Thursday, August 27, 2009

Zijue faida za kufunga kiafya

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ndiyo umeshawadia na waislamu wako kwenye funga ya muda wa siku 30 au 29 kuanzia Jumamosi iliyopita. Kama tujuavyo, funga ni nguzo ya nne miongoni mwa nguzo tano za uislamu, ambapo ni lazima kufunga kwa mtu mzima na mwenye afya njema.

Kuna funga za aina nyingi, lakini kubwa ni ya kiroho ambayo waumini hufunga kwa ajili ya kutii maamrisho ya Mungu, ingawa ufungaji wake unatofautiani kutoka dini moja hadi nyingine. Wakati waislamu wanafunga kwa kutokula kitu chochote kuanzia asubuhi hadi jua linapozama, wakristu wao wakati wa funga huruhusiwa kula, lakini kwa kiasi na utaratibu maalum.

Tunaposikia neno kufunga, wengi tunaliangalia tendo hilo kwa upande wa kiroho kuwa ni amri ya Mungu ambayo tunapoifuata tunapata thawabu. Funga pia huchuku?iwa kama njia moja wapo ya kufanya maombi maalum kwa Muumba ili kujibiwa maombi yetu kwa namna ya kipekee.

Kama ambavyo mtu akifunga na kufuata sawasawa mafundisho yote ya funga anavyopata fadhila kutoka Mungu, ndivyo ambavyo pia mtu huyo anaweza kupata faida za kimwili kutokana na funga hiyo.
Katika ulimwengu wa sasa, funga imegundulika kuwa njia bora ya kupambana na maradhi mbalimbali na hatari mwilini, ambayo katika hali ya kawaida yameshindikana kutibika kwa kutumia tiba za kisasa.

Ingawa funga inaonek?na kama ni ibada fulani ngumu kwa baadhi ya watu, lakini Mungu bila shaka alikuwa na siri kubwa na aliamrisha tufunge kwa faida ya miili yetu na pengine kama watu wote wangekuwa wanafunga kama inavyotakiwa, bila shaka maradhi mengi yangepungua.

NINI FAIDA ZA FUNGA KIAFYA?
Faida za kufunga za kimwili ziko nyingi, zikiwemo kuponya mwili. Unapofunga una upa nafasi mwili wako kupumzika na kujitengeneza upya wenyewe. Funga inaupa nafasi mwili kuondoa sumu sehemu mbalimbali za mwili ambazo zilijijenga kwa muda mrefu.

Halikadhalika funga hufufua upya chembecheme hai za mwili, huboresha mfumo wa hewa. Tofauti na imani kuwa mtu mwenye njaa hukosa nguvu, funga huongeza nguvu za mwili na uchangamfu wa akili pia.
Baada ya wataalamu mbalimbali wa sayansi kugundua kuwepo kwa faida kubwa ?a kufunga, wamebuni funga zingine zenye lengo la kuboresha afya tu na siyo kwa mambo ya kiroho. Kuna aina nyingi za funga, kama vile kufunga kula vyakula vyote isipokuwa juisi ya matunga tu kwa siku kadhaa.

Aina nyingine ya funga ya tiba ni ile ya kufunga kula vyakula vyote, isipokuwa kunywa maji peke yake kwa muda maalum. Funga za aina hii huwa ni za muda maalumu zikiwa na lengo maalumu, ama kupunguza uzito, kutibu shinikizo la damu, kisukari ama magonjwa mengine. Hata hivyo inashauriwa mtu kujijua hali yake ya kiafya kwanza kama kabla ya kufunga.

Hivyo, ni ukweli ulio wazi kuwa waislamu au wakriostu wanapofunga ili kutekeleza amri ya Mungu, wanapata faida nyingine ya kiafya bila wao kujijua. Hata utafiti wa kawaida nchini unaonesha kuwa watu wanaofunga hali zao kiafya huimarika sana katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani na hata idadi ya wagonjwa huripotiwa kupungua hospitali.
JE, FUNGA INAFANYAJE KAZI MWILINI?
..itaendelea wiki ijayo

(Samahani sana wasomaji wangu wa makala haya, kwa kuchelewa nilighafirika, nilidhani nilishapost)

No comments: