Friday, February 12, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!


Bongo Flava artists
THT Dancers
Ray C
Barnaba
Bi Kidude
Jide

Tamasha kubwa la Malaria kesho
Mpango mzima wiki hii kunako ishu ya burudani utakuwa ni pale ndani ya Viwanja wa Readers Club, Dar es Salaam litakapofanyika tamasha kubwa lenye lengo la kukemea vikali ugonjwa unaoongoza kuua watu wengi zaidi duniani, Malaria, lililopewa jina la “Zinduka, Maralia haikubaliki”.

Tamasha hilo litakalofanyika kesho Jumamosi, ambalo litawakusanya maelfu ya Watanzania wanaotarajiwa kuhudhuwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye atakuwa mgeni rasmi kwenye ishu hiyo itakayopambwa na wasanii kibao wanaofanya vema katika sanaa zao akiwemo Rehema Chalamila a.k.a Ray C.

Akipiga stori na ShowBiz juzi, jijini Dar ,Ray C alisema kwamba tangu kampeni hizo za kupambana na Maralia zilipoanza baada ya kuzinduliwa na Rais Kikwete hivi karibuni amejifunza mambo kibao ikiwemo jinsi mama mjamzito anavyoweza kujifungua mtoto mwenye mtindio wa ubongo au kupoteza maisha yeye na mwanaye kwa ugon jwa huo.

“Zamani nilikuwa nadhani ni ugonjwa wa kawaida tu, ukiugua unakunywa dawa mchezo umekwisha, kumbe siyo. Kampeni hizo zimenipa changamoto na naamini nitakuwa mama bora”, alisema Ray C ambaye katika shoo hiyo ataungana na wasanii kama Frola Mbasha, Lady Jaydee, Chegge, Madee, Prof. Jay , Marlaw na Johmakini

Vile vile steji itaendelea kupambwa na Ngwea, Barnaba, Pipi, Bi. Kidude, madensa kutoka THT, Kidumu kutoka Burundi na wengine kibao. Kwa kifupi itakuwa ni siku ya kipekee kwa wapenzi wa burudani watakaohudhuria kesho.

Mchizi mwingine aliyepiga stori na safu hii ni msanii Barnabas a.k.a Barnaba Boy kutoka THT ambaye alisema kuwa kampeni hizi zimemtoa ‘ujinga’ kuhusiana na ugonjwa wa Maralia kwani amejifunza mambo mengi ikiwemo umuhimu wa kutumia chandarua kwa kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wakilala bila Chandarua lakini baada ya kupata somo na kufahamu kuwa uonjwa huo unaua kwa haraka ameamua kubadilika na ataendelea kufanya hivyo hata atakapokuwa na familia yake.

Kwa upande wao, Clouds Entertainment ambao ndiyo wanasimamia kwa karibu shughuli hiyo kubwa walisema na safu hii kwamba shoo hiyo ambayo itafundisha na kuburudisha itaanza majira ya saa moja usiku hadi saa sita, huku mashabiki watakaofurika siku hiyo wakichangia shilingi elfu tatu kila mmoja. Ebwana ee, siyo ishu ya kukosa sisi pia tutakuwepo pande hizo kwa ajili ya kujifunza mambo mengi kuhusiana na ugonjwa wa Maralia.

compiled by mc george

1 comment:

Anonymous said...

REY C. NAYE?