Sunday, June 7, 2009

MUNGU NDIYE MUWEZA WA KILA JAMBO!!



Wameungana vichwani, Mmoja mwanamuziki , mwingine ameajiriwa hospitali

Kuna vitu vingine inabidi uvione ndio uamini kuwa ni vya kweli, kama hawa mapacha walioungana kichwani tu huku kila mmoja akiwa na viungo vyake vingine . kingine cha ajabu ni kwamba wakati pacha mmoja ni mwanamuziki pacha mwingine anafanya kazi hospitalini.

Hao ni Lori na Reba Schappell ambao wanaaminika kuwa ni mapacha wa kike walioungana ambao wameishi muda mrefu kuliko wote duniani .

Lori na Reba wanaishi Reading, Pennsylvania, nchini Marekani na walizaliwa mwaka 1961 na kulelewa kwenye nyumba ya watu wasiojiweza hadi walipofikisha umri wa miaka 24.

Mapacha hao wanapendelea vitu tofauti, Reba anaendesha maisha yake kama mwanamuziki , Lori anafanya kazi hospitali kwenye kitengo cha mashine za kufulia nguo.

Kutokana na kuwa mwimbaji hodari wa muziki wa Country, Reba aliwahi kujinyakulia tuzo ya mwanamuziki anayechipukia wa muziki wa Country mwaka 1997 na amewahi kutumbuiza nje ya Marekani kama vile Ujerumani na Japani.

Reba anatumia kiti alichokitengeneza mwenyewe ili kumsaidia kusogea kutoka sehemu majo hadi nyingine .

Lori kwa upande wake humbidi apunguze muda wake wa kazi yake ya hospitali ili pacha wake Reba aweze kuhudhuria matamasha yake ya muziki .

Mapacha hao wamekuwa wakitokea kwenye vipindi mbalimbali vya televisheni kwa ajili ya mahojiano na waliwahi kutengenezewa kipindi kinachoeleza maisha yao .

“Usifikiri tuna maisha ya tabu mpaka tukutamkie hivyo,” alisema Lori akiwaambia watu ambao walikuwa wakiona maisha yao ni ya tabu sana.

HAKIKA MUNGU NI MUWEZA WA KILA JAMBO NA HATUNA BUDI KUMSHUKURU KWA HIVI TULIVYO!!

1 comment:

shamim a.k.a Zeze said...

HAKIKA !! YEYE NDIYE...IMAGINE HAWA WAMEKUA KUFIKIA HAPO HIVYO WALIVYO...GOD IS GREAT!!