Friday, February 12, 2010

Koleta kubeba mikoba ya Maimartha EATV?

Maimatha

Minong’ono iliyopo mitaani hivi sasa ni kwamba huenda staa wa kike katika Kiwanda cha Filamu Bongo Coletha Raymond a.k.a Koleta akachukua mikoba ya Mtangazaji ‘sumu’ nchini Maimatha Jesse aliyetimkia katika Kituo cha luninga cha TBC 1 na kuacha kipindi chake cha Afro Beat kikiwa hakina mtu maalum wa kukiendesha.

Hisia hizo zimeibuka baada ya msanii huyo kuonekana akitangaza Kipindi cha Afro Beat hivi karibuni na kurudiwa mara kadhaa na kituo hicho, huku akimwagiwa sifa kuwa alikamua vizuri sana.

Baada ya Mai wa Jesse kuhamia TBC 1 kipindi hicho kimekuwa hakina mtangazaji maalum, lakini nyepesi nyepesi kutoka kwa chanzo kimoja kilichopo Channel 5 zinasema kwamba muongozaji wa kipindi hicho, Josiah Murungu akishirikiana na Musa wamekuwa wakiendesha zoezi la kumsaka mrithi wa Mai kimya kimya.

Koleta alipopigiwa simu ili aeleze kama amepata ajira katika kituo hicho, alisema hana taarifa zozote, lakini ni kweli alitangaza kipindi hicho kwa siku moja.
“Sijui chochote kaka yangu, niliombwa na akina Josh nitangaze, nikawaambia wanipe muda nijiandae wakasema watanipa maelekezo mafupi kabla ya kurekodi, nilipowakubalia, wakanielekeza kisha nikarekodi,” alisema Koleta.

Alipoulizwa kama alikuwa na taarifa za shindano la kumsaka mrithi wa Mai, alisema: “Sijaambiwa kama nashindana, kwa ujumla sijui chochote.”

1 comment:

Anonymous said...

Mh1 huyu niliyemuona jana Gymkhana kaongozana na watoto si rizki???