Saturday, September 19, 2009

BINTI WA MFALME TAJIRI DUNIANI!!


Anaitwa Majeedah Nuurul Bulqiah, mwenye umri wa miaka 33, ni Binti wa Mfalme Hassanal Bolkiah wa Brunei. Crown aliyoivaa imetengezwa kutokana na dhahabu ya hali juu (pure glod) na almasi tu.

Hii ilikuwa ni siku ya harusi yake Juni 2007, sherehe ambayo inaelezwa ilitumia zaidi ya dola za Kimarekani milioni 5 kwa siku 14. Binti ana masters ya Mazingira kutoka Uingereza. Mume ni mtumishi wa umma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Mfalme Hassanal ni miongoni mwa watu matajiri dunaini na inaelezwa kuwa Brunei ni nchi tajiri kuliko nyingine barani Asia, watu wake hawalipi kodi, elimu na matibabu ya hali juu hutolewa bure kabisa. Ni nchi ndogo sana, isiyozidi watu 500,0000. Utajiri wao mkubwa unatokana na mafuta na gesi asilia ambayo haipatikanani sehemu nyingine duniani - kwa kifupi huko ni pepo ya dunia.

6 comments:

ginfizz said...

kaka mrisho hiyo nchi ni ya kwanza kwa utajiri dinian pamoja na watu wake hakuna rushwa wala EPA kule kipata cha mtu mmoja mmoja kina zidi cha mtu wa marekani kwa siku lakini hawana mashauzi kimya kimya
na nchi yenye magari mengi ni duniani ni Australia inakadiliwa watu wawili umiliki gari moja.bye bye Eid Mubaraka kaka

Anonymous said...

duh! kumbe kuna faa huko brunei kwa boxi.maana kwote sasa hivi boxi adimu jamani vipi wana ubalozi dar haojama wa bruneoo??

mdau msaka boksi

Anonymous said...

SAWA Lakini hao juu ni watu wawili tofauti baba!

Anonymous said...

kaka kunaingilika huko?
heheheeeee! au ndio huioni pepo mpaka utende mema....

Ibra said...

Kujilipuwa vpi?kesi gani zinafaa??Kirundi kisomali au kizimbabwe?Pablo machine umesikia hii??au umeshikika na ndombolo hapo Sweden tu?Ibra.

Anonymous said...

Huko kuna nchi ambazo wenyewe wanaruhusu kuingia sio watu kutoka nchizozote duniani na unalimitiwa mji wa kufikia hawachui wakimbizi wala nini ni wenyewe tu