Sunday, August 30, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Sara Kaisi 'Shaa'
AY kupimana ubavu na Jigga, Shaa naye kuumana na mastaa kibao wa nje

Stadi wa Bongo Flava mwenye heshima ya kutosha, Ambwene Yesaya ‘AY’ anaona mzuka kupimana ubavu na mtu mzima Sean Cutter a.k.a Jay Z au Jigga.

Kama haujainyaka hii ni kuwa AY, amependekezwa kuwania Tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop katika Tuzo za MTV Africa Music Awards. Katika category hiyo, AY anakamuana na nominees wengine kama Jay-Z, Kanye West wa Marekani, MI wa Nigeria na Zulu Boy wa Bondeni.

AY alisema kuwa anaona mzuka bin poa kupambana na Jigga pamoja na Kanye kwa sababu kitendo cha MTV kuwapambanisha kwenye category moja maana yake viwango vinalingana. “Hata nikishindwa, bado heshima itabaki kwangu, pia nimeteuliwa kufanya shoo siku ya event, kwahiyo nitapata nafasi ya kujitangaza zaidi kimataifa,” alisema AY. Mbali na AY, katika tuzo hizo, Mtanzania mwingine aliyekula shavu awamu hii ni Sara Kaisi ‘Shaa’ (kwenye picha kubwa juu) ambaye yupo ndani ya katika category ya Msanii Bora anayechipukia ambako anang’atana meno na nominees wengine kama MI, STL, Bigiano na Rhythimic Element.

Taratibu za kuwapigia kura AY na Shaa ili waweze kuibuka kidedea, zinatarajiwa kutajwa leo katika mkutano na waandishi wa habari kati ya wahusika wakuu na washiriki hao. Washindi watatajwa Oktoba 10, 2009, Nairobi, Kenya. Unaweza kutembelea website kama www.mama.mtvbase.com au www.mtvmama.mobi 4 more details.
*****************************

Mama’ke Chris Brown atoa sentensi yake kuhusu hukumu
Limesemwa hili na lile kuhusiana na staa wa R&B na Pop anayeminya kwenye himaya ya Obama, Chris Brown lakini mama yake alikuwa hajanena kitu kuhusiana na hukumu ya mwanaye.

Wiki iliyopita, mama wa Chris, Joyce Hawkins alitoa sentensi kadhaa kuhusiana na matatizo ambayo mwanaye ameyapata. Joyce aliviambia vyombo vya habari kuwa anawashukuru mashabiki wote wa Chris kwa kumfariji katika kipindi hiki kigumu.

Alisema: “Nasema kutoka moyoni, nashukuru kwa kuwa karibu na mwanangu, nilishindwa kulisema hili kwa sababu kesi ilikuwa bado inaendelea. Labda niseme tu kwamba tatizo hili limenisumbua na kuniumiza mno katika maisha yangu.” Hivi karibuni, Chris alihukumiwa kifungo cha nje miezi sita, kufanya kazi za kijamii kwa muda wote huo, pia akatakiwa na mahakama kuwa mbali na Rihanna kwa miaka mitano.

Hukumu hiyo ilimfika Chris baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Robyn Rihanna Fenty na kumuumiza. Hata hivyo, inaelezwa kuwa Chris hajutii kosa wala hajaumizwa na hukumu hiyo kwa sababu mara kwa mara anaonekana kiwanja akijirusha bila wasiwasi.

****************************
LL Cool J: Jamaa kacheki na watatu tu!
Ana jina kubwa na heshima tele katika kona za muvi na muziki hasa Hip Hop. Ni Ladies Love Cool James a.k.a LL Cool J.

Mtandao wa kimbeya ambao ume-specialize katika kufunua uhusiano wa mastaa umeambulia orodha kiduchu ya babies waliokwishajikunja naye on the bed. Ni warembo watatu tu ambao wametajwa ku-shear urojo na LL Cool J. Debbie Allen anatajwa wa kwanza lakini hakuna maelezo ya kutosha ni lini alichizika naye.

Simone Johnson anatajwa kuwa alichangamsha damu na mchizi huyo mwenye umbo la miraba minne mwaka 1995. Wakati Kidada Jones yeye alikuwa naye kati ya mwaka 2002 – 03. Kwa mujibu wa mitandao mingine Simone ndiyo mke halali wa LL Cool J ambaye amefanikiwa kuzaa naye watoto kadhaa.

Hii ni orodha fupi kutokana na staili ya mastaa kupenda kubadili wapenzi kama disposable instrument. Inawezekana pia akawa si msafi kihivyo, ila anajificha kwa sana. Jina lake kamili ni James Todd Smith, alizaliwa Januari 14, 1968, Queens New York, Marekani. Ana umri wa miaka 41. Ana urefu wa futi 6 1½. Je, wewe msomaji unapenda kujua uhusiano wa staa gani wa kiwanja? Tuandikie ujumbe mfupi 0715-110 173.
*************************
compiled by mc george

1 comment:

Unknown said...

Naomba utuandikie juu ya mahusiano ya kimapenzi ya mgosi Lil Wine, na pia nifahamu amezaa watoto wangapi?