Monday, August 10, 2009

Hatimaye Michael Jackson Azikwa


Hatimaye mwili wa mfalme wa muziki Pop, Michael Jackson aliyefariki juni 25 mwaka huu umepumzishwa kwenye nyumba yake milele.Mwili wa Michael Jackson ambaye alifariki juni 25 mwaka huu, hatimaye umepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huku familia yake ikikanusha madai ya rafiki yake wa karibu Mark Lester ambaye alidai kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa kike wa Michael Jackson, Paris. Familia ya Michael Jackson ilisubiri wiki kadhaa kabla ya kuamua kuuzika mwili wake baada ya ubongo wake kuchukuliwa kwaajili ya uchunguzi zaidi juu ya kifo chake. Ubongo wake ulirudishwa kwenye mwili wake wiki iliyopita. Michael Jackson alizikwa kwenye makaburi ya Forest Lawn Cemetery yaliyopo Hollywood Hills, huku mazishi yake yakifanyika kimya kimya na kuhudhuriwa na familia yake pekee. Hakuna shabiki yoyote wa Michael Jackson aliyealikwa kwenye mazishi hayo na familia yake ilifanya mazishi hayo kwa siri kwa kuhofia maelfu ya mashabiki wake watatembelea makaburi hayo na kusababisha hali ya usalama wa kaburi lake kuwa mashakani. zaidi: nifahamishe.com