Sunday, June 10, 2018

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AIPONGEZA HOSPITALI YA MAMC-MLOGANZILA KWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) anayemfuatia ni Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa magonjwa ya dharula Dkt. Catherine Shali wakati wa
ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu,  Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipata maelezo katika mashime ya MRI wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) akipanda ngazi za umeme.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (mwenye kilemba cha bluu) na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kulshoto) wakimsikiliza Mkuu wa Skuli ya Meno-MUHAS Dkt. Elison Simon wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akitoa maelekezo kwa Meneja wa Maabala Glory Mmbando wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa wakuu wa vitengo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Amani Ahmada mwenye umri ya miaka 6, wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza machache.
Wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini.
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kutolea machache ufafanuzi.
Picha ya pamoja na uongozi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Picha ya pmoja na wafanyakazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza wananchi wanaopata huduma ya matibabu Mloganzila wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Huduma za Hospitali, Prof. Said Aboud akitolea ufafanuzi malalamiko ya wananchi wanaopata huduma katika hospitali ya Mloganzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameupongeza ungozi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila kwa juhudi wanazokabialiana nazo katika kutatua changamoto wanazokabilia nazo. Mhe. Suluhu ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila. Makamu wa Rais amesema kwa vifaa vya kisasa vya umeme vilivyopo hospitalini hapo havipaswi kupata umeme wa mashaka . Makamu wa Rais amesema kuwa wananchi wengi hawajajua umuhimu wa kuwa na bima ya afya hivyo elimu zaidi itolewe ili wananchi wengi wachangie huduma ya afya kwa kupitia bima zao hii itawapunguzia gharama sana wakati wa matibabu. Makamu wa Rais aliutaka uongozi wa Mloganzila kutangaza kwa wananchi huduma zinazopatikana hospitalini hapo ambapo wana vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi wa afya, Makamu wa Rais alisema huduma ya kupima saratani ya matiti katika hospitali ya Mloganzila ni shilingi elfu 30 tu. Akiongea na Watumishi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais amesema “ Mnaofanya kazi sekta ya afya mnafanya kazi ya Uunguzi na kujitolea malipo yetu yapo kwa mwenyezi Mungu” Makamu wa Rais pia aliwasikiliza wananchi waliofika kwenye kupata huduma hospitalini hapo na kusema kuwa Serikali itajitahidi kushughulikia changamoto zinazojitokeza lakini aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya. Mapema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimuambia Makamu wa Rais kuwa (MAMC) Mloganzila ni kati ya hospitali saba zinazomilikiwa na serikali ambazo zinatoa huduma za matibabu ya kibingwa ngazi ya juu pia alimpongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuweka msukumo wake katika huduma ya mama na mtoto ambapo juhudi za Makamu wa Rais zimezaa matunda ambapo leo hii kuna vituo 208 vimeboreshwa na kutoa huduma

No comments: