kunyakua taji hilo.

Akizungumza baada ya mashindano hayo, Clement alisema kilichomsadia ni mazoezi ya mara kwa mara aliyokuwa akiyafanya ingawa milima ilimsumbua katika mashindano hayo.

Clement alisema kwa ushindi huo atawashauri wenzake wa Shinyanga kununua baiskeli za mashindano kwa sababu, baiskeli za kawaida zinasumbua, fedha alizozipata atatumia kununulia baiskeli za mashindano.

Naye Adison alisema mashindano ya mwaka kwake yalikuwa na upinzani mkali kwa sababu ushindani ulikuwa ni wa hali ya juu hasa wenye baiskeli za Phoenix ambao walikuwa hawampi nafasi.

Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Steven Kingu alipongeza ushindi wa Clement kwa sababu mara nyingi ushindi huenda mikoa mingine ambako pia alitoa wito kwa washiriki wa mikoa ya Kanda ya ziwa kuwa na baiskeli za kisasa na za mashindano ili wafanye vizuri zaidi katika mashindano ya Kimataifa.

Kingu alisema mara zote Vodacom kila mwaka wanatoa zawadi zaidi ya mwaka uliopita ili kuleta chachu ya washiriki kujiandaa vilivyo kwa mashindano yajayo na kutoa wito kwa mashindano ya mwakani.

Mgeni rasmi katika mashinano hayo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Kanali Mstaafu Serenge Mrengo.

Mashindano hayo yalishirikisha washiriki 403 kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam, Dodoma, Mara na Kagera.

Wednesday, November 10, 2010

DIAMOND APIGA DEI WAKA UK!

Diamond akionesha msosi aliokwisha utengeneza..
..kafanya kila kitu mpaka mambo ya kubeba taka....
... akiwa kweye maandalizi
...finyango li tayari kwa kuliwa...kama mbagala vile!
Wadau wa Urban Pulse kutoka kushoto ni Linda, Hunga, Diamondo Na Maboxi wa Vincent Alan na Gardol
Msanii wa kizazi kipya Diamond a.k.a Mzee wa Mbagala, ambaye yuko nchini Uingereza kwa ziara ya kimuziki, mapema wiki hii alijitolea kupiga 'dei waka' kwenye mgahawa wa Vincent (Vincent Restaurant) iliyopo Reading (mji wa kusoma) nchini humo kwa ajili ya kusaidia kuchangia na kupromote Urban Tour ambayo inachangisha fedha kwa ajili ya kampeni za kugiga vita ugonjwa wa Malaria. Ijumaa hii, msanii huyo,nne usiku, kiingilio ni £10.00 kabla ya saa sita usiku. kazi kwenu wa Bongo wa UK.

Mzee wa mbagala Ndani ya Congo National TV


URBAN PULSE inapenda kuwaletea a sneak preview ya tv interview ya Diamond ndani ya Congo national TV akihojiana na mtayarishaji/ presenter Oliver Katoto wa Congo National TV kwa ajili ya kupromote URBAN TOUR dhidi ya malaria. Stay tune ili kuona full length interview.

SONY YALETA TV ZA 3D

Kampuni ya Kimataifa ya Sony, imezindua aina mpya ya televisheni yenye teknoljia ya kisasa duniani ya 3D. PICHANI ni Mkurugenzi Mkuu wa Sony Osamu Miura (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mauzo Afrika Mashariki Dinakaran Munaswamy (wa pili kulia) wakizindua TV ya Sony 3D jijini Nairobi, kenya leo.

Tuesday, November 9, 2010

Diamond akutana na Chris Gold Finger UK


Baada ya makamuzi ya kufa mtu kule Milton Keynes wikiendi iliyopita, kituo kinachofuata ni The Club Croydon, jijini London Ijumaa Nov 12 ambapo mkali kutoka Bongo, Diamond pamoja na Mish 'The Fyah Sister', watafanya kweli wakiongozwa na Legendary Dancehall Master, DJ Chris 'Gold Finger'. Mpango mzima ni kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa malaria unaoua watu wengi barani Afrika, ikiwemo Tanzania.

URBAN PULSE CREATIVE MEDIA

ZIZZOU YAIPA TAFU COASTAL UNION

Mkurugenzi wa Zizzou Fashions na ambaye aliwahi kuwa Nahodha wa Timu ya Mpira ya Coastal Union ya jijini Tanga, Tippo Athuman (kulia), akimkabidhi jezi na mipira Kiongozi wa Coastal Union, Bw. Steven Mgoto ikiwa ni sehemu ya vifaa vya michezo kama vile jezi, Soksi, mipira na beebs, vilivyotolewa kwa timu hiyo. Mababidhiano hayo yamefanyika katika duka la Zizzou Fashions, tawi la Victoria, jijini Dar es salaam leo.

Monday, November 8, 2010

KANUMBA, RAY WAJA NA MOJA KALI!

Ni muda mrefu umepita kila mmoja akiwa busy na kutengeneza sinema yake. Katika hilo, Ray alifungua njia kwa kuanzisha RJ Production kama kampuni inayotengeneza filamu zake. Kampuni yake imeonesha kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, hasa katika filamu ambazo amemshirikisha mwana dada machachari, Irene Uwoya ambaye kumbukumbu zake zingali fresh kwenye hisia za mashabiki wa filamu za Bongo pale alipocheza filamu ya Oprah na kuwachanganya Ray na Kanumba vilivyo. Kwa upande wake Kanumba, naye amekuwa busy na kampuni yake Kanumba The Great Films ambako ameonesha mafanikio katika filamu zake za Uncle JJ.

Safari hii wanakuja kwa pamoja na Off Side - Hidden Truth. Mimi na wewe bado hatujui kilichomo humo, lakini kama ulishaona Oprah, filamu iliyozua mjadala mkubwa wa kimaadili, bila shaka unategemea makubwa zaidi katika hii, hasa vinapokutana vichwa viwili...Ray, Kanumba na kati mamaa Ndikumana, Irine!

BASATA KUANDAA KONGAMANO KUBWA LA MUZIKI NCHINI

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego akifafanua masuala mbalimbali yaliyoibuka kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii.Katikati ni Mtangazaji wa ITV/Radio One,Maulid Kambau na Hassan Bumbuli Katibu wa CAJAtz.
Maulid Kambau kutoka ITV/Radio One ambaye aliwasilisha mada Kuhusu Mchango wa Maprodyuza Katika Kukuza Utambulisho na Soko la Muziki Tanzania akijibu moja ya maswali yaliyoelekezwa kwake kutoka kwa wadau wa Jukwaa la Sanaa.
Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakisikiliza kwa makini masuala mbalimbalil yaliyoibuka kwenye Jukwaa.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) liko kwenye mikakati ya kuandaa kongamano kubwa la muziki linalotazamiwa kufanyika katika siku za hivi karibuni ili kujadili mwenendo mzima wa fani hii ikiwa ni pamoja na kujenga utambulisho wa muziki wa Tanzania .

Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego aliweka wazi hilo wakati akifafanua masuala mbalimbali yaliyojitokeza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa BASATA ambapo alisema kwamba,kongamano hilo pamoja na mambo mengine litakuja na majibu kadhaa ya changamoto mbalimbali zinazoikabili fani ya muziki nchini sambamba na kujenga heshima ya wasanii wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

“Tunakusudia kufanya kongamano kubwa ambalo litahusisha maproducer, wadau wa vyombo vya habari, mapromota, wasanii wote wa muziki na wadau mbalimbali wa sekta ya sanaa ili sasa kwa pamoja tujiulize ni muziki gani tunaoutaka, fani yenyewe iendeje na ni kwa vipi tutajenga utambulisho wa muziki wetu na hivyo kuuzika kimataifa” alisisitiza Materego.

Aliongeza kwamba, muda umefika sasa kwa wasanii wa muziki na wadau wote kukaa chini na kukuna vichwa juu ya muenendo mzima wa fani hii kwani kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikiibuka na kuzua wasiwasi wa fani hii kudidimia na kukosa muelekeo kama jitihada za makusudi hazitafanyika.

Alihoji tabia inayokua kwa kasi ya baadhi ya wasanii wa kitanzania kunakiri vionjo (beats) vya miziki kutoka nje hasa Marekani na kuonesha wasiwasi wa wasanii wetu kuja kuburuzwa mahakamani na hata kutozwa faini kubwa za fedha kutokana na kitendo hicho kukiuka sheria za kimataifa za hakimiliki na hakishirikishi.


“Mimi najiuliza sana hivi siku wasanii wa Marekani wakija Tanzania na kuwaburuza wasanii wetu mahakamani kwa kosa la kunakiri kazi zao bila ruhusa nani atapona kiama hiki?Nasema hivi kwani hili haliko mbali kutokana na ukweli kwamba, tunaingiliana nao sasa.Ni lazima haya tuyaangalie mapema ndiyo maana BASATA inaona ni muda muafaka sasa wa kuwa na kongamano hili la wanamuziki wote” alimalizia Materego.

Mada ya wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa iliwasilishwa na Mtangazaji wa ITV/Radio One,Maulid Kambau na ilihusu Mchango wa Maprodyuza wa Muziki Katika Kukuza Utambulisho na Soko la Muziki Tanzania ambapo alilenga kuwakumbusha wasanii na waandaaji wa muziki kujikita kwenye muziki wenye vionjo vya kitanzania na kuacha kabisa tabia inayoota mizizi ya kunakiri kazi za watu wengine.

Picha/Habari na Afisa Habari wa BASATA,Alistide Kwizela

FILM CENTRAL!

DIAMOND AFANYA KWELI UK

Msanii anayekuja juu Bongo, anayejulikana kwa jina la Diamond, yuko nchini Uingereza kwa ziara ya kimuziki ambapo usiku wa kuamkia jana alikuwa akifanya shoo iliyotakata katika mji wa Milton Keynes ambako alikonga nyoyo za mashabiki wa kibongo waishio mjini humo. Ziara hiyo, ambayo ni maalum kwa kuchangisha fedha za kampeni ya vita dhidi ya malaria, inaratibiwa na Urban Pulse Creative na wikiendi ijayo Nov 12, Diamond atakamua tena Croydon, London akifanya vitu vyake.
...mashabiki wakiyarudi mangoma ya Diamond 'mtoto wa Mbagala'
...uhondo unapokolea...
..kundi la muziki la Red City wakila pozi na mmoja wa waandaji, Frank (kulia) kabla ya kufanya makamuzi jukwaani kumsindikiza Diamond
....Diamond akiwa akiwa 'mtu kati' na totoz!

Raise The Roof!

Sunday, November 7, 2010