Taarifa kwa vyombo vya habari
APRILI 9, 2012
Msanii wa filamu,
aliyebeba mapenzi makubwa ya Watanzania, Waafrika na dunia kwa jumla, Steven
Charles Kanumba aliyefikwa na mauti ghafla Aprili 7, 2012, atazikwa kesho
Makaburi ya Kinondoni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Mazishi ya Kanumba,
yamepangwa na kuratibiwa kwa kuzingatia heshima, umaarufu, mapenzi yake kwa
watu na hadhi ya kimataifa aliyonayo, hivyo imetolewa fursa ya wengi kumuaga
msanii huyo ambaye ni mwanamapinduzi wa tasnia ya filamu ukanda wote wa Afrika
Mashariki na Kati.
Mpangilio wa ratiba na
nafasi itatolewa kwa kila mtu mwenye kuhitaji kushiriki mazishi ya Kanumba,
kufanya hivyo katika tukio la kihistoria la kumsindikiza ndugu yetu huyo kwenye
maisha ya milele. Hivyo, wito unatolewa kwa kila mtu kujitokeza kwenye shughuli
nzima.
RATIBA
Mwili wa marehemu
Steven Kanumba utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili
saa 2:30 asubuhi. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi
hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa
pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.
Wito unatolewa kwa watu
kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi, wakijipanga kando ya Barabara za
Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi ili wautolee heshima mwili wa Kanumba
wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.
Saa 3:30 asubuhi, mwili
wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi
wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed
Gharib Bilal.
Saa 4:00, itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo
itachukua dakika 60, saa 5:00 kitakuwa kipindi cha salamu kutoka kwa watu
mbalimbali.
Saa 6:00 mchana, ratiba ya kumuaga Kanumba itaanza
mpaka saa 9:00 alasiri na baada ya hapo, utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa
msafara kutoka Leaders Club mpaka Makaburi ya Kinondoni, msafara ukipita Barabara
ya Tunisia, utakatisha Barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.
Saa 10:00 alasiri, mazishi yatafanyika kwa
kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.
Kamati ya Mazishi inatoa wito kwa watu
watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu Kanumba, kuja na maua ili
kumuaga kwa heshima.
Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo
muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Sisi wote tulimpenda
kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa
mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.
K.N.Y GABRIEL MTITU
MWENYEKITI
WA KAMATI YA MAZISHI
4 comments:
Kweli watanzania wanapenda mambo ya hovyo kupita mambo muhimu! Who was Kanumba by the way? Acheni usanii hata hao viongozi na wake zao wanawafanyia usanii. Kuna mambo mengi muhimu ya kulifanyia taifa na siyo kuhudhuria misiba jamani.
That's very true., mfano kuna waheshimiwa wawili wametoa rambirambi mil 30., na mwingine 10mil. Huu ni ujinga wakati wahanga wa majanga ya mabomu na mafuriko pamoja na walimu wanahaha kupata haki zao wao wanatafuta SIFA ZA KIPUMBAVU KUGAWA HELA. HATUONI HATA HEKIMA ZAO ZAIDI NIKUTAKA SIFA. pumbavu sana
Nakuunga mkono mdau yaani hii nchi yetu kuanzi viongozi tuko nyuma, Kuna mambo mengi yakufanya tena heti wanawake kibao wakajifanya wamezimia unafiki mtupu. Mbona Mama yake hatujamuona kuzimia au dada zake au ninyi ndiyo wenye uchungu sana? Tena halipokua hai mlikuwa mnamponda eti kafa mnajifanya mnampenda wanafiki, na huyo Lulu apate azabu hili na hao wasanii wengine wapate fundisho ujinga mtupu
MAPUMBAFU tena!
Post a Comment