Friday, October 20, 2017

DC MTATURU AFUNGUA MKUTANO JUU YA MAOMBI YA KUREKEBISHA BEI ZA HUDUMA YA MAJI WILAYANI MANYONI


Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua  wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira

Baadhi ya wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi
wa Mazingira wakifatilia Mkutano

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua  wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira. (Picha Zote Na Mathias Canal)

Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Nobert Kahyoza akiwasilisha hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA wakati wa mkutano wa wadau na watumiaji wa huduma ya maji Manyoni. Wengine ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe Moses Matonya.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe Moses Matonya akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na watumiaji wa huduma ya maji kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo ambaye ni Mhe Mtaturu.

Meneja Ufundi wa Mamlaka na Usafi wa Mazingira Mji Mdogo wa Manyoni (MAUWA) Ndg Maduhu Shija akiwasilisha taarifa ya mapitio juu ya maombi ya kubadili bei za maji.
 Baadhi ya wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira wakifatilia Mkutano.
Mkazi wa eneo la Manyoni Mjini ambaye ni mdau wa huduma ya mamlaka ya Maji Bi Bahati Suleiman Matonya akichangiamada wakati wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe Moses Matonya wakati wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.

Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua  wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.

Na Mathias Canal, Singida

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu leo Octoba 20, 2017 amefungua  Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira juu ya kutoa maoni na mapendekezo juu ya maombi ya Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Wilaya ya Manyoni (WSSA) ya kurekebisha bei za Huduma za Maji Safi.

Akizungumza Wakati wa ufunguaji wa Mkutano huo ulioandaliwa na (EWURA) na kufanyika katika Ukumbi wa Maktaba Mhe Mtaturu Alisema kuwa Maji Ni Huduma muhimu kwa wananchi na uchumi wa Nchi yoyote ile na upatikanaji wake Ni kielelezo tosha Cha ubora wa maisha ya watu wote kwa ujumla hivyo Mkutano huo Ni dira ya maboresho ya upatikanaji maji kwa ajili ya kuwapunguzia kadhia wanayokumbana nayo wananchi ikiwemo umbali kwa ajili ya kuifikia Huduma hiyo.

Alisema kuwa Mwaka 2001 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya kuanzisha chombo chenye jukumu la kudhibiti na kusimamia watoa Huduma (EWURA) katika sekta ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ikiwa Ni pamoja na sekta ya nishati ambapo baadhi ya majukumu yake Ni pamoja na kudhibiti ubora wa Huduma ya Maji nchini kwani awali Huduma za Maji zilikuwa zikisimamiwa na serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kutumia Sheria na mikataba mbalimbali.

Alisema Uundwaji wa Mamlaka za udhibiti Kama EWURA Ni kielelezo Cha utekelezaji wa kanuni za utawala Bora wenye lengo la kutenganisha majukumu ya kuandaa sera na kusimamia utekelezaji wake kwa upande mmoja, na yule wa udhibiti kwa upande mwingine ambapo serikali imebaki na jukumu la kuandaa sera na kuwasilisha miswada ya Sheria Bungeni, Kusimamia utekelezaji wa sera na mikakati yake, Kuwezesha wananchi kushiriki katika masuala yanayohusu mustakabali wao na kuhamasisha wawekezaji kushiriki katika maendeleo ya sekta na KUJENGA miundombinu.

Mhe Mtaturu Alisema kuwa pamoja na Mkutano huo wa majadiliano Kati ya wadau wa maji Wilayani Manyoni lakini wananchi wanapaswa kutambua kuwa ili kuboresha Huduma za upatikanaji wa maji pia Ni muhimu wananchi kutunza Mazingira kwani maji Yana mahusiano ya Moja kwa Moja na Mazingira.

Mhe Mtaturu Alisema kuwa uharibifu wa Mazingira Ni chanzo Cha upatikanaji hafifu wa maji hivyo wanachi wanapaswa kupanda miti kwa wingi ikiwa Ni pamoja na kutunza vyanzo vya maji.

Sambamba na hayo pia aliitaka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mji Mdogo wa Manyoni (MAUWA) Inayojihusisha na Huduma ya usambazaji maji Safi na salama ndani ya Mji wa Manyoni kutoa taarifa sahihi ya utendaji kazi kwa wateja wao na EWURA lakini zaidi kusimamia kwa umakini jukumu lao la Msingi la utoaji Huduma na bidhaa Bora na kwa Wakati kwa watumiaji wengi zaidi.

Mhe Mtaturu alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kujenga uwezo wa kupata fedha za kuimarisha miundombinu ya kusambaza maji ili kutimiza dhamira ya kuwawezesha wananchi kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Nobert Kahyoza ambaye ni Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Alisema kuwa Bei ya ada zinazotozwa Sasa na Mamlaka ya Maji Manyoni kwa ajili ya Huduma zake zilipitishwa mwaka 2011 hivyo ili kuongeza ufanisi katika Huduma ya utoaji maji EWURA imeamua kujadiliana na wadau wake ili kurekebisha gharama za Maji.

Marekebisho hayo ya Bei yatayahusu makundi yote ya wateja kwani marekebisho hayo ya Bei yatasaidia kupata fedha za kutosha kukidhi gharama za uendeshaji Kama vile uzalishaji na matengenezo vya vipuri mbalimbali.

Naye Meneja Ufundi wa Mamlaka na Usafi wa Mazingira Mji Mdogo wa Manyoni (MAUWA) Ndg Maduhu Shija Alisema kuwa uzalishaji wa maji kwa ajili ya Mamlaka ya Maji Manyoni unafanyika katika maeneo ya Mitoo Mbugani (Visima 8), Kaloleni kisima Kimoja, Na Mitoo ya Chini Kisima kimoja ambapo kea ujumla Visima hivyo vina uwezo wa kutoa lita 794,000 kwa siku.

Alisema miongoni mwa mikakati ya utatuzi Ni pamoja na kuongeza vyanzo vya maji kwa kuchimba Visima Vinne ndani ya miaka mitatu ijayo, na Kuongeza idadi ya wananchi wanaopata Huduma ya Maji Safi na salama kwa kuongeza idadi ya maunganisho ya maji katika makundi yote na kupeleka mtandao wa maji kwenye maeneo ya Jasiliamali, Kaloleni ya Chini, Mwembeni, Chang'ombe na Mitoo ya Chini.

Mikakati mingine Ni kuendelea kuomba fedha kwa ajili ya utekelezaji mkubwa wa Mradi wa maji wa Tsh Bilioni 19 kwa ajili ya kuboresha Huduma ya maji, Kununua madawa ya kutibu maji yatakayowezesha maji yanayosambazwa kwa wateja na kupendekeza marekebisho ya Bei za Maji.

AIDHA, Katika Mkutano huo Wadau na watumiaji wa maji, Baraza la ushauri la watumishi wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC), Baraza la wawakilishi la serikali (GCC) wamepinga vikali ongezeko la zaidi ya asilimia 100% kwenye gharama za upatikanaji wa huduma za maji safi na Usafi wa Mazingira Manyoni.

MWISHO

No comments: