Friday, July 11, 2008

Jim Carrey ajiachia beach na nguo ya mkewe





Hivi karibuni staa maarufu wa muvi za vichekesho Marekani, Jim Carrey, aliwaacha watu midomo wazi baada ya kuhamishia sanaa yake ya vichekesho kunako sehemu ya kujirusha tena mbele ya mkewe, Jenny McCarthy.

Jim Carrey, ambaye alidondoka na mkewe katika ufukwe mmoja wa bahari uliopo Malibu, nchini humo, alifanya vituko vya ajabu na kuwafanya baadhi ya watu waliokuwepo ufukweni hapo kuangua vicheko. Mbali na yote aliyofanya kubwa zaidi lilikuwa ni lile ya kuchukua nguo ya kuogelea ya mkewe na kuivaa yeye kama anavyoonekana katika picha tofauti hapo juu.

Staa huyo wa filamu za vichekesho amejipatia mafanikio makubwa kupitia muvi kibao ikiwemo Mask.

No comments: