Baada ya Mungu kutuumba, alitupa pia zawadi nzuri ya matunda na mboga. Kila tunda au mboga, ina faida zake za kipekee katika kutoa tiba ama kinga mbadala kwa mwanadamu dhidi ya maradhi. Halikadhalika, kila tunda au mboga ina kazi ya kipekee mwilini katika ukuwaji na ustawi wa mwili.
Matunda na mboga zina aina zote za madini ya asili, vitamini, chumvi, sukari, tindikali, n.k, hivi ni vitu vya asili ambavyo hutoa dawa mwilini katika njia ya kipekee kabisa na iliyo salama zaidi.
Kila siku tunaelezwa kwamba, kutokana na umuhimu wa vitu hivi, tunatakiwa tuvile kwa wingi kila siku, vinatakiwa vichukue sehemu tatu kati ya nne ya mlo wetu wa kila siku. Hii ina maana kwamba kama una vyakula vinne mezani, vitatu viwe ni mboga na matunda na kimoja tu ndiyo kiwe chakula kingine.
Ili kupata virutubisho vyote, inashauriwa kutokumenya, kupika wala kuhifadhi matunda kwa muda mrefu. Embe linapoliwa na maganda yake lina faida nyingi kuliko lile lililomenywa, halikadhalika matunda mengine yanayoweza kuliwa bila kumenya maganda, kama vile epo, pera, n.k
Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu cha You Are What You Eat, Bi. Podder, ulaji wa matunda halisi, ni bora kuliko kutengeneza juisi kwa sababu katika mchakato wa kuandaa na kutengeneza juisi, virutubisho vingi hupotea zikiwemo ‘fibre’ ambazo hupungua kutokana na kusagwa na mashine ya kutengeneza juisi (blender), halikadhalika sukari na chumvi ya asili iliyomo kwenye tunda ama mboga nayo hupotea.
EPO
Kama tulivyoona wiki iliyopita katika makala kuhusu ugonjwa wa ‘gauti’, epo (Apple) ama Tufaha, kama linavyojulikana kwa jina lingine, lina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Tunda hili limejipatia umaarufu mkubwa duniani kutokana na faida zake kiafya, ambazo hupaswi kuzikosa.
Miongoni mwa virutubisho vinavyopatikana kwenye tunda hili muhimu ni pamoja na ‘pictin’, kirutubisho ambacho kinaaminika kuwa na uwezo mkubwa wa kuponya matatizo yote ya kwenye utumbo na kufanya usagaji wa chakula tumboni uende sawa.
Halikadhalika tunda hili, ambalo kwa Bongo huuzwa kati ya shilingi 400 na 500, ni dawa ya ini, kwani lina uwezo wa kuhuisha ini lenye matatizo kwa kuliongezea kiwango cha nyongo kinachotakiwa kufika na kuongeza uwezo wake wa kuondoa sumu mwilini.
Vile vile Epo lina uwezo wa kusafisha damu mwilini, kuondoa vijimawe kwenye figo, kuondoa tindikali tumboni na kurekebisha mfumo mzima wa tumbo lenye matatizo. Mbali na faida hizo za kimwili, lakini pia epo linatumika sana katika masuala ya kuandaa vipodozi vya aina mbali mbali.
ROZELA
Huu ni mmea ambao hutoa maua mekundu na umeenea sana nchini Tanzania. Katika siku za hivi karibuni, watu wengi wameshagundua siri ya mmea huu kwa kuchuma maua yake na kutengeneza juisi ambayo ina faida nyingi mwilini.
katika nchi za magharibi, Rozela, ambayo kitaalamu inajulikana kama ‘Hibiscus Sabdariffa’ au ‘Rosella’, hutumika kama tiba ama kinga mbadala ya magonjwa mbalimbali yanayoweza kumpata binadamu.
Magonjwa yanayoweza kutibiwa na Rozela kama dawa ni pamoja na matatizo ya figo ambayo yanaweza yakarekebishwa na kutoweka, ute wa muda mrefu tumboni (mucus) na kuziba kwa pua.
Orodha kamili ya magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa mtu kutumia Rozela mara kwa mara, ni kama ifuatayo:
*kupunguza mafua
*Kufungua pua zilizoziba
*kusafisha ute tumboni (mucus)
*makunyazi ya ngozi
*kulainisha choo
*kuboresha utendaji kazi wa ini
*kuongeza damu, n.k
kuna njia mbali mbali sahihi za kutengneza juisi ya Rozela na kutumia ama kuhifadhi. Maua yake yanaweza kukaushwa na kutengenezwa juisi yakiwa yamekauka ama kutumia kama chai.
Rozela bora ni ile ambayo ingali fresh (mbichi) unayoweza kutengeneza juisi ama kinywaji kingine kwa lengo la kulinda afya yako. Tutumie matunda haya yaliyoletwa kwetu na Muumba wa vitu vyote kama zawadi, ili tuwe na afya imara.

No comments:
Post a Comment