Hakuna kitu kibaya kwa mgonjwa kama kula vyakula ambavyo huongeza tatizo alilonalo bila kujijua. Kwa kuwa tunaamini kwamba, jinsi tulivyo tunatokana na tunavyokula, basi kupona au kuendelea kuugua nako kutategemea sana vyakula tutakavyokula.
Vyakula viko vya aina mbalimbali na kila kimoja kina umuhimu wake katika mwili wa binadamu. Lakini mtu ukishakuwa mgonjwa, hasa wa maradhi sugu kama vile presha, kisukari, ukimwi, n.k, ni lazima ujue vyakula gani unapaswa kula na vyakula gani unapaswa kuviepuka.
Leo tunaangalia vyakula anavyopaswa kuvila ama kuviepuka mgonjwa wa shinikizo la juu la damu (High Blood Pressure). Kama inavyojulikana, maradhi haya hutokana na staili ya maisha anayoishi mtu, vivyo hivyo hata udhibiti wake utategemea na atakavyoishi.
NYAMA NA MAYAI
Nyama na mayai ni adui mkubwa wa mgonjwa wa presha. Ni wagonjwa wangapi wanafahamu kwamba vyakula hivi ni hatari kwa maisha yao na wakaacha kabisa kuvitumia? Naamini ni wachache sana wanaolifahamu hili na kulizingatia, hasa ukizingatia utamu wa vyakula hivyo.
Inaelezwa kuwa katika vyakula ambavyo mgonjwa wa presha akivila huchangia kupandisha presha ni mayai na nyama, hasa ile itokanayo na ng’ombe, mbuzi, nguruwe na nyingine za jamii hiyo.
ZINGATIA VYAKULA HIVI
Ukisha kuwa mgonjwa wa presha, ulaji wa vyakula vitokanavyo na nafaka halisi, matunda na mboga za majani, linakuwa suala la lazima na siyo hiyari. Mgonjwa wa presha anashauriwa kula zaidi vyakula hivyo na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi, ikiwemo nyama kama ilivyoolezwa awali.
Katika orodha ndefu ya matunda anayopaswa mgonjwa kula na kupata nafuu, ni pamoja na hii ifutayao, ambayo huweza kutumika pia kama tiba, kwani matunda haya yameonekana kuwa na virutubisho vingi zaidi vinavyoweza kudhibiti presha:
Vitunguu saumu
Kula vitunguu saumu kwa wingi, hutoa nafuu kubwa kwa mgonjwa. Unaweza kula punje mbili hadi tatu kwa siku na kuchanganya kwenye mboga pia.
Limau
Pia penda kula limau mara kwa mara, nalo ni miongoni mwa matunda yanayotoa nafuu kwa mgonjwa wa presha. Limau lina Vitamin P ambayo utaipata kwa kunywa juisi yake au nyama na maganda yake.
Zabibu mbivu
Zabibu nazo zimeorodheshwa miongoni mwa matunda anayotakiwa kula mgonjwa wa presha ili kupata nafuu, nayo yana vitamin P ambayo huzuia kuziba kwa mishipa ya damu.
Tikiti maji
Tikitimaji nalo ni miongoni mwa matunda anayopaswa kula mgonjwa wa presha. Halikadhalika, mbegu za tikiti maji zinaweza kutengenezwa na kuliwa kama dawa inayoweza kumpa nafuu kubwa mgonjwa. Kausha mbegu zake, kisha zikaange, ziliwe mara kwa mara kama karanga.
Mchele
Mchele una kiwango kidogo cha ‘fat’ na pia una kiwango kidogo cha ‘kolestrol’, hivyo kukifanya kuwa chakula bora kwa mgonjwa wa presha. Hivyo wali ni sawa kuliwa na mgonjwa wa presha, hasa ukipata ule mchele usioondolewa virutubisho vyake (brown rice).
Viazi vitamu
Viazi vitamu, hasa vile vya kupika na maganda yake, vinafaa sana kuliwa na mgonjwa wa presha kwani vina madini mengi ya ‘potasiamu’ na havina madini chumvi.
Juisi ya mboga majani
Ulaji wa mchanganyiko wa juisi ya mboga, hasa karoti na mchicha (spinach) ni mzuri sana kwa mgonjwa wa presha, huweza kutumika pia kama tiba. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili au tatu.
Kwa kuzingatia ulaji wa vyakula vilivyoainishwa hapo juu na kufanya mazoezi mara kwa mara, mgonjwa wa presha anaweza asisumbuliwe kabisa na tatizo hilo na kujihisi kupona hata bila kutumia dawa. Hata hivyo, hilo linawezekana tu iwapo utajitambua mapema na kuanza kuchukua hatua za ulaji sahihi wa vyakula sasa na siyo baadaye!

12 comments:
Thanks for your dietory publishing notes
Its realy opening minds
Thank u once agn
Asante
Yaan leo umeokoa maisha yangu maana nimeacha kula vyakula vya wangu lakini nakula sana mayai na samaki niliambia ndio chakula sahihi kumbe mayai nakosea..sasa vipi kuhusu samaki naweza kuendelea kutumia au niache pia
Asante sana
Kumbe nyama na Mayai sio chakula kizuri kwa mwenye BP ya kupanda??
Mimi mwenyewe nina tatizo la presha..ya kupanda.
Asante kwa makala hyo nimepata kitu
Sina namna, nalazimika kuacha kula mayai na nyama maana hali si shwari
Vipi kuhusu chumvi
WhatsApp +255 679 282 874 kwa matibabu sahihi ya tatizo lako karibu saaaana

Hakika ugonjwa huu ni tishio ila hatuna budi kuijal Afya kwa kuzingatia ulaj wetu
Post a Comment