Friday, October 17, 2008

IJUMAA SHOWBIZ

Manka Mushi
Irene Uwoya
Angela Lubala
Hadija
Sexiest Girl:Warembo 20 waliotajwa

Pichani juu ndiyo baadhi ya mastaa 20 wa kike waliotajwa kuingia ndani ya shindano la kumtafuta Mrembo wa Ijumaa mwenye mvuto zaidi wa kimahaba (Ijumaa Sexiest Girl) ambalo tayari limeanza kuwashtua mashabiki wengi ambao wamekuwa wakilifuatilia tangu lilipoanzishwa miaka miwili iliyopita.

Pamoja na ishirini hawa kutajwa, wanatakiwa warembo 12 tu, ambao wataingia kunako fainali kubwa ambayo itaanza rasmi hivi karibuni kupitia safu hii. Ili kuwapata 12 hao, wewe msomaji na mpenzi wa shindano hili tunaomba utuambie nani anastahili kuendelea kuwepo shindanoni? Tutumie ujumbe mfupi (SMS) kupitia namba zile zile, 0784-275 714, 0787- 110 173, ukitaja jina la mrembo uneyeona anastahili kubaki shindanoni. Maoni yako ni muhimu sana kwetu. Tuma sasa.


Prof. Jay kuwapotezea kina Lil Wayne Kongo
Katika kuhakikisha kwamba mchizi aliyekomaa kitambo katika game ya Muziki wa Kizazi, Kipya Joseph Haule a.k.a Profesa Jay anawafunika Lil Wayne na The Game, katika kinyang’anyiro cha Tuzo za MTV Afrika (MTV Africa Music Awards), kwa upande wa Mwanahip Hop Bora, MTV ikishirikiana na Kampuni ya Global Publishers inatararajia kumpeleka mkali huyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo kwa ajili ya kampeni za kuomba kura kwa mashabiki wa huko, Rebeka Bernard anatambaa nayo.

Akipiga stori na ShowBiz hivi karibuni Mwakilishi wa MTV nchini, Christine Mosha a.k.a Seven, alisema kwamba, kila mshiriki kunako shindano hilo ataenda katika nchi aliyopangiwa kwa ajili ya kuomba kura kwa mashabiki wa nchi husika.

“Zimechaguliwa nchi nne kwa ajili ya washiriki kwenda kufanya kampeni, kwa upande wa Jay amepangiwa Kongo. Tutakuwa naye bega kwa bega kwa ajili ya kumpa tafu mtu wetu,” alisema Seven.

Aidha aliongeza kwamba, wanaamini kampeni ya Prof. Jay itaenda vizuri kutokana na kukubalika kwake katika nchi nyingi za Afrika hivyo atakwenda sambamba na wapinzani wake Lil Wayne na The Game wa Marekani.

Mambo ndiyo yako hivyo, lakini kwa dodoso zaidi fuatilia vituo vya Redio Clouds FM na Kituo cha Luninga cha TBC.
***************

3 comments:

Anonymous said...

Huyo balozi wa Reds Angela lubala anafanya nini kwenye kinyang'anyiro cha mahaba tena? basi rudia hulo taji la pombe umeruka mkojo wakanyaga mavi.

Anonymous said...

Wee Lubala mbona husikii? umewashinda nini akina Deo na mkewe mambo ya muonekano wa mahaba na dini wapi na wapi nenda shule mama angela keshakufundisha mahaba ya Tanga nini?

Anonymous said...

Mrisho hizo picha tutazishindanishaje sasa? waweke wote wakiwa full. Mbona umempendelea Irene?