Monday, October 20, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ


Whitnes hajaambulia ziro Channel O
Msanii wa kike anayekomaa kunako game ya muziki wa Hip Hop, Whitness Kaijage hajaambulia ziro kama ulivyo wimbo wake, badala yake amedondoka Bongo na tuzo ya Channel O, kupitia video ya ngoma yake, ‘Ziro’ iliyomshirikisha Fareed Kubanda ‘Fid Q’ na kusema kuwa hafanyi muziki kwa ajili ya Tanzania tu, bali anataka Afrika nzima na baadhi ya nchi za mbali zaidi wamtambue.

Akipiga stori na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten mwishoni mwa wiki iliyopita msanii huyo ambaye pia ni ‘muhanga’ wa kundi la Wakilisha alisema kwamba anaamini ipo siku ndoto zake hizo zitatimia, kwani dalili za mafanikio tayari zimeshaanza kuonekana kupitia tuzo hiyo ambayo hutolewa na Kituo cha TV cha Channel O cha Afrika Kusini kila mwaka.

Hiyo inaonesha ni jinsi gani game ya muziki wa Bongo flava inavyozidi kubamba Afrika, kwani mwaka jana mchizi kutoka TMK Halisi, Juma Kassim ‘Nature’ alirudi kutoka Afrika Kusini na tuzo ya Channel O baada ya video ya wimbo wake, Mugambo kufanya vyema. Sisi kama Abby Cool & MC George Over The Weekend tunatoa Big Up za kumwaga kwa Whitness, aendelee kukomaa zaidi katika game.

MTV Africa Awards:PROF. JAY YUKO FULL KUJIAMINI
Wakati siku za utoaji Tuzo za MTV Afrika (MTV Africa Music Awards) zitakazofanyika nchini Ghana hivi karibuni zikiwa zinazidi kusogea kwa kasi, muhusika wa shughuli hiyo anayeiwakilisha Bongo, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ anazidi kuonesha ‘komfidensi’ za kutosha kwa kutamka kwamba mwaka huu ni wake, Rebeka Bernard anashuka nayo.

Akiwa anawania tuzo moja na wakali wa Marekani, Lil Wayne na The Game, Jay alisema kuwa watu wasishangae pale atakapoibuka ‘Best Hip Hop’ na kuwamwaga wasanii hao kwasababu ngona anazofanya zina ujumbe na mafunzo ya kutosha kwa jamii kitu ambacho kinamfanya asiwe na wasi wasi kwa hilo.

“Nafahamu kwamba wasanii ninaopambana nao katika tuzo hiyo ya mwana Hip Hop bora ni wakali, lakini naamini mashabiki wangu na wapenzi wa Hip Hop Bongo hawataniangusha kwasababu ushindi wangu ni wa nchi nzima,” alisema Jay.

Mbali na Lil Wayne na The Game, ndani ya kategori hiyo, Jay pia atakutana na wasanii wengine kama 9ice kutoka Nigeria na HHP wa Afrika Kusini. Ishu zaidi kuhusiana na tuzo hizo za MTV endelea kufuatilia katika magazeti yanayotolewa na Kampuni ya Global Publisher na kusikiliza Radio Clouds FM, bila kusahau Kituo cha Runinga cha TBC 1.
Street Version

MASANJAa.k.a Mkoboaji
Hivi karibuni msanii wa Kundi la Comedy Original, Masanja (pichani juu) ambaye sasa anajiita Mkoboaji, alijichanganya kinyemela ndani ya Viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam ulipokuwa ukifanyika mkutano wa Chama cha Wananchi, CUF. kamera ya Street Version ilimbamba laivu.
*********************************************************
SHAKIRA: Alijiachia na wanaume watatu tu!
Inakuwaje wapenzi wa safu hii, ‘Ebwana Dah!’, wale wasomaji waliotutumia sms wakitaka kufahamu mwanamuziki Shakira aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume gani, leo ndiyo siku yao ya ‘kujilamba’.

Ishu ni kwamba, binti huyo Shakira Isabel Mebarak Ripolli a.k.a Shakira mwenye umri wa miaka 31 sasa anaonekana kuwa bonge la mjanja, kwani tangu alipoukaribisha ustaa amewahi kujiachia na wanaume watatu tu ambao ni Osvaldo Rios, Wyclef Jean aliyefanya naye kolabo ya wimbo ‘Hips Dont Lie’ na Antonio de la Rua ambaye anatanua naye hadi hii leo.

Kwa Osvaldo Rios na Antonio de la Rua inaweza isiwe ishu sana kwa mashabiki wa mrembo huyo aliyezaliwa February 2, 1977, Barranquilla, Colombia, lakini kwa Wyclef inaweza ikawashangaza mashabiki wengi na huenda wasiamini kama kweli mchizi aliwahi kujiachia na mtoto huyo, bingwa wa mauno awapo stejini kwani walidhani urafiki wao uliishia kwenye kolabo ya Hips Dont Lie tu.

No comments: