Ray C: Apiga kolabo na sura mpya kwenye ‘Touch Me’
Kutoka ndani ya Jiji la Dar es Salaam, sista aliyejiajiri kupitia sanaa ya muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesema na safu hii kwamba, anavutiwa na sura mpya ambazo hivi sasa zimeikamata game ya Bongo Flava kwa ngoma zinazofanya vyema, kitu kilichomfanya apige nao kolabo kunako albamu yake mpya yenye jina la ‘Touch Me’, Hawa Mkombozi aliangusha naye maongezi.
Ray C alisema kwamba, wasanii kama Marlaw, Kassim na wengine walioibuka hivi karibuni anawakubali kwa sababu wameonesha uwezo wa hali ya juu katika game kiasi cha kusumbua akili za wakongwe na kwamba wote ameshirikiana nao kunako albamu hiyo bila kuvisahau vichwa kama Chid Benz na Wayre kutoka Kenya.
“Tayari wimbo uliobeba jina la albamu, ‘Touch Me’ nimeshaufanyia video katika nchi za Kenya na Australia, siku chache zijazo itakuwa hewani. Albamu ina nyimbo 10, zikiwemo Nihurumie wangu, My Love, Nalazimisha penzi, Moyo unaniuma na nyingine, nimefanya katika studio tofauti kama Big Time na 41 Records, “ alisema
Ray C.
****************************************************************
Jennifer Mgendi Kuwainua Wazanzibari kwa Injili
Mwanamuziki wa Injili nchini, Jennifer Mgendi ameiambia ShowBiz kwamba, anarajia kufanya ziara visiwani Zanzibar na kuwafunua wananchi wake kwa nyimbo takribani 20 za kumtukuza Mungu.
Msanii huyo amesema kuwa, zoezi hilo litakalofanyika ndani ya Ukumbi wa Golf, pia litamshirikisha Bahati Bukuku ambaye naye anafanya vizuri katika sanaa hiyo.
Jennifer ambaye hivi sasa anasikika zaidi na wimbo wenye jina la ‘mchimba mashimo’ alitamka kwamba, mbali na tamasha hilo yupo mbioni kutoka na filamu yenye jina la ‘Teke l a mama’.

King of Hip Hop
Langa: Nafanya Hip Hop Kimataifa, simhofii mtu
Bado tunaendelea kukudondoshea ishu tofauti kutoka kwa wakali wa Hip Hop wanaowania ufalme wa game hiyo kupitia shindano la Ijumaa King Of Hip Hop linaloendeshwa na gazeti hili. Leo ShowBiz ilipiga stori na Langa Kileo ‘Langa’ ambaye naye alijipa shavu kwamba ana uhakika wa kuwaliza wasanii wote waliopo kunako mpambano huo kwakuwa yeye yupo kimataifa zaidi, Eunice Macha na Chausiku Omary walisema naye.
Zaidi, mchizi alisema kuwa kinachompa jeuri ya kujitaja yeye ni wa kimataifa ni uwezo mkubwa alionao ndani ya game hiyo ikiwemo uwezo wa kuandaa mashahiri kwa muda mfupi na kujiamini anapokuwa stejini. “Uwezo wangu naweza kuulinganisha na wasanii wa nje kama Akon, Marehemu 2 Pac na wengine wengi. Lakini kwa Bongo sioni,” alisema Langa.
Aidha msanii huyo alisema: “Japo ninauhakika wa kuibuka na ushindi, bado nawaomba mashabiki wote wanaoshiriki katika zoezi la upigaji kura wawe makini, wasiwe na ubinafsi kwa sababu huo ni mpambano ambao mshindi wa kweli lazima apatikane”.
Mratibu wa Shindano hilo, Charles Mateso aliwataja wasanii wengine waliochaguliwa na mamia ya mashabiki kushiriki kunako shindano hilo kuwa ni Fid Q, Chid Benz, Kalapina, Profesa Jay, Kala Jeremiah, Rado, Johmakini, Lord Eyes na Black Rhino.
Mateso, aliwataka wasomaji kumchagua msanii wanayemuona anapaswa kutwaa taji hilo kwa njia ya sms, wakiandika neno HP halafu waache nafasi, wafuatishe jina la wanayemtaka awe Ijumaa King Of Hip Hop na kutuma kwenda namba 15551.
***********************************************************************

No comments:
Post a Comment