Friday, September 26, 2008

Ijumaa KIng of Hip Hop: Top 05



Kutoka ndani ya shindano la kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop, tunayofuraha kubwa ya kuwataja rasmi washiriki waliyofanikiwa kuingia katika tano bora, hatua ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa.

Kwa mujibu wa mratibu wa mpambano huo, Charles Mateso washiriki waliyopasua mpaka ‘Top 5’ ni Johmakini, Chid Benz, Fid Q, Kalapina na Profesa Jay ambao kwa pamoja wameingia katika hatua ya fainali itakayomtoa mshindi mmoja, yaani Ijumaa King Of Hip Hop.

“Tunawaomba wasomaji na wapenzi wa muziki wa Hip Hop waendelee kutuma kura zao wakituambia nani anastahili kuwa bingwa. Wanaandika neno HP (wanaacha nafasi) wanaandika jina la mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuwa mshindi, kisha watume kwenda namba 15551,” alisema Mateso.
***************

2 comments:

Anonymous said...

Mapozi mengine bwana, mvuto ni 0% kama huyo wa kwanza hapo juu, ndio pozi gani sasa.... kama kipofu??

Anonymous said...

Ni kweli, Huyo wa kwanza hapo juu, pozi lake halina MVUTO kabisaa... we Broo jaribu pozi lingine bwana hapo ujatoka shegaa!!

Kama vile ndiye aliyechukua T-SHIRT ya kaka MICHUZI... au nimekosea??? ndiye yeye.... mrudishie kaka MICHUZI T-shirt yake.... ntamwambia