Monday, July 14, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Masai waipa shavu Bongo Ujerumani
Kundi la muziki wa asili, Masai Morani Dancer Group, linaloundwa na wabongo wenye asili ya kabila hilo ambalo liliwahi kufanya vyema kunako tamasha kubwa lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam kwa jina la Chrismas Festival, miaka kadhaa iliyopita, limeendelea kufanya maajabu hayo nchini Ujerumani na kuitangaza ile mbaya nchi yetu ya Tanzania.

Akichati za safu hii kwa njia ya mtandao wa computer (Internet), kiongozi wa kundi hilo, Jacob Paringo (Pichani juu) alisema kwamba, tangu wafike nchini humo wamefanikiwa kuitangaza vyema Tanzania, kwani mbali na kucheza ngoma za asili wameweza kuwashawishi raia wengi nchini humo kuvaa vitu vya asili ya kabila la Kimasai wanavyotengeneza.

“Tunashukuru kwamba kazi zetu zinakubalika sana, watu wanazipenda. Hivi karibuni nilipewa heshima na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani kutengeneza sanamu ya mnyama mmoja maarufu wa huku ambayo imewafurahisha watu wengi. Kwa kifupi ziara yetu huku ni ya mafanikio makubwa, tunatarajia kuwasili nchini Julai 16, mwaka huu” alisema Jacobo.

*****************************************
"Full Kujiachia"
Ray C ‘mtamu’kuliko Irene
Kupitia kona ya ‘Full Kujiachia’ ya gazeti la Ijumaa Wikienda, leo tunakupa matokeo, yaani maoni ya wasomaji ambao wiki iliyopita walitakiwa watutumie ujumbe mfupi (SMS) na kutuambia kwamba, endapo wangepata nafasi ya kujiachia na mmoja kati ya warembo hawa, Irene Uwoya, Ray C na Lisa Jensen wangemchagua nani na kwanini?

Ndani ya ‘meseji’ zaidi ya mia moja zilizotufikia, asilimia karibu 60 zimemtaja Ray C kuwa ndiye ana mvuto zaidi ya wengine, huku wakitoa sababu mbalimbali yaikiwemo mauno yake anapokuwa jukwaani na macho yenye ushawishi wa kumvutia karibu kila mwanaume.

“Ningemchagua Ray C kwasababu ana macho ya kimahaba, naweza kuuza bajaji yangu nikiwa naye,” alisema Calvin wa Ubungo, Dar es Salaam. Naye Rahim wa Sinza alisema kwamba. “Mimi ningemchagua Ray C kwasababu navutiwa na mikao yake ya kujiachia”.

Kwa upande mwingine Irene Uwoya amekamata nafasi ya pili baada ya kuibuka na asilimia 30, huku Lisa Jensen akiibuka na asilimia 10 ya maoni yote yaliyotumwa na wasomaji wa safu hii. Je, ni mastaa gani tutakuwa nao wiki ijayo kunako ‘Full Kujiachia? Usikose kuchungulia.
******************************************
King of HipHop Kalapina kujifanyia kampeni mikoani
Katika kile kinachoonesha kwamba amedhamilia kuibuka na taji la King Of Hip Hop, msanii Kalama Masoud ‘Kalapina’ na kundi zima la Kikosi cha Mizinga yupo katika ziara ndefu kwa ajili ya kujifanyia kampeni kwa mashabiki wake, huku wakiwahamasisha baadhi ya vijana kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya.

Akipiga stori na safu hii kwa njia ya simu kutoka Mkoani Mwanza, Kiongozi huyo wa Kikosi cha Mizinga alisema kwamba, bado anaamini kuwa endapo mashabiki hawataangalia sura ataibuka na ufalme huo kwani ana kila sifa inayomfanya aitwe King Of Hip Hop.

“Wengi ninaoshindana nao hapo wanafanya Bongo Flava, hawana mzuka wa Hip Hop ya ukweli kama mimi, hivyo sioni sababu ya kuukosa ubingwa huo,” alisema Kalapina ambaye akiwa na kundi lake Julai 25, mwaka huu watapiga bonge la shoo ndani ya Ukumbi wa City Cabana na kufuatiwa na CCM Kirumba, Mwanza, Julai 26.

Baada ya kutoka Mwanza, Kalapina na kundi lake wataelekea kunako mikoa mingine kwa ajili ya kuendeleza kampeni hizo, Hip Hop bila madawa inawezekana. Naye mratibu wa shindano la King Of Hip Hop, Charles Mateso amewataka mashabiki kuendelea kupiga kura wakimtaja mshiriki ambaye anastahili kuibuka na ushindi kwa kuandika neno HP waache nafasi kisha jina la msanii, halafu watume kwenda namba 15551, zoezi ambalo litaendelea mpaka mshindi atakapopatikana.
******************************************************

3 comments:

Anonymous said...

samahani kaka angu, hivi huyu kala pina ana jicho moja kama anavyoonekana au ni fashion tu????

Mrisho's Photography said...

Kala ni msanii tu, hana jicho bovu wala nini, ni fashion tu ya ki hip hop, si unajua tena mambo flani.... siku moja ntakuwekea picha yake halisi....thx!

Anonymous said...

asante kwa kunifahamisha, maana picha zake nying
naona yuko hivo kumbe ni fashion tu!
Tukopamoja kaka angu mpendwa