Mgeni rasmi wa hafla hiyo,Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba pichani kati,shoto kwake ni Mkurugenzi wa huduma za uuguzi hospitali ya Taifa Muhimbili na mwisho kabisa ni Mwendesha kipindi cha Njia Panda,Dr Isaac Maro wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine wa kipindi hicho kinachorushwa na Clouds FM kila siku ya jumapili..
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akimlisha keki mtoto anayelelewa na kipindi cha Njia Panda,dada Juliana Maganyiro,ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 19,ambapo yeye na wadau wengine wa Njia Panda waliamua kufanya hafla fupi sambamba na kutoa msaada katika wodi ya watoto wenye matatizo ya saratani.
Leo hii kipindi cha Njia Panda kimefanya hafla fupi ya mwaka mpya katika wodi ya watoto wenye matatizo ya saratani,wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili,hafla hiyo iliambatana na sherehe fupi ya siku ya kuzaliwa ya mtoto Juliana Maganyiro ambaye amekuwa akilelewa na kipindi cha Njia Panda tangu alivyokuwa na umri wa miaka 13,Juliana ni mtoto Yatima na amekuwa chini ya Kipindi cha Njia Panda kwa miaka 6 sasa,aidha katika hafla hiyo iliyofanyika leo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba.Pichani mbele kulia ni Dada Juliana na nyuma kabisa ni mwendeshaji wa kipindi cha Njia Panda,Dr Isaac Maro akiwa na Mwanaharakati mwingine wa kipindi hicho Bw.Edmond Lyatuu.
Waziri wa Maendelea ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akiwaaga walezi/wazazi wanaowauguza watoto wao wenye matatizo ya saratani,ambapo pia Mh Simba mbali na misaada iliyotolewa na kipindi cha Njia Panda,alijitolea kiasi cha fedha shilingi laki tatu kwa ajili ya kula sikukuu ya mwaka mpya kwa watoto hao.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akizungumza na Mama anayemuuguza mtoto wake mwenye matatizo ya saratani na kumpa pole,Pichani kati ni mtoto anayelelewa na kipindi cha Njia panda aitwaye Juliana Maganyiro ambaye ni mtoto yatima aliyeamua kula keki yake ya sherehe ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 19 tangu kuzaliwa kwake na watoto walioko kwenye wodi hiyo.
Watoto walioko kwenye wodi ya watoto wenye matatizo ya saratani wakifurahia msaada wa vitu mbalimbali uliotolewa kwa ajili yao.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo,Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akimkabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kipindi cha Njia Panda,kwa niaba ya Mganga Mkuu,Mkurugenzi wa huduma za uuguzi hospitali ya Taifa Muhimbili,Dada Agnes Mtawa,pichani kulia ni Meneja huduma na bidhaa kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom,Bw.Elihuruma Ngowi,ambayo ni mdhamini mkuu wa kipindi cha Njia Panda.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo,Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akimkabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kipindi cha Njia Panda,kwa niaba ya Mganga Mkuu,Mkurugenzi wa huduma za uuguzi hospitali ya Taifa Muhimbili,Dada Agnes Mtawa.
Waziri wa Maendelea ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akizungumza na baadhi ya wazazi wanaowauguza watoto wao kwenye Wodi ya Watoto wenye matatizo ya saratani wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili,kabla ya kutoa msaada kwenye wodi hiyo iliyotolewa na Wadau mbalimbali wa kipindi cha Njia Panda kinachoongozwa na Dr Isaac Maro kupitia redio ya Clouds FM kila siku ya jumapili,pichani nyuma ni baadhi ya Wadau wa kipindi cha Njia Panda ambao walifika kwenye Wodi hiyo sambamba na kuwapa pole watoto wanaosumbuliwa na saratani,hafla hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar.
No comments:
Post a Comment