Wednesday, July 29, 2009

TANZANIA HAKUNA WASANII

Nashawishika kusema kwamba Tanzania hakuna wasanii kama wengi wetu wanavyodhani bali tuna wajanjawajanja wanaojiita wasanii. Mtazamo wangu huu utasababisaha baadhi ya watu kudai kwamba mimi sio mzalendo .

Tanzania hakuna wafinyanzi wala wachongaji,je wajua kwamba mmiliki wa ukumbi wa new world cinema alitafuta watu wanaoweza kuchonga sura ya mwalimu nyerere ,wale wanaojiita wachongaji wote waliikosea sura ya mwalimu,je unajua sanamu ya mwalimu nyerere mwanza iliwahi kukataliwa na mkuu wa mkoa kutokana na sura yake kukosewa,angalau sanamu ya nyerere ya dodoma pale nyerere square sijui nani aliichonga,

ukienda ulaya miji yote imejaa masanamu ya wanyama na watu mashuhuri iliyochongwa kiustadi hali ni tofauti kwa tanzania jiji la dar les salaam lina sanamu mbili tu ya nyerere na ile ya askari pale samora ,sanamu ni sehemu ya historia.

Tuje kwenye sanaa ya uigizaji,huko ndio kuna wababaishaji waliokubuhu wacheza filamu wananakili kazi za kinaijeria na kuzibadilisha majina na mazingira na lugha alafu mtu anajiita msanii,wasanii hawafuati script wanaongea maneno yanayowatoka kichwani kwao. Wasanii hawaangalii hali halisi ya maisha ya kitanzania eti unakuta wanaonyesha kijana wa miaka ishirini anamiliki hekalu na magari ya kifahari,ni watanzania wangapi wanaishi maisha hayo.

Sitaki kuongelea kwenye ubora kwa sababu nitkosa mpaka kesho.

Hata wachekeshaji(comedians) hakuna ,komedi orijino ni kikundi cha wajanja wajanja futuhi ndio kabisa wanahitaji msaada mkubwa sana kuweza kumchekesha mtu kama muhogo mchungu alivyowahi kusema kwamba ni vigumu kwa wasanii wa kibongo kumchekesha mtu mwenye uchungu wa kuibiwa simu yake mtaa wa kongo .

Tukija kwenye Muziki ndio hakuna kitu je wajua kwamba wasanii wengi wa kitanzania wanakwapua kazi za nje ,orodha ni ndefu sana TID ,kila mtu najua kwamba wimbo wake wa nyota yangu ameukopi Angola ,Mwanafalsafa anayehishimika na wasiomjua ananakili nyimbo za mwanamziki wa marekani ,wimbo kama ingekuwa vipi amenakili wimbo uitwao what if, mabinti amenakili wimbo uitwao perfect bitch zote za Fredro Starr list ya nyimbo alizonakili ni nyingi sana,

Banana zorro na wimbo wake wa nzela amenakili kwa Oliver Mtukuzi,Mr Blue wimbo wake wa tabasamu kanakili kwa Riyana,FM Academia hao ndio wamekubuhu asilimia tisini ya nyimbo zao wameiba Congo,Myalu nae aliiba wimbo wa Ginuwine wa same OG akauita sitobadilika.

Orodha ni ndefu cha kuchekesha wasanii hao hao ndio wanaolilia haki iliki ya nyimbo zao wakati wao ndio vinara wa kukwapua kazi za wenzao pasipo kufuata utaratibu,lazimaieleweke kunakili kazi ya mwenzako sio kosa cha msingi ni kufuata taratibu,

Kumbe ndio maana mashabiki wa soka wa Tanzania waliamua kushabikia timu za majuu kwa sababu Taifa Stars inashinda mechi za kirafiki na kufungwa za ushindani japo ni wazalendo .

I humbly submit - Clement Togo.


6 comments:

Anonymous said...

Habari kaka Mrisho!
Kwanza ni kweli hakuna wasaniii kabisa kwetu wababaishaji tuu wizi mtupu kazi kuimba mapenzi tuuu.


Halafu leo umejitahidi kutoa mada ya chakula j5 siku ingine unafika mpaka ijumaa jaman.

Anonymous said...

labda umesahau hadi kwa vionngozi wetu napo hakuna kitu cjui hii tanzania ya leo inapoenda tuombe Mungu kila siku yasije kutupata yaliyowapata majirani zetu, vita vya wenyewe kwa wenyewe maana siku hz mtu huwezi kuwa na hela kama cio kiongozi. Na uongozi wa siku hz ni wa kunua kwa hiyo hapo hakuna haki mdau hongera sana kwa kutoa lilo moyonin mwako mimi kila cku kazi humu ni kumkosoa mtu anayeidharau bongo ila ka hili nakupa 100%

PM said...

True kabisa! Nchi hii inakoelekea, mmh Mola atuepushe. Maana siku si nyingi watu tutachoka, na kitakachofata hapo......!

Anonymous said...

Naipenda tanzania lakini lazima niseme kuwa tanzania HAKUNA HESHIMA.Watanzania tunahulka na tabia za kipekee zinazoshehenezwa na WIZI(USANII),WIVU,UVIVU na UBINAFSI unaorudisha nyuma maendeleo.Tabia hizi zimepelekea wawekezaji wa nje nao waende sambamba na hali hii pindi wanapoingia katika ardhi hii ya TZ.Mwanzoni mwa miaka ile nilomaliza masomo yangu pale Mlimani nilipata tabu sana kupata kazi ,kila nilipoandika barua ya kazi matokeo yalipokuja hayakua mazuri.KUJUANA NA KUSHIKANA MIKONO,katika Tanzania nilijifgunza kuwa haikujalisha una NINI bali UNAMJUA NANI.nikasema NCHI HII HAINA ADABU.
Nikaja huku kwenye ustaarabu,nikayaona mengi.nikajifunza mengi.USTAARABU ndio msingi wa maisha ya UGHAIBUNI.RUSHWA,UKANDAMIZAJI,UONEZI,WIZI na ubabaishaji huku ni mwiko.HUDUMA ni nzuri ktk kila sehemu unayoenda kuanzia hospitali hadi AIRPORT.
Tanzania AIRPORT ni mara ngapi USANII unafanyika hapo.
watu wa ushuru ni usanii mtupu.

Kwa kifupi USANII UPO katika damu ya watanzania ukinijumlisha na MIMI.

Asante.

Anonymous said...

Hapo hata sikatai Tanzania wizi ni mwingi wasanii wa maigizo wana ana copy sript zote kutoka katika filamu za kinaigeria.

Umeongea kweli kabisa

Anonymous said...

Ni kweli kabisa mie nakubaliana na huyu mwandishi kuhusu ubabaishaji wa wasanii wa bongo. Ila mimi wanaonikera zaidi ni hao wanaojiita mastaa wa kuigiza filamu. Jamani wanakera sio siri!!! Filamu zote za bongo ambazo mie nishaziona zote zimekopiwa toka Nigeria, halafu hapo hapo wengine wanadiriki hata kujiita majina makubwa kama "THE GREAT kanumba wakati kazi yao kuiga tu, Kwa kweli inakera saana na tena inatia hasira!!!!