Friday, July 31, 2009

TUSIWALAUMU SANA!

Ndugu

Wakati mwingine Tusiwe Tunalaumu tu vitu mara kwa mara , wewe
unayesema wasanii sio wabunifu umefanya nini kuwa mbunifu katika
shuguli zako wewe mwenyewe ? hiyo ni moja je umefanya nini kuhakikisha
unasadia japo kidogo kitu katika sanaa hiyo husika ? kama unadownload
miziki yao bure kwenye mitandao , kama umejaza miziki ya bure katika
computer yako na unacopy bandia za cd za wanamuziki au wasanii hao
halafu uje kusema wamelaaniwa wewe ndio umelaaniwa wa kwanza kwa
kudidimiza maendeleo ya wengine , hapa kila mmoja anyooshe kidole
aseme hiyo miziki iliyokuwa katika computer yako au flashdisk kama
kanunua utakuta hakuna wachache sana labda wale wa nje ambao kwa namna
moja sheria za huko zinawabana ingawa wakija hapa wanabeba miziki hiyo
kwa kiasi kikubwa na kwenda kuuza huko kwa bei haramu .

Pamoja na kulaumu wetu kwa sasa sanaa inazidi kukua ingawa sio kwa
spidi ya kutisha kama wengine wanavyotaka iwe , huko tunaweza kufika
kama sisi wenyewe watumiaji wa sanaa hizo tukiamua kwa moyo mmoja na
kuwa wazalendo kwa kutumia vyema kazi hizi za wasanii hawa .
YONA MARO

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Asante Yona Maro kwa maoni yako japo sina hakika kama ni ya kujenga wasanii maana "unafukia" mapungufu yao. Nimesoma maandishi kuhusu TANZANIA HAKUNA WASANII na nakubaliana na mengi ya yaliyosemwa. Mimi ni mmoja wa wale ambao wamekuwa wakiwaeleza ukweli wasanii (naamini hii inaweza kuchukuliwa kama kulaumu) hasa kwa kutokuwa wabunifu katika kazi zao. Kama umesoma maandishi ya wale waijuao sanaa halisi utakubali kuwa sanaa ya Tanzania inaharibiwa na wenye uchu na upungufu wa ubunifu na heshima katika sanaa. Ntakupa mfano wa mmoja wa watu walioianzisha hii Bongo Flava na ambao amekuwa nayo na anaendelea kuiandikia na kuichambua japo anafanya kazi na kuishi nchi yenye muziki wa aina hiyo iigwayo nyumbani. Namzungumzia MIKE MHAGAMA na waweza kumsoma katika makala yake hapa http://pesambili.blogspot.com/2009/07/ushauri-wa-bure-kwa-wanamuziki-wa.html na ukiifuatilia utaona aliyoandika na utaona links za maandishi yangu kuhusu Muziki na sanaa ya Tanzania. Siamini kuwa unastahili kukaa kimya pale ambapo unaamini hawafanyi vema na mimi sitafanya hivyo. Kutowaeleza ukweli ndio kuwadidimiza. Baadhi ya wasanii wanasikitisha na niseme wengine WANATIA KINYAA na wala hawastahili kuwemo katika muziki. Tatizo kubwa ni kuwa hakuna "chujio" linaloweza kuwatenganisha wenye kipaji, juhudi na maadili na wale ambao wanasaka maisha kupitia uimbaji. Binafsi sina la kusema kuhusu kazi zangu kwani NAJUA nina ubunifu na inapotokea nikaonesha upungufu katika hilo, niko tayari kuelezwa. Na lazima utambue kuwa KUPOKEA USHAURI ni kati ya yaliyo muhimu kwa ukuaji wa kila mmoja.
Yona umeuliza "je umefanya nini kuhakikisha unasadia japo kidogo kitu katika sanaa hiyo husika ?" Well, msaada ninaoweza kuwapa ni kuwakosoa. Kama una tatizo nalo nadhani wewe ndiye uwadidimizaye.