Monday, February 15, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

A-z Tamasha la Malaria
Usiku wa kuamkia jana (Jumapili) ulikuwa ni wa burudani na elimu ndani ya Viwanja vya Leaders Club vilivyopo pande za Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya kuungana na Rais Jakaya Kikwete katika lile tamasha kubwa la kupiga vita ugonjwa wa Malaria lililokwenda kwa jina la Zinduka, Malaria haikubaliki.

Tamasha hilo lililojaza nyomi lisilo la kawaida lilianza mishale ya saa I:30 ambapo watu walimimika kwa wingi huku ulinzi na usalama wa eneo hilo ukionekana kuwa wa kiwango cha juu kutokana na kuwepo kwa askari wa usalama wa raia, mbwa, mabaunsa, walinzi kutoka kampuni binafsi za ulinzi na watu wa Usalama wa Taifa.

Majira ya 2:30 usiku ndipo walipoanza kutia maguu wanene kutoka serikalini wakiwemo Rais JK, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Margareth Sitta, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na wengineo.

Mpango mzima wa burudani ulianza mida ya saa 3:20 usiku na wa kwanza kutoa shoo walikuwa ni wasanii kutoka Tanzania House of Talent (THT) wakifuatiwa na wasanii wengine kama vile Marlow, Profesa Jay, Jide, Ray C, Maunda Zorro, Banana Zorro na B-Band, Mangwea, Diamond, Chegge, Mheshimiwa Temba, Johmakini, Mwasiti, Kidumu kutoka Burundi na Bi. Kidude.

Licha ya burudani zilizotolewa na wasanii hao, pia watu waliohudhuria tamasha hilo walipata fursa ya kupata elimu juu ya njia mbalimbali za kujikinga na ugonjwa hatari wa Malaria kutoka kwenye hotuba zilizotolewa na viongozi mbalimbali na nyimbo za wasanii waliopata nafasi ya kufanya kweli jukwaani usiku huo.
Shughuli nzima iliisha majira ya saa 7:00 usiku.
***********************************
Stan Boi akiwa na Omario

Stan Boi akiwa na Chamillionaire

Stan Boi Underground wa Upanga sasa ni one class na kina Omarion, Chamillionaire
Underground aliyekuwa akifanya chorus za ukweli kwenye nyimbo za memba wa crew marehemu ya East Coast Team, Stan Boi kwa sasa yupo level nyingine kimuziki na sasa anachangia jukwaa moja huko kiwanja na wakali kama Omarion, Chamillionaire na wengine kibao.

Stan Boi ambaye alivuna jina kiduchu Bongo, pale sauti yake iliposikika kwenye wimbo Itikadi ambao ni mali ya Amiri Jeshi Mkuu wa ECT, Gwamaka Kaihula ‘GK’, alitimba kiwanja days, months and few years ago kwa ajili ya kupiga kitabu lakini as you know kipaji ni kipaji, wakali wa Mtoni wakamuona na sasa anakwea matawi ya juu.

Iko hivi, kwa sasa Stan Boi anafanya R&B ya ukweli nchini Marekani, na amekuwa akifanya maonesho mbalimbali na wakali kama Omarion, Jaicko, Se Trill, LP, Ester Dean, Sippi, C-Rider, Chamillionaire na Huriccane.
**************************

Bebe Cool jino kwa jino na Serikali ya Museven
Mkali wa muziki wa kizazi Uganda, Moses Ssali a.k.a Bebe Cool ameamua kula sahani moja na Serikali ya Rais Yower Kaguta Museveni, Uganda na tayari amefungua mashtaka mahakamani dhidi ya jeshi la polisi.

Msingi wa madai ya Bebe Cool ni kuwa, polisi nchini Uganda wanahusika moja kwa moja na tukio la yeye akiwa na walinzi wake kupigwa risasi, walipokuwa kwenye onesho moja la muziki mjini Kampala.

Katika madai hayo, Bebe Cool analitaka Jeshi la Polisi Uganda, kumlipa shilingi milioni 800 za Uganda kama fidia kutokana na hasara pamoja na majeraha waliyoyapata.

Bebe Cool pamoja na walinzi wake walipigwa risasi hivi karibuni baada ya kuzuka vurugu baina yao na polisi na wakili wake ameandika kuwa msanii huyo anategemea maonesho ya muziki kuweza kuishi lakini kutokana na majeraha aliyoyapata, anaweza kukaa muda mrefu bila kufanya kazi itakayomuingizia kipato.
*************

Rasheeda aamua kusaka njemba ya kumtuliza!
Safu inayochungulia harakati za kimapenzi kwa mastaa wa kiwanja ipo hewani tena, Ebwana Dah! Leo ni ‘mimba’ moja na Malkia wa Crunk, Rasheeda.

Kioja ni kwamba ile tovuti yetu ambayo hudili na news about nani kamrukia nani na lini haijaweza kung’amua chochote kwa Rasheeda, lakini uchokonozi wa Ebwana Dah! Umegundua tofauti.

Katika upekuzi wa safu hii, ndani ya tovuti moja ya kiwanja, Rasheeda ametangaza kusaka mwanaume sahihi wa maisha yake baada ya huko nyuma kuhangaika na wengi bila mafanikio.

Anasema: “Jina langu ni Rasheeda Hinton, nina umri wa miaka 26, napenda kusoma, kuongea kwa simu na kufanya shopingi… na wakati mwingine napenda kutulia peke yangu.

“Kwa sasa natafuta mwanaume sahihi, usinitafsiri vingine lakini nimewahi kujirusha na wanaume wengi lakini huzuni ni kwamba sikupata mtu sahihi. Nataka mtu ambaye ni muelewa, ana akili, mwenye kazi yake, pia aliye na muonekano bomba.”
**************************


No comments: