Saturday, November 14, 2015

MTEMVU ACHANGIA KIKUNDI CHA SANAA TSH. MILIONI 3

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas  Mtemvu achangia Kikundi  cha Sanaa cha K & S Alt Vision cha Temeke Jijini Dar es Salaam,  Pesa Taslim Tsh. Milion 3 (PICHA ZOTE NA KAMISI MUSSA)
Mtemvu akizungumza jambo na kikundi cha Sanaa na  Viongozi wao
Msemaji wa kikundi hicho, Saba Habibu akizungumza jambo kabla ya kupokea pesa hizo

 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas  Mtemvu (kulia) akimkabidhi msemaji wa kikundi  cha Sanaa cha K & S Alt Vision cha Temeke Jijini Dar es Salaam,  Pesa Taslim Tsh. Milion 3,  Saba Habibu,  kwa maandalizi ya kuandaa Filamu inayoitwa Kwanini Rafiki Yangu? ambapo leo wanaanza safari kwenda  Mkoa wa Pwani Bagamoyo katika Kijiji cha Kaole ambapo wataweka kambi kwa ajili ya kazi hiyo, wa Pili kulia ni Diwa wa Kata ya Kilakala, Amiri Osama na watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kikundi hicho, Edwin Mgoli
Msemaji wa kikundi hicho, Saba Habibu akitoa shukurani kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  kwa niaba ya kikundi hicho
Diwani wa Kata ya Kilakala Amiri Osama akitowa shukurani kwa niaba ya kikundi hichokwa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu Dar es Salaam.
Mtemvu katika Picha ya pamoja na Kikundi cha Sanaa cha K& S Alt Vision.

 Msemaji wa kikundi hicho akizungumza kwa niaba ya kikundi hicho cha Sanaa cha K& S Alt vision  mara baada ya kupokea Pesa Tsh. Milioni 3 toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke,
 Abbas Mtemvu, Saba Habibu, alisema anamshukuru Mtemvu kwa moyo wakujitolea

 Mtemvu anamoyo wa dhati na ukizingatia amepita katika kipindi kigumu cha mpito hakuweza kuwaangusha kwakuwa na msimamo wa kuwasaidia, aliendelea kusema  Saba Habibu, 

Mtemvu alikuwa akimsihi msemaji huyo kama mwanaye wa kumzaa kwamba ahadi yake ataitimiza kama alivyo itowa kwa kundi lake ipo palepale haijalishi popoteatapokuwa ataitowa kwa kukamilisha ahadi yake kwani aliitowa kwa ridhaa yake na moyo wake yeye kama yeye atawasaidia,

 kauli hiyo iliendelea kunipa faraja  msemaji wa kikundi hicho Saba Habibu alisema na akiendelea kusema, hata hivyo anawashukuru Wasanii wenzake kwa kumuamini wakati alipokuwa akifanya mawasiliano na Mtemvu. msemaji huyo alisema,
tumeomba na tumefarijika kwa msaada huu na tunamuahidi hatutomuangusha kwa kile tulichokiomba tutakifanyia kazi kwa nguvu zao zote na kwauadilifu mkubwana kwa unyenyekevu mkubwa hadi kufikia malengo yao na mwisho akasema Mungu awaongoze.

Diwani wa Kata ya Kikalaka, 
akizungumza kwa kumpongeza kwa moyo wake anao endelea nao kwa kusaidia vikundi vingi na haijawahi tokea kwa Mbunge mwenyekusaidia vikundi vingi kama mwenzetu, rafikiyetu, kaka yetu, ambaye amesaidia Vikundi vingi na vijana wengi kwa kuwasaidia kwa hali na mali na kuwa begakwabega na kumtia moyo na kumuombea Dua kwa mwenyeezi mungu ili aweze kuwasaidia vijana wa temeke

Diwani huyo akasema, waswahili husema  kutowa ni moyo wala si utajiri na wala si tajiri sana bali nikuwa na moyo kuwasaidia vijana wetu wa Jimbo la Temeke, 

Hivyo tuzidi muombea Dua kwa mwenyeezi Mungu ampe maisha marefu na mungu amjalie aweze pata riziki na maisha mema na tutaendelea kumkumbuka daima dumu. (Amin) 

No comments: