Saturday, August 11, 2007

Taarifa maalum kwa Chahali, gazeti la Kulikoni

Kampuni ya Global Publishers & General Entreprises wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi, imesikitishwa sana na makala iliyoandikwa katika Gazeti la Kulikoni linalotolewa na Kampuni ya Media Solutions Ltd ya jijini Dar es Salaam.

Makala hayo yaliyochapishwa katika toleo lake la Jumatano ya Agosti 8, mwaka huu, yaliyokuwa na kichwa cha habari ‘Magazeti ya Udaku yanaandika habari feki’, iliushutumu uongozi wa gazeti hili kuwa waliandika habari ya uongo katika toleo lake la Julai-20, mwaka huu.

Habari ambayo mwandishi huyo alidai kuwa ni ya uongo ilikuwa na kichwa kisemacho, ‘Warembo wa TZ wapiga picha za X tupu’.

Pamoja na shutuma hizo, Kulikoni pia kupitia kwa mwandishi wake anayejiita Evarist Chahali, mwanafunzi Mtanzania anayesoma katika Chuo cha Aberdeen, nchini Scotland, lilidai kuwa, mhariri alitumia picha za wasichana watatu ambao alielezwa na rafiki yake kuwa ni wacheza filamu za ngono (Porn stars) nchini Marekani na si Watanzania wanaojiuza kama gazeti hili lilivyoandika.

Kupitia makala yake, mwandishi huyo amediriki pia kulishambulia gazeti hili waziwazi akidai kuwa yeye binafsi linamkera sana kwani linaandika habari za kuzusha.

Maelezo aliyoandika mwandishi huyo kwa kweli yanatufanya tuamini kuwa, digrii alizonazo zina mashaka kutokana na kushindwa kwake kufanyia uchunguzi wa kutosha kabla ya kufikia hatua ya kutoa shutuma kama hizo zenye lengo la kuchafuliana.

Kwa ujumla, tungependa kusisitiza kuwa habari iliyoandikwa kwenye gazeti hili ni ya kweli na kwamba wasichana waliochapishwa wametambulishwa katika mtandao huo kuwa ni watanzania wanaojiuza kwa njia ya kupiga picha chafu na si Wamarekani kama alivyodai Chahali.

Tunaamini kuwa Chahali ni msomi, hata kama si katika nyanja ya uandishi, hivyo hakupaswa kuandika shutuma zile baada ya kumnukuu mtu kwa maneno ambayo hakuyafanyia uchunguzi, kwani hatua hiyo inaweza kumfanya ashindwe kuthibitisha mbele ya sheria.

Kimsingi picha za wasichana waliochapishwa kwenye gazeti hilo ni Watanzania kama walivyojieleza wenyewe kupitia tovuti ambayo tumelazimika kuiweka wazi mwisho wa taarifa hii, ili kuuthibitishia umma kuwa hatuandiki, hatujaandika na wala hatutaandika habari ‘feki’.

Chahali anapaswa kuelewa kwamba habari tuliyoiandika haikuwa jambo geni sana ambalo haliwezi kufanywa na Watanzania wa leo, hayo mambo yapo, tena mengine ni mazito zaidi na hayaandikiki kwenye gazeti.

Aidha, asifikiri wasomaji wetu ni wajinga ambao wanaweza kudanganywa kirahisi kwa kuwaandikia habari za uongo. Hayo ni mambo ya kawaida katika jamii yetu hivi sasa, lakini Chahali anaonekana kuwa ni mgeni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kufikiri kwamba kitu kama hicho kinafanywa na Wamarekani pekee.

Tunapenda kumfahamisha Chahali kuwa sisi hatuna haja ya kutunga habari ‘sensational’ wakati hizo zipo nyingi katika jamii tunayoishi na kama yeye hazijui haina maana kuwa hazipo. Hivi inawezekana kweli yeye tu ndiye awe ameiona habari ile ni ya uongo miongoni mwa mamilioni ya Watanzania wa ndani na nje ya nchi walioisoma?

Tunawaheshimu sana wasomaji wetu na wao ndio vyanzo vyetu vikuu vya habari tunazoziandika. Chahali anapaswa kuelewa kwamba tunachokiandika, siku zote huwa kinatoka kwa wasomaji hao na ndio maana wamekuwa wakituamini kwa miaka karibu kumi sasa.

Kwa kumrahisishia kazi Chahali na kumjuza kuwa hatuna sababu ya ‘kutunga’ habari ili tupate pesa, atembelee tovuti hii: http://swallowmyjuice.hi5.com ili akajionee mwenyewe wasichana hao anaodai ni Wamarekani, ili siku nyingine aache kuropoka na kuingilia mambo ya watu asiyoyajua.

Hatukatai kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake ilimradi havunji sheria, lakini si vizuri kutoa shutuma nzito dhidi ya mtu mwingine kwa chuki binafsi na ‘roho ya kwa nini’, kama vile ambavyo Chahali mwenyewe amesema katika makala yake, eti ‘mmeshatengeneza faida ya kutosha’!

Kimsingi magazeti ya Udaku yanafanya kazi sambamba na vyombo vingine katika kupasha habari, kuelimisha na kuburudisha jamii na kwamba hayapo Tanzania tu bali hata katika nchi nyingine kama Uganda, Marekani, Uingereza na kwingineko na yanapendwa kama yanavyopendwa ya hapa nchini.

Mwisho, kwa taarifa hii tunawaomba wahariri wa Kulikoni, ambao tunawaheshimu sana, kuwa makini na waandishi wanaotaka kutumia gazeti hilo kwa manufaa yao binafsi kwa lengo la kuchafuliana na kushushiana hadhi mbele ya jamii.

Imetolewa na kusainiwa na:
Abdallah Mrisho
Meneja Mkuu
Global Publishers & General Enterprises Ltd

10 comments:

Anonymous said...

Kaka Mrisho,

Nimeandika hapa kama mara nne hivi kusistiza kuwa wale wasichana unaoleta kutoka Hi5 siyo watanzania lakini post zangu hazitoki. Huyu anayeitwa Melanie unayemleta hapa na Grace, mimi nawafahamu siku nyingi sana karibu miaka minane iliyopita wakati walipokuwa regular pale South Beach, Miami. Wote hawakuwa watanzania ingawa "Grace" alikuwa mwafrika, "Melanie" alikuwa anaonekana kama mchanganyiko wa mwasia na mwafrika, na picha uliyoonyesha ya "Melanie" ni ya zamani sana. Kwa sasa hivi ni mama mzima kiasi ingawa sijamwona siku nyingi sana zaidi ya miaka sita tangu nihame kutoka Miami. Picha zake nyingine za wakati huo ziko hapa

Anonymous said...

Kuna uhakika gani na usahihi wa habari zilizotolewa kwenye tovuti ya http://swallowmyjuice.hi5.com ? kwamba hao akina dada ni Watanzania. Je, ni kwa sababu wameandika kuwa wanatoka Tanzania? Au kuna njia nyingine ya kuhakikisha ukweli wa hizo habari?

Anonymous said...

Naona kuendelea kujadili mada hii ni kupoteza muda na kujiweka katika hali ya watu kutokukuamini kutokana na mada yako.

Kwanza kabisa kuchukua habari kutoka kwenye website kama Hi5, na kuiandika kwenye gazeti ni kosa kubwa, huko ndio kupotosha jamii sasa. Kama ulivyosema ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ukumbuka kuwa hata mimi ambaye ni mwanaume naweza kusign in, na kujiita Mtanzania, mwanamke...na jina Feki ili mradi tu kusumbua watu....Sasa wewe mwandishi ulikuwa na uhakika gani? Au una amini sana wetu na kufanya ndio chanzo cha habari....Logically, huyu jamaa aliyeponda hiyo habari alikuwa right, kama unatueleza kuwa habari yako uliitoa kwenye Hi5....Si kumtetea, si mfahamu ila katika kuweka mambo wazi.

Anonymous said...

mimi naona Chahali yuko sawa kwa maelezo aliyotoa, habari ni udaku na chanzo chake si cha uhakika, yote haya ni kufanya biashara ya kuuuza magazeti

Anonymous said...

ni kweli chahali amechemka kama mrisho ulivyo chemka

Anonymous said...

chahali amechemka

Anonymous said...

Mimi sasa naona global publisher mnajishushia hadhi,kama mnaweza kuripoti habari ambayo chanzo chake hakina mhariri,sijui mnakwenda wapi.Mtu yeyote anaweza kuitumia hiyo hi5 atakavyo,kuandika chochote atakacho wala hakuna wa kuhoji,umepewa uhuru wa ku upload picha ,bila kujali ni yako au ya nani,kuandika utakacho ndo maana kuna picha nyingi tu za mastar wa porn ambazo watu wanazitumia kwenye profile zao,sasa jaribuni kutoa habari zilizo haririwa siyo kumjia juu tu Chahali ,inavyoonyesha hamna taaluma ya habari.

Anonymous said...

Hivi na swala la kashfa ya kuchangia kwa kiasi kikubwa kusababisha kifo cha amina chifupa pia mlilitolea maelezo ya kina namna hii, Global publishers BOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Mrisho,mimi nadhani wewe ndio kihiyo kabisa.Hivi doesn't it make sense to you till now that your story was a fake one?Ningekuwa Chahali haki ya mungu mngekutana na mimi mahakamani kwa maneno yenu.Ohh mara elimu yake ina utata,mara hafanyi vizuri darasani..upuuzi mtupu.Wewe ushasikia mwanafunzi wa PhD akawa wa kwanza au wa mwisho darasani?Umesomea wapi wewe?Au na wewe ndio wa Royal College sijui.Acheni nyie kudanganya watu,toeni habari kutoka kwa vyanzo vya uhakika.Mbona blogu za wenzenu kama kina Michuzi,bongocelebrity,mjengwa,jikomboe nk wanapata habari za uhakika?Mnashindwa vipi ninyi wenye kampuni kabisa??

Anonymous said...

hiyo habari uliandika bro. mrisho ni ya kizushi na kama vp omba radhi kwa chahali na umma pia,mbona ukwelli umetundikwa wazi na huyo Mr. KICHUGUU kwenye hiyo comment yake!!!sasa mpaka kufikia point hiyo kama hutaki kukubali kwamba umelisha watu 'matango pori' basi wewe utakuwa unataka upinzani kwenye fani ambayo inaonesha ni mgeni..kubali kosa bro kwa manufaa ya umma..by er