Monday, April 23, 2018

JE UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUPENDEZESHA NYUMBA YAKO NA JUMIA?

Na Jumia Tanzania

Asilimia kubwa miongoni mwetu tunaishi kwenye nyumba ambazo hatuwezi kupaita ni nyumbani. Najua unaweza ukajiuliza kuna tofauti gani kati ya nyumba na nyumbani.

Nyumba ni jengo ambalo unaishi na kukupatia mahitaji yako ya msingi pamoja na hali ya usalama. Wakati, nyumbani ni mahali
ambapo panakupatia amani na utulivu wa kiakili, mahali ambapo unatamani kuwepo pindi unapokuwa mbali na pilikapilika za ulimwengu.


Lakini jambo la kusikitisha miongoni mwa watu wengi wanaishi katika nyumba ambazo hazistahili kuziita ni nyumbani. Mwonekano wao nje na shughuli wanazozifanya ni tofauti kabisa na mahali wanapoishi na kutumia muda mwingi kutafakari mustakabali wa maisha yao ya kila siku.

Je na wewe unadhani kwamba nyumba yako unaweza kuiita ni nyumbani? Unajisikia vibaya kwamba sehemu unayoishi haistahili kuitwa nyumbani? USIJALI


Amini usiamini nyumba yako inaweza kuwa na muonekano mzuri, wa kisasa na wenye kustarehesha bila ya kutumia gharama kubwa! Jambo la msingi ni kufahamu ni kwa namna gani unaweza kufanya manunuzi ya vifaa ambavyo vitaipendezesha nyumba yako au sehemu unayoishi!

Jumia, inaendesha kampeni inayokwenda kwa jina la ‘BIG HOME MAKEOVER.’ Kampeni hii imedhamiria kuwawezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na nyumba zenye hadhi ya kuitwa nyumbani. Kupitia kampeni hii Jumia inalenga kupendezesha nyumba za wateja wake kwa kuwapatia mapunguzo makubwa ya bei ya vifaa mbalimbali vya nyumbani.


Akizungumzia juu ya kampeni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Vifaa vya Nyumbani wa Jumia Tanzania, Priscilla Eliphas ameelezea kuwa, “tumegundua kuwa watu wengi wana kasumba ya kutumia vifaa vya nyumbani kwao kwa muda mrefu. Kwa mfano, unaweza kukuta mtu anatumia jokofu (friji), jiko la umeme, mashine ya kufulia nguo au kupasha chakula moto pamoja na samani za ndani kwa muda wa takribani miaka 10! Na unaweza kustaajabu ni sababu zipi zinazopelekea mtu kuendelea kutumia vifaa kwa muda mrefu kiasi hiko! Na bado wengi miongoni mwao huendelea kuvitumia kadri iwezekanavyo. Tunafahamu kwamba vifaa kama hivyo ni uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye nyumba za kuishi hivyo ni dhahiri kwamba watu huwa makini kwenye ubora na makampuni yanayotengeneza hivo vifaa.” 

“Jumia inafahamu kwamba kufanya mabadiliko kwenye nyumba hususani kuifanya iwe na muonekano mpya na wa kuvutia ni kazi kubwa na tena yenye gharama. Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyotupelekea kuja na kampeni ya kupendezesha nyumba za wateja wetu. Kwa kuliona hilo tumekuja na kampeni ya zaidi ya wiki moja ya manunuzi ya vifaa tofauti vya nyumbani kama vile jikoni, sebuleni na mapambo ya nyumbani. Kampeni hii imeanza tangu Aprili 16 na kudumu mpaka Aprili 26, wateja wataweza kununua bidhaa lukuki za nyumbani kwa bei nafuu zenye ofa na mapunguzo makubwa,” alihitimisha.


Jumia inawasihi wateja wake kuitumia kampeni hii ipasavyo kwani wameshirikiana na kampuni kubwa za nchini Tanzania na kimataifa zinazotengeneza bidhaa zenye ubora wa kuaminika kama vile Samsung, Bruhm, Sony, Geepas, Nippotec, TCL, Star X, Philips, Aborder, Nikai, Ocean na Tronic. Cha kuvutia zaidi kuna mapunguzo ya bei, ofa, vocha za bure na zawadi kemkem kupitia kwenye tovuti yao! 

Wateja wanaweza kufanya manunuzi kwa urahisi kupitia mtandaoni, mahali popote walipo kwa bei za kipekee. Kwa kuongezea, bidhaa hufikishwa kwa mteja alipo kwa uharaka zaidi huku mteja akiwa na fursa ya kufanya malipo baada ya kuridhika na bidhaa alizoziagiza. Wateja wamepewa machaguo mengi zaidi ya bidhaa, takribani bidhaa zaidi ya 20,000 zimewekwa mtandaoni huku punguzo la bei likifika mpaka asilimia 60! 

No comments: