Monday, June 23, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

TID kujiachia TA

Kutoka ndani ya Top Bend, kijana Khalid Mohamed ‘TID’ anatarajia kujiachia na wastaarabu wa Korogwe Mkoani Tanga, kupitia shoo moja ya kutosha, Rebeka Bernard anadondoka nayo.

Kwa mujibu wa waandaaji, Korogwe Traders, ‘Top In Dar’ atafanya mashambulizi ‘TA’ Julai 25 mwaka huu, ndani ya ukumbi wa Chuo cha Waalimu (TTC) cha Korogwe.

“Lengo kubwa ni burudani, ukizingatia kwamba TID hatakuwa peke yake, atapigwa tafu na wasanii wengine kama Mass Diso na wengine kibao,” alisema Stanley Joel Bendera, mratibu.
********************************************************

Tollywood yaingia mzigoni rasmi

Kampuni mpya ya usambazaji wa filamu za Kibongo, Tollywood imeingia mzigoni rasmi kwa ajili ya kazi hiyo, ambapo kwa kuanza siku chache zijazo itadondosha sokoni muvi mpya yenye jina la ‘Mama Devi’ ambayo imeibua vipaji vipya zaidi katika tasnia hiyo.

Msemaji wa kampuni hiyo, Chris Magori amesema na safu hii kwamba, Tollywood imeamua kuanza na filamu hiyo kwasababu imetengenezwa katika ubora wa hali ya juu huku ndani yake ikiwa imejaa mafunzo ya kutosha ambayo yatasaidia kuielimisha jamii hususan wanandoa.

“Filamu hiyo, Mama Devi inaelezea kisa cha mke wa mtu mmoja aliyepigwa risasi baada ya kufumwa akijirusha baa na mume wa mtu,” alisema Magori.

“Wadau wakumbuke kuwa kampuni yetu sasa inazalisha na kusambaza filamu katika VHS, DVD na VCD hivyo nawashauri wenye filamu zao wafike katika ofisi zetu zilizopo Sinza Bamaga, Dar es Salaam ili waweze kupata maelezo kamili ya jinsi gani wataweza kufanya kazi na sisi,” alisema Magori.
***************************************************
Mzuka zaidi King OFHip Hop

Ebwanaee! Mzuka unazidi kupanda kwa mashabiki wengi na hata wakali waliotajwa kuingia kunako shindano la kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop, nawazungumzia wale wanaharakati wanaofanya staili ngumu yaani Hip Hop kupitia kategori ya muziki wa kizazi kipya.

Tunawaomba radhi wasomaji wetu ambao hawakuweza kupiga kura wiki iliyopita kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza ambayo hivi sasa yamesharekebishwa.

Unachotakiwa kufanya hivi sasa wakati wa kupiga kura, unaandika neno HP unaacha nafasi, unaandika jina la msanii unayehisi anastahili kuwa Ijumaa King Of Hip Hop kisha unatuma kwenda namba 15551.

Msanii atakayepigiwa kura nyingi ndiye atakayekuwa mshindi wa shindano hilo, baada ya wiki mbili msanii mmoja atakuwa akitolewa kila wiki. Ikumbukwe kwamba, wasomaji wanaondelea kupiga kura zao, pia wameandaliwa zawadi za kutosha kutoka kwa waandaaji, Gazeti la Ijumaa linalotoka kila siku ya Ijumaa. Wakali kumi wa Hip Hop waliotajwa kuwania Ufalme huo ni Profesa Jay, Fid Q, Kalapina, Langa, Black Rhino, Joe Makini, Chid Benz, Rado, Kala Jeremiah na Lord Eyez.


No comments: