Saturday, August 23, 2014

WASANII WATAKAOTUMBUIZA TAMASHA LA FIESTA 2014 JIONI YA LEO JIJINI TANGA WAMJULIA HALI MZEE NJENJE NYUMBANI KWAKE SAHARE.

 Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,almaarufu kama Mzee Njenje akizungumza machache mbele ya wasanii mbalimbali wa bongofleva waliofika nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga,kumjulia hali kutokana na maradhi yake yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa.

Mzee Njenje amewaasa wasanii hao ambao amekiri wazi kuwa wanafanya vizuri katika anga ya muziki wao,kupata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo na suala la kutoendekeza masualaua ya anasa kama vile ulevi,ngono na mengineyo ambayo huchangia kuporomoka kwa wasanii wengi,amesema kuwa Muziki wa sasa una ushindani mkubwa hivyo kila msanii anapaswa kujituma kwa namna anayoona inafaa ili kutimiza malengo yake sambamba na kuitangaza nchi kwa ujumla.
 Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Rachael na Linah wakiwa wamepozi katika picha ya ukumbusho na Mzee Njenje.
 Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya,Alli Kiba akizungumza jambo na Mzee Njenje. 
Mzee Njenje akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakaotumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014 linalofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga,Wasanii hao walikwenda kumsabahi mkongwe huyu wa Muziki hapa nchini,Nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga ambako ndiko anaendelea kupata matibabu yake ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa,Mzee Njenje amesema kuwa kwa sasa anamshukuru Mungu anaendelea vizuri na afya yake inazidi kuimarika kadiri ya siku zinavyozi kwenda.  
 Baadhi ya Wasanii mbalimbali ambao Watatumbuiza kwenye tamasha la Fiesta jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani ,wakiwasili nyumbani kwa Mzee Njenje,Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga kumjulia hali.Picha zote na Michuzi Jr-FIESTA TANGA

Rais Kikwete azindua mradi mkubwa wa maji ya mji morogoro, awataka viongo


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014


Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wataalamu walioshughulikia ufungwaji wa mtambo huowakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Morogoro mjini Mhe Aziz Aboud wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wadau wa mji wa Morogoro wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Jengo la  mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Vijana wakishangilia wakati wa sherehe za ufunguzi  rasmi wa mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Baadhi ya wafanyakazi wa MORUWASA  wakishangilia wakati wa sherehe za ufunguzi  rasmi wa mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Burudani wakati wa sherehe hizo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akifungua pazia la sherehe hizo
Sehemu ya jengo la mradi huo
Kwa ubavuni
Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu akitoa muhtasari wa mradi huo
Bango linajieleza
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akipokea kwa niaba ya serikali  hati rasmi ya kukamilika kwa mradi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akimkabidhi hati hiyo Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike
Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akifurahia
Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Rais Kikwete akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu kwa kufanuikisha mradi
Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiongea machache 
Mama Salma Kikwete akimpongeza Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher akisoma hotuba yake kwa Kiswahili wakati wa sherehe hizo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akiongea wakati wa sherehe hizo na kumkaribisha Rais Kikwete aongee na wananchi
Rais Kikwete akizungumza na kuzindua rasmi mradi huo mkubwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifunua pazia kuzindua mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifurahgia baada ya kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akibofya kitufe kupiga king'ora kuzindua rasmi mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine wakielekea kukagua  mradi huo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikata utepe kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akipata maelezo ya mradi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASA 
Sehemu ya mitambo ya mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikagua mitambo ya  mradi huo
Mkurugenzi  Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiendelea kutoa maelezo ya mradi

Rais Kikwete atawazwa kuwa chifu msaidizi wa waluguru na chifu kingalu

 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.  Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha "muibukaji", kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.


 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvika  mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvipa pama lililosukwa kwa ukindu  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimkabidhi kifimbo maalumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimuonesha  Rais Jakaya Mrisho Kikwete namna ya kuweka kifimbo maalumu begani wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo
 Mke wa Chifu Kingalu akimkabidhi Mama Salma Kikwete shuka katika sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia kifimbo maalumu alichokabidhiwa wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akiongea na wananchi wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akihutubia  wakati wa sherehe hizo
 Umati wa wananchi ukimsikiliza Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila wakati wa sherehe hizo
 Hotuba ikiendelea 
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akisikiliza maelezo Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Morogoro Injinia Juliana J. Msaghaa akieleza juhudi za upatikanaji wa maji safi na salama wilayani humo wakati wa sherehe hizo
 Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila  wakati wa sherehe hizo
  Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia pama lake wakati wa sherehe hizo
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14 akibadilishana mawazo na Rais Kikwete wakiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe Joel Bendera na kushoto ni msaidizi wa Chifu Kingalu
 Mama Salma Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe hizo, akisisitiza umuhimu wa kinamama kujiunga na SACCOS pamoja na kupambana na ugonjwa wa Fistula kwa wakati muafaka
Rais Kikwete akiwaaga wananchi wa Kinole baada ya sherehe hizo.
PICHA NA IKULU