Saturday, August 3, 2013

RAIS KIWETE AFUTURISHA WASANII WA BONGO FLEVA IKULU

 
 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Filamu na  Bongofleva,Hemed Suleiman.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,TV,Mbwiga Mbwiguke.
 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Mkongwe wa Bongofleva,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa bongofleva na muigizaji wa Filamu hapa nchini,atambulikae kwa jina la kisanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Bongofleva,Ally Kiba na mdogo wake Abdull Kiba.
 
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongofleva mara baada ya kufturu.Kutoka kushoto,Snura,Keisha,Mwasiti,aliyechuchumaa ni Shilole,Dj Fetty ,Mwanahawa Abdul a.k.a Quee Doreen.
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya pichani shoto Mwasiti Almas na kulia Zuwena Mohamed a.k.a Shilole wakiwa sambamba na Mtangazaji wa Clouds FM,Dj Fetty wakipakua ftari kufuatia mualiko wa Rais Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar jana.
  
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakipata ftari kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar jana kufuatia mualiko wa Rais Kikwete.
 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wa bongofleva,Lawrence Malima a.k.a Marlow,kulia kwake ni Ally Kiba pamoja na Abdul Kiba na kushoto ni Mtangazaji wa East Africa Radio,Samisango
 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wamuziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda na kulia kwake ni msanii wa bongofleva,Cassim Mganga,wakati wa kupata ftari jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar.
 Rais Kikwete akiwasabahi baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya,mara baada ya kupata ftari mapema jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar,Rais Kikwete aliwaalika wasanii mbalimbali kupata ftari ya pamoja Ikulu jana jioni. 

HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI WA JULAI 2013


Hivi ndivyo Kansa ya Ngozi Ilivyomuharibu Mtoto wa Miaka 7....Baba yake aomba msaada kwa wasamaria wema. FROM z

1
Mtoto Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.
Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.
2
“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.

Thursday, August 1, 2013

KARIBU ZuRii FASHION & BEAUTY BOUTIQUE ILIYOPO SINZA LEGHO DAR ES SALAAM.

HABARI NZURI KWA WALE WATEJA WETU VIBONGE aka PLUS SIZE NI KWAMBA MZIGO UMESHAFIKA DUKANI. 
KWA WALE KAKA ZETU MNAO TAKA RABA ZA MTOKO ORIGINAL CONVERSE, TOMS NA VANS PIA ZINAPATIKANA. 
WALE WA SIZE NDOGO PIA KUNA NGUO NZURI SANA ZINAPATIKANA.
WAZAZI WAPENDEZESHE PIA WATOTO WAKO NA ZuRii KIDS COLLECTION.
KARIBUNI MJIPATIE VITU VYA SIKUKUU, MAKAZINI, MITOKO NA KANISANI. 
NGUO NZURI, QUALITY NZURI NA BEI NAFUU. 
LOOK GOOD, FEEL GOOD WITH ZuRii FASHION & BEAUTY BOUTIQUE. 
TUNAPATIKANA SIZA LEGHO, NYUMA YA ROMBO GREEN VIEW HOTEL (KUNA KIBAO BARABARNAI PIA). TUPIGIE +255659189769 or WHATSAPP +447404332910 (BUSINESS ONLY). 
NGUO ZA PLUS SIZE ZINAZOPATIKANA NI SIZE 14-20 (UK).  NA SIZE NDOGO NI 8-14 (UK).
KARIBUNI SANA.



UNIC YAHAMASISHA VILABU VYA KUJISOMEA KWA SHULE ZA MSINGI.

IMG_1445
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akielezea jukumu lao kubwa wao kama Unic ni kuelimisha jamii ambapo kwa kufanya hivyo wamehamasika kuanzisha vilabu vya kujisomea kwa shule za msingi vitakavyowajengea watoto msingi mzuri wa kupenda kujisomea ili kufahamu mambo mengi zaidi yanayoendelea duniani katika nyanja ya Sayansi, Teknolojia na habari.
IMG_1488

Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha ( wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga ( wa nne kushoto) wakikabidhi vitabu vya kujisomea kwa walimu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa kushirkiana na Soma Book Café walihamasisha kuanzishwa kwa Klabu za Kujisomea katika shule tatu za msingi ambazo ni Hananasif, Kumbukumbu na Oysterbay ili kujenga tabia ya kujisomea kwa watoto tangu utotoni. Klabu ya Kujisomea ya Shule ya Msingi Oysterbay imezinduliwa rasmi jana tarehe 31 Julai 2013 kwa kukabidhiwa mashelfu na vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Soma Book Café pamoja na Book Aid International kupitia Maktaba Kuu ya Taifa.
IMG_1498
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akishiriki zoezi hilo la kukabidhi vitabu kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakihamasisha wanafunzi kujenga tabia ya kujisomea tangu wakiwa wadogo.
IMG_1494
Afisa Habari wa UNIC Usia Nkhoma Ledama naye alishiriki zoezi hilo.
IMG_1508
Mwalimu Salome Makanza (kushoto) akitoa shukrani kwa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa msaada huo ambapo waliahidi kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wanafunzi wao kujijengea tabia ya kujisomea na hata kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba shuleni hapo. Katikati ni Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga.
IMG_1398
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akitoa ushauri wa namna ya upangaji vitabu kwa Msimamizi wa Maktaba ya shule hiyo Mwl. Veronica Kassidy.
IMG_1401
Unic team wakijikumbushia baadhi ya vitabu walivyowahi kuvisoma walipokuwa shule za msingi.
IMG_1415
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay wakichagulia vitabu vya kujisomea katika maktaba ya shule yao.
IMG_1513

Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga na Afisa Habari wa UNIC Stella Vuzo wakiteta jambo na baadhi ya wanafunzi wa shule mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi vitabu wanafunzi hao.

Wednesday, July 31, 2013

JIMMIE MAGGETTE MILIONEA NA MFANYABIASHARA MAARUFU AMWALIKA MPIGANAJI WETU DAVIS MOSHA KATIKA KUSHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE HOLLYWOOD, L.A

Davis Mosha "The CEO", Deo Temba "Mayor wa LA" na milionea Jimmie Maggette wakiwa katika Supper Club Hollywood jana usiku kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa tajiri Jimmie ambaye ni mdogo wa mcheza basketball maarufu na tajiri Corey Maggette. MC wa party alikuwa mwanamuziki maarufu J Cole. Wamarekani weusi wanajisikia proud sana wanapokutana na successful people kutoka Afrika.

The CEO Davis Mosha, D. Temba, Jimmie Maggettte na Alex King

 Deo Temba "Mayor wa L.A." katikati ni Mlinzi (BodyGuard) wa Davis Mosha " The CEO"

Baada ya The CEO Davis Mosha kukubali mwaliko wa Jimmie Maggette alitumiwa mlinzi maalum (Body Guard) wa kumlinda, maana sehemu hiyo hawaendi watu wa kawaida, lazima uwe na mlinzi. Hapa Boss Mosha akiteta jambo na Body Guard wake.

   Mayor wa L.A. Deo Temba akikaribishwa kwenye gari na Boss Mosha

NYUMBA INAPANGISHWA MBEZI BEACH

 
Nyumba ipo MBEZI GOIG, mita chache kutoka Barabara Kuu (Bagamoyo Road), upande wa kushoto kama unatokea Mbezi Tangi Bovu. Ina vyumba 3 vikubwa vinavyojitosheleza (3 Master Bedrooms), Two kitchens, Two Sitting Rooms, Garage ya kuweka magari na Fencing.
HAKUNA DALALI. KUJUA BEI NA MALEZO MENGINE, TAFADHALI PIGA SIMU NAMBA: +255 0657 803 139

APARTMENTS FOR LETTING


MAABARA YA KISASA YENYE UWEZO WA KUTAMBUA MAGONJWA MAPYA NA YALE YA HATARI SANA IKIWEMO EBOLA YAZINDULIWA BAGAMOYO.

Bagamoyo 2
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid na Balozi wa Italia nchini Pierluigi Velardi wakizindua maabara ya kisasa kwenye majengo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) huko Bagamoyo hivi karibuni. Maabara hiyo ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inajulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3, na ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI).
Bagamoyo 1
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Seif Rashid hivi karibuni amezindua maabara ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inayojulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3 ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) kwenye maabara zake za Bagamoyo. Pichani anaonekana Mratibu wa mradi wa maabara hiyo Bw.Francesco Vairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afyya (wa pili kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani ( WHO) Dr. Rufaro Chatora na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wakiwa ndani ya maabara hiyo.

BONDIA MTANZANIA OMARI KIMWERI ALIVYO MGALAGAZA Thailand kwa KO

 Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake baada ya kumtwanga  Ekkalak Saenchan  wa Thailand kwa KO raundi ya kwanza  PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa akimsukumia makonde mazito mfululizi bondia Ekkalak Saenchan  wa Thailand na kufanikiwa kumtwanga kwa kwa KO raundi ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita picha kwa niaba ya Mtandao wa SUPER D

Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia akimsikilizia mpinzani wake baada ya kumtwanga kumi nzito na kuhesabilwa wakati wa mpambano wake ata hivyo mpinzani wake akuendelea na kufanikiwa kupata ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza


--

Tuesday, July 30, 2013

:WADAU WA HOUSTON TX WAMPA HAFLA NZITO MPIGANAJI "THE CEO" DAVIS MOSHA KATIKA KIWANJA CHA PAPPADEAUX WESTHEIMER

Upscale Spot ndani ya Houston
Mpiganaji maarufu Davis Mosha akiteta jambo na wadau wa Houston, kulia ni Grace Mmari


Juliet, Christa wakifurahia jambo
 Juliet na Christa wakichagua kitengo
Frank Mutafungwa (Mbabe wa zamani Masaki)  na Alex Kassuwi wakiangalia menu
 Wahudumu walikuwa busy sio mchezo kuhudumia wadau

 Christa akimsikiliza "The Boss" alipokuwa akielezea jambo
  Juliet. Kila mtu makini kumsiliza mpiganaji Davis Mosha akiwapa wadau idea za kutoka.

 The Boss, akitafakari jambo

 Frank akisiliza idea toka kwa The CEO Davis Mosha

Kulia, Alex Kassuwi akichangia jambo katika hafla ya chakula iliyoandaliwa na marafiki wa karibu














 PICHA ZOTE NA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM