Tuesday, August 27, 2013

WANAMICHEZO WAZURI KWA MAZOEZI, LAKINI WABAYA KWA LISHE!


Tunaendelea kuelezea umuhimu wa maji na vidonge lishe vya LIFEGAIN...ENDELEA.....
Ukinywa glasi 8 za maji kila siku kwa wiki mbili tu, utaona maumivu yameanza kupungua, ukiendelea kunywa maji kwa miezi mitatu utakuwa umepona siyo tu mgongo, miguu, nyayo, kiuno, kizunguzungu na mengineyo, bali hata ujana unarudi! Amini hili na uone maajabu.

83% ya damu ya binadamu ni maji
Usipokunywa maji unauakaribia mstari wa kupungukiwa na damu mwilini. Utakaribisha pia maradhi ya moyo kwani vyakula unavyokula bila kuviyeyusha na maji vinakuwa sumu kali mwilini na mwisho utakufa. Hapo utagundua kuwa mchezaji asiyekunywa maji ni mwepesi kumsukuma na akaanguka tu.

Kazi za maji mwilini
Maji yana kazi nyingi mwilini, hata hivyo kazi nyingi bado hazijawekwa bayana mpaka leo, lakini chache ya hizo zilizoelezwa hapo juu zinatosha kabisa kukushawishi kuwa mnywaji mzuri wa maji. Maji husafirisha virutubisho vyote tunavyokula pamoja na hewa ya oksijeni kwenda sehemu zote za mwili. Maji ndiyo yanayoirutubisha hewa ya oksijeni katika mapafu, huku yakiwa bado kama korokorokoni kulinda na kukarabati seli zote za mwili.

Ukisikia kichwa kinauma mara kwa mara basi kitu cha kwanza angalia unywaji wako wa maji! Siyo kichwa tu kinachouma, bali hata ngozi ya midomo inabanduka kwa ukavu, ni unakuwa mwoga, hujiamini n.k. Maji pia hurekebisha joto la mwili, na ndiyo maana wakati wa jua wauza maji baridi ni neema kwao na wakati wa baridi wauza kahawa nao si haba.

Kutokunywa maji kumechangia miili yetu kuzalisha magonjwa nyemelezi ya aina mbalimbali ambayo leo yamewalaza wagonjwa majumbani na mahospitalini wakiwa taabani. Hata hivyo, madawa ya mahospitalini yameshuhudiwa hivi karibuni kwa kiasi kikubwa yakitibu huku yakiwa yameambatana na lishe maalumu za wagonjwa kwa kuwa mgonjwa hafi kwa ugonjwa wake, la hasha! Kifo ni matokeo ya mgonjwa kukosa hamu ya kula na ndipo maradhi hupata urahisi wa kumuua mgonjwa kwa kuwa ana njaa.

NYONGEZA YA CHAKULA (Food Supplements)
Kutokana na mazingira tunayoishi kutofautiana, wakati mwingine mtu hukosa kupata lishe sahihi hata pesa akiwanayo na unapokuwa mgonjwa sana unakuwa huwezi tena kula. Kwa kutambua hilo, watafiti na wanasayansi waligundua mbinu mbadala inayoweza kumpatia mtu lishe kamili kwa njia nyingine kwa kutengeneza vyakula kwa vidonge au unga (food supplements) vikiwa na virutubisho vyote muhimu.

Vyakula vya aina hiyo viko vingi na vya aina mbalimbali, lakini katika makala haya nitawaeleza sifa ya chakula maalum kijulikancho kwa jina la LIFEGAIN kinachotengenezwa nchini Afrika Kusini na Kampuni ya Nativa, ambayo imejipatia umaarufu mkubwa duniani kutokana na utengenezaji wake wa vyakula asilia kwa njia ya vidonge ama unga. Pia ipo LIFEGAIN SPORT maalum kwa wana soka.

Miongoni mwa virutubisho vilivyomo kwenye chakula hiki, chenye uwezo wa kumuinua mgonjwa, ni pamoja na vitamini, protini, madini mengi pamoja na ‘Amino Acids’, kwa pamoja huupa nguvu mwili haraka, kwa mtu aliyeathirika na maradhi ya muda mrefu na huimarisha kinga ya mwili hivyo kwa mtu mzima kumuhakishia kinga imara dhidi ya magonjwa yoyote yanayoweza kujitokeza. Kwa wale watakaohitaji chakula hiki wawasiline na mwandishi kwa namba ya simu hapa chini.

Zipo sababu nyingi sana zinazozifanya timu zetu zisifanye vizuri katika mashindano mbalimbali zikiwemo hizi za kiafya. Nimeona ni vema kuwakumbusha wachezaji na wadau wote wa michezo kuwa kutojua umuhimu wa kunywa maji ya kutosha na kula lishe sahihi ni janga la kitaifa katika medani ya soka na michezo kwa ujumla.

Tafadhalini sana wadau wa michezo na hasa madaktari wa timu zetu, tuwahimize wachezaji wetu kuzingatia suala la lishe bora na kunywa maji zaidi ya glasi nane au lita mbili zilizopendekezwa na madaktari duniani kote ili tuje tufurahie ushindi siku zijazo. Tujiulize, kwa nini tunafungwa kila mara? Ni kweli hatuna mazoezi? HAPANA.
Kwa mahitaji ya LIFEGAIN, maoni na ushauri nipigie 0768 215 956/ 0713 839363


No comments: