Na Swahili TV, Washington DC
Omar
Sykes mwanafunzi raia wa Tanzania aliyeuwawa katika jiji la
Washington, huenda akaenziwa kwa kupewa jina la mtaa ili kuweka
kumbukumbu na ujumbe kwa wote walioathirika na mauaji ya bunduki
mitaani jijini Washington, Dc, na Marekani kwa ujumla. Kama pendekezo
hilo litapitishwa atakuwa mtanzania wa kwanza kupewa mtaa nchini
Marekani.
Akiongea
katika shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Omar Sykes, meya wa jiji
la Washington, mstahiki Vicent Gray, alisema kuwa anatarajia
kupendekeza katika kikao kijacho cha halimashauri ya jiji mwezi
Septemba kubadilisha mtaa wa Fairmont St, ambako mauti yalimkuta ili
uitwe Omar Sykes Street.
Meya
Gray aliongeza kusema kuwa kitendo hicho kitakuwa ni ujumbe kwa nchi
nzima ya Marekani katika kuelezea ubaya wa ghasia za mauaji ya risasi
mitaani. Marehemu Omar aliuwawa kwa risasi akiwa katika mazingira ya
karibu na chuo kikuu anachosoma cha Howard.
Katika
shughuli hiyo ya kuuaga mwiili , Swahili TV ilifanikiwa kuona baadhi
ya viongozi maarufu waliohudhuria shughuli hiyo kama Naibu waziri wa
mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bwana Jandel
Frazier.
Akiongea
na Swahili TV, baba wa marehemu bwana Adam Sykes ambaye naye alikuwepo
katika shughuli hiyo, alisema ni heshima ya pekee kwa taifa kubwa kama
hili kumuenzi mwanae kwa kumpa jina la mtaa.
“Ni
heshima ya aina gani kwa taifa kubwa kama hili kumuenzi mwanangu
kwa kumpa mtaa”Alisema kwa majonzi huku akionesha furaha ya kupata
heshima hiyo, bwana Sykes ambaye yeye na kaka Allyas Sykes waliwasili
jumanne wiki hii nchini Marekani.
Swahili
TV iliweza kuongea na wananchi mbalimbali waliohudhuria shughuli hiyo
ambao wengi walionyesha hali ya majonzi ya kifo cha kijana huyo,
mahojiano ya Swahili TV na baadhi ya viongozi wa serikali na Uongozi
wa shule yatachapishwa na kuonyeshwa blog yetu.www.swahilitv.blogspot.com
No comments:
Post a Comment